Tafuta

2024.09.09 Ziara ya 45 huko  Papua Nuova Guinea - Kukutana na vijana katika Uwanja wa SIr John Guise. 2024.09.09 Ziara ya 45 huko Papua Nuova Guinea - Kukutana na vijana katika Uwanja wa SIr John Guise.  (Vatican Media)

Papua New Guinea:Historia za imani

Historia na uzoefu wa watu wengi tofauti imengeneza mikanda tofauti ambayo inawakilisha ziara ya Papa Francisko huko Papua New Guinea.

Na Linda Bordoni - Dili

Nilipoondoka Port Moresby siku ya Jumatatu, mwishoni mwa ziara ya siku tatu ya Papa Francisko huko Papua New Guinea, akili yangu ilikuwa imejaa picha na hisia na kumbukumbu za nchi isiyo ya kawaida. Lakini nilipofikiria kwa kina, ni historia mbili zilikaa akilini mwangu. Hizi ni historia za watu kibinafsi za kawaida ambazo nilikutana nazo nilipokuwa nikizungumza na kila mtu aliyesimama karibu nami katika baadhi ya matukio ya papa. Nilikuwa nimesafiri hadi Vanimo alasiri kufuatia Misa katika Uwanja wa Port Moresby na nilikuwa nimesimama kwenye jua kwa muda mrefu sana. Kulikuwa na joto na miguu yangu ilikuwa imechoka nilipomwona mwanamke aliyekuwa upande wangu wa kulia ameshika picha na medali mbili kifuani mwake. Niliangalia kwa karibu, alijitambulisha, na akaniambia historia yake kwa furaha. Picha ilikuwa zamani aliyoishikilia ambayo ilionesha Papa Paulo VI, akisalimiana na  mwanamume wakati wa kile kilichoonekana kama Katekesi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Nyuso za waamini wa Papua New Guinea
Nyuso za waamini wa Papua New Guinea

Mwanamume huyo, Carol aliniambia, alikuwa babu yake, Mpapua wa kwanza kusafiri hadi Roma na kuhudhuria Katekesi ya  papa mnamo mwaka wa 1975. Katika pindi hicho kisicho cha  kawaida, Papa alimpatia babu yake nishani mbili za Vatican alizoleta, na ambazo zimethaminiwa na familia yake tangu wakati huo. Carol pia aliniambia kuwa alikuwa ametembea kwa siku katika msitu ili kufikia Vanimo na hazina zake ili kuwa na Papa: "Zawadi ya thamani ambayo babu yangu alipokea karibu miaka 50 iliyopita", zawadi ya thamani, aliongeza, "Ninapokea leo. ”

Uliogopa wakati wa safari yako kupitia msitu?" niliuliza. “Hapana” lilikuwa jibu lake: “Mungu alikuwa pamoja nami.” Sista wa Kihindi mmisionari wa Shirika la Mkingwa Dhambi ya Asili alikuwa amesimama kwenye foleni akisubiri kusalimiana na Papa kabla ya mkutano wake na vijana kuanza. Yeye aliniambia alikuwa amekuja Port Moresby kutoka ncha ya kusini kabisa mwa Papua New Guinea ambako amekaa miaka mitano iliyopita akifanya kazi katika misheni na Masista wengine wa PIME. Kila siku, alisema, wanasafiri kwa saa nyingi kwenye mitumbwi katika  bahari iliyochafuka, huku baadhi ya watu wanaowasaidia wakitembea kwa saa nyingi msituni ili kuwafikia.

Wamisionari huko Papua New Guinea
Wamisionari huko Papua New Guinea

Watu hawana lolote. Wanaishi kwenye nyumba ambazo hazina umeme wala maji. Wengi hufariki wakati wa kujifungua au wakiwa wachanga kwa sababu hakuna huduma za afya. Bahari inayoinuka inazidi kukaribia na kukaribia nyumba ya Masista. Aliniambia moja ya malengo yao kuu ni kuwaelimisha watoto amani kwani migogoro ya kikabila inaendelea kusababisha, migogoro, vifo na uharibifu. "Hatufikirii Vanimo ya mbali!" alisema kwa mshangao, “maeneo halisi ya pembezoni, kama yetu, hayawezi kufikiwa.” Lakini yeye ana furaha. Nilipomuuliza kama anaogopa kwenye boti alisema: “Hapana, Mungu yu pamoja nami.”

Papua hisoria za imani zinasimuliwa na Linda Bordon
10 September 2024, 09:19