2024.09.11 Vijana wa  Timor Mashariki walikutana na Papa  huko  Dili 2024.09.11 Vijana wa Timor Mashariki walikutana na Papa huko Dili  (Vatican Media)

Vijana wa Timor Mashariki wamefurahishwa na ziara ya Papa

Kulingana na Ricardo Da Costa Belo ambaye ni mjumbe wa Tume ya Kitaifa ya Vijana wa Kikatoliki wa Timor ya Mashariki amebainisha kuwa ziara ya Papa Francisko nchini humo inaweza kuwa na matokeo mazuri ya muda mrefu kwa vijana katika taifa la Asia pia linalokabiliwa na vurugu na uhalifu wa vijana.

Na Padre  Bernardo Suate na  Lisa Zengarini - Dili.

Ricardo Da Costa Belo ni mjumbe wa Tume ya Kitaifa ya Vijana wa Kikatoliki ya Timor ya Mashariki ambaye alizungumza na Vatican News, kupitia mwakilishi wetu Padre Bernardo Suate anayeshiriki Hija ya kitume ya Papa pamoja na wengine,  kuhusu ushiriki wa vijana Wakatoliki wa Timor  ya Mashariki katika maisha na mipango ya Kanisa na pia kuhusu changamoto zinazokabili huduma ya vijana katika taifa hilo changa. Kwa mujibu wake anatumaini hali ya furaha na amani inayozunguka tukio hilo la kihistoria linaweza kuchangia kuleta amani ya muda mrefu na utulivu kwa jamii ya Timor ambayo bado inakabiliwa na ghasia zinazohusisha idadi ya kuishi ya  vijana. Yafutayo ni mahojiano  kamili na Mjumbe  Tume ya Kitaifa ya vijana.

Papa na vijana
Papa na vijana

Je, unaweza kutuambia kuhusu ushiriki wa vijana katika Kanisa la Timor ya mashariki?

Kuna vijana wengi wenye bidii katika Kanisa na mashirika kadhaa ya kiulimwengu ambayo hufanya kazi na vijana. Idadi inayoongezeka ya vijana hushiriki katika shughuli za Kanisa ikijumuisha harakati za Laudato Si, parokia na shughuli za kimisionari. Hata hivyo, upatikanaji wa shughuli za umma zinazofadhiliwa na serikali ni mdogo zaidi kutokana na mapungufu kadhaa, hasa katika maeneo ya vijijini.

Papa alikutana na vijana
Papa alikutana na vijana

Je, ni changamoto gani kuu mnazokabiliana nazo leo hii?

Tunakabiliana na  changamoto nyingi nchini Timor ya Mashariki, hasa zinazohusisha vijana. La muhimu zaidi ni upatikanaji wa elimu.  Viwango vya elimu nchini Timor ya Mashariki bado viko nyuma sana kulinganisha na nchi nyingine, hasa shule za serikali kwa sababu serikali haijaweka elimu kuwa kipaumbele. Tatizo jingine ni kuhusiana na kusambaa kwa gym za karate kwa ajili ya kujilinda ambazo zimekuwa zikipendwa sana na vijana. Sanaa ya kijeshi sio mbaya yenyewe, lakini vijana wengine huitumia kwa malengo tofauti, ya kupigana.

Papa Francisko alikutana na vijana
Papa Francisko alikutana na vijana

Je, unafikiri Papa Francisko ataleta kitu kizuri kwa vijana katika Timor ya Mashariki?

Kama unavyojua, nchi yetu ni ya Kikatoliki na pia vijana kwa sehemu kubwa ni Wakatoliki. Papa Francisko ameleta hali nzuri hapa, hasa kwa vijana wakatoliki. Kabla ya maandalizi ya ziara hiyo tulikuwa na matatizo mengi ya ukatili wa vijana. Lakini habari za ziara hiyo zilipoibuka, jeuri la vijana na uhalifu ulipungua. Kwa hivyo, labda, uwepo wa Papa umeleta amani kidogo kati ya vijana katika nchi hii.

Papa huko Dili na vijana
Papa huko Dili na vijana

Papa alipofika, tarehe 9 Septemba 2024, wengi wa watu waliokuwa mitaani kumkaribisha walikuwa vijana wakatoliki. Walifurahi sana kumkaribisha Papa wetu mpendwa. Baadhi walihamishwa. Na hii ni chanya Tunatumaini kwamba hii itadumu ili amani na utulivu viendelee katika jamii yetu na pia katika Kanisa letu mahalia.

Mkutano wa vijana huko Dili
Mkutano wa vijana huko Dili
Furaha ya Vijana nchini Timor ya Mashariki
11 September 2024, 11:50