Vijana wa Romania Vijana wa Romania  (Vatican Media)

Papa kwa vijana,Romania:Muwe hodari wa imani,tumaini na bila kuchoka upendo

“Katika ulimwengu uliopotea na usio na matumaini mnaitwa kuwa nuru ya ulimwengu na chumvi ya dunia.Tumaini la Kikristo si matumaini tu bali ni uhakika unaotegemea uaminifu wa Mungu.Yesu Kristo,Mfufuka,ndiye tumaini letu!Kwake kila kitu kinawezekana.”Ni maneno ya Papa katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 15 wa kitaifa wa vijana wakatoliki nchini Romania kuanzia tarehe 4-7 Septemba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko aliandika katika barua vijana wa Romania waliokusanyika kwa ajili ya toleo la 15 la Mkutano wa Kitaifa wa Vijana Wakatoliki. Barua hiyo iliwasilishwa na Balozi wa Vatican huko Romania, Askofu Mkuu Giampiero Gloder katika Mkutano wa Vijana ulioanza jioni ya tarehe 4 Septemba 2024  huko Cheile Gradistei (Brasov) na kulimalizika tarehe 7 Septemba 2024, ukiwaleta pamoja vijana 1,200 kutoka majimbo na makanisa yote ya Kanisa Katoliki nchini Romania. Katika Ujumbe huo, Baba Mtakatifu aliandika kuwa “Wapendwa vijana, nawasalimu kwa upendo. Ni furaha kubwa kujua kwamba mmekusanyika kuishi nyakati za sala, udugu na kutafakari juu ya imani yetu ya pamoja.” Kwa kuongeza, Baba Mtakatifu alindika kuwa “Katika ulimwengu uliopotea na usio na matumaini mnaitwa kuwa nuru ya ulimwengu na chumvi ya dunia. Tumaini la Kikristo si matumaini tu, bali ni uhakika unaotegemea uaminifu wa Mungu. Yesu Kristo, Mfufuka, ndiye tumaini letu! Kwake kila kitu kinawezekana”.

Kuweni imata katika imani

Baba Mtakatifu Francisko aliwahimiza vijana kushuhudia imani yao kwa furaha, kuwa Wakristo halisi, na kutumia mitandao ya kijamii “kueneza ujumbe wa upendo, amani na matumaini ya Injili”: “Kuweni washawishi wa imani, mkileta nuru ya Kristo ndani ya nafasi halisi ambapo vijana wengi hutafuta majibu, mifano ya kuigwa na maana!”. “Kuweni imara katika imani, hodari katika tumaini na bila kuchoka katika upendo! Songa mbele kwa kujiamini na endelea kuwa mashahidi wa furaha na matumaini ya Kikristo!”, Papa aliongeza huku akiwahakikishia vijana ukaribu wa Kanisa na kuwataka wamuombee.

Ujumbe wa Papa kwa vijana wa Romania
09 September 2024, 15:24