2024.09.09  Papa Francisko wakati wa Mkutano huko Uwanja wa  SIr John Guise. 2024.09.09 Papa Francisko wakati wa Mkutano huko Uwanja wa SIr John Guise.  (Vatican Media)

Ujumbe wa Papa wa amani na mshikamano utakaa Papua New Guinea kwa miaka

Padre Giorgio Licini,mmisionari wa PIME wa Kiitaliano huko Port Moresby,aliviambia vyombo vya Vatican News kwamba ujumbe wa Papa Francisko wa amani,mshikamano,urafiki na upatanisho utasindikiza watu wa Papua New Guinea kwa miaka ijayo.

Na Claudia Torres – Port Moresby, na Angella Rwezaula – Vatican.

Kufika kwa Papa, Papua New Guinea ni kitu cha kipekee, kitu ambacho hakiwezi kutokea mara kwa mara kwa sababu ya umbali na kwa sababu hii si moja ya nchi muhimu zaidi duniani Padre  Giorgio Licini, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon, alithibitisha hilo katika mahojiano na Vatican News, muda mfupi kabla ya kuanza kwa Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Sir John Guise, Port Moresby, Dominika  tarehe 8 Septemba 2024.

Vijana wakitumbuiza na kucheza katika Ujwanja wa Si John Guise
Vijana wakitumbuiza na kucheza katika Ujwanja wa Si John Guise

Mmisionari wa PIME kutoka kaskazini mwa Italia, Padre Licini amekuwa katika nchi ya Pasifiki ya Kusini tangu 2003, na uzoefu wake umempa ufahamu wa kina wa vikwazo vya msingi ambavyo Kanisa Katoliki hukabiliana navyo huko. Alieleza kwamba “linapokuja suala la kushuhudia Kristo na Injili katika jamii,” masuala ya kijamii yanaleta changamoto kubwa zaidi. Umaskini, kutengwa, na ukweli kwamba watu wengi wanaishi katika vijiji vya mbali sana na ambako shule na vituo vya afya vinakosekana, ni baadhi ya masuala aliyotaja. Padre Licini pia alitaja pia  jeuri na “machafuko, nyakati fulani kutokana na mapigano ya kikabila na masuala ya mila za mababu ambayo watu hao wanaendeleza."

Mkutano wa faragha na wamisionari
Mkutano wa faragha na wamisionari

Mwishowe, alisisitiza kwamba huku umaskini wa mijini ukiongezeka, vijana wengi hujikuta katika hali fulani: “Hawawezi kuona wakati ujao ulio wazi pamoja na ukosefu wa fursa na elimu duni.” Hata hivyo, Padre  Licini anabaki  na matumaini, akiwa na uhakika kwamba “ujumbe wa Papa Francisko wa amani, mshikamano, urafiki na upatanisho utaambatana na watu wa Papua New Guinea kwa miaka ijayo.

Mkutano na wamisionari
Mkutano na wamisionari
Ushuhuda wa Pad Licini
09 September 2024, 14:40