2024.09.11 Siku Kuu ya Msalaba Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq 2024.09.11 Siku Kuu ya Msalaba Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq  

Wamoja katika imani:Watu wa Iraq wanasherehekea Sikukuu ya Msalaba Mtakatifu

Katika kitongoji kimoja cha Erbil huko Ankawa,Wakristo Wakatoliki,Waorthodoksi na Waashuri kwa pamoja walitayarisha sherehe katika muktadha wa Sikukuu ya Msalaba Mtakatifu ifanyikayo kila tarehe 14 Septemba ya kila mwaka,huku jamii zikijaribu kujenga upya maisha pamoja kufuatia na ghasia nchini Iraq.

Na Federico Piana na Angella Rwezaua – Vatican.

Wakati wa kihistoria huko Erbil, kaskazini mwa Iraq, ambako huko Ankawa, kitongoji cha mji mkuu wa Kurdistan wa Iraq ulioko kaskazini mwa nchi hiyo, mamia ya Wakristo wanashiriki katika Sikukuu ya Msalaba iliyoanza Jumatatu tarehe 9 Septemba na itaendelea hadi Ijumaa tarehe 14 Septemba ambapo mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Kutukuka kwa Msalaba. Tukio hilo la furaha linadhihirishwa na matumaini makubwa ikizingatiwa kwamba Wakristo wa mila mbalimbali wanakusanyika pamoja kwa ajili ya maadhimisho hayo wakiwa ni Wakatoliki, Waorthodoksi na Waashuri - kwa mara ya kwanza  ambapo wameungana pamoja katika kuadhimisha kumbukumbu ya kutukukuka kwa Msalaba Mtakatifu ambao Bwana wetu Yesu  Kristo  alifia kwa ajili ya ukombozi wa wote.

Tamasha la Msalama Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq
Tamasha la Msalama Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq

Mtazamo wa maadhimisho hayo unasisitizia imani inayowaunganisha Wakristo. Hawa wanasali kila siku katika Kanisa tofauti na kushiriki katika mikutano mbalimbali ya kiutamaduni iliyoandaliwa katika mitaa ya vitongoji, na ambayo inafanywa sherehe na taa maalum na rangi. Matukio yote  hayo ni sehemu ya maandalizi ya Sikukuu kubwa ya kiliturujia ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu, ambayo itafanyika makanisa Ulimwenguni yanayofuata kalenda ya Gregorian au 27 Septemba kwa wale wanaofuata kalenda ya Julian.

Tamasha la Msalaba Mtakatifu huko Erbili nchini Iraq
Tamasha la Msalaba Mtakatifu huko Erbili nchini Iraq

Katika ufunguzi wa sherehe siku ya Jumatatu 9 Septemba, msalaba mkubwa ulibebwa kwa maandamano hadi Kanisa la Ashuru la Mashariki la Mtakatifu Yohane Mbatizaji. Uzito wa maadhimisho hayo ulijidhihirisha katika nyimbo zilizoimbwa na mapadrei na waamini wakiwa wameshika mishumaa mikubwa iliyowashwa, ishara siyo tu ya kusifu na kuabudu bali pia kushirikishana amani. "Makanisa yamekuwa yakiadhimisha ukumbusho huo kila mwaka tofauti. Lakini mwaka huu ni tofauti sana," alisisitiza Padre  Bashar Matti Warda, paroko Jimbo Katoliki la Erbil, ambaye aliandaa hafla hiyo kubarikiwa na Patriaki  Mar Awa III, wa Kanisa la Ashuru la Mashariki, na Maaskofu wa Makanisa ya Syro-Katoliki na Syro-Orthodox.

Tamasha la Msalaba Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq
Tamasha la Msalaba Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq

Katika hotuba yake wakati wa tamasha hilo, Patriaki Mar Awa III alieleza jinsi ambavyo “sherehe ya Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo inawakilisha hatua muhimu katika mpango wa kimungu katika Kanisa la Mashariki. Tunapoutazama msalaba, tunakumbuka mateso ya Kristo, lakini pia ufufuko wake wa utukufu kutoka kwa wafu. Na tunapofanya ishara ya msalaba juu yetu wenyewe, tunatangaza matarajio yetu ya Ujio wake wa Pili na imani yetu katika uzima wa milele."

Tamasha la Msalaba Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq
Tamasha la Msalaba Mtakatifu huko Erbil nchini Iraq

Maadhimisho ya Sikukuu ya Kutukua kwa  Msalaba Mtakatifu yanawakilisha hatua zaidi na madhubuti ya uekumene ambayo Kanisa Katoliki linaipatia umuhimu mkubwa, kama Baba Mtakatifu Francisko alivyothibitisha katika Waraka wake wa Kitume Evangelii Gaudium: “Kujitoa katika uekumene huitikia sala ya Bwana Yesu kwamba 'wote wanaweza kuwa kitu kimoja.'”

Matukio hayo pia yanawakilisha ishara chanya kwa mustakabali wa Wakristo wa Iraq: baada ya muda, vita, machafuko ya kisiasa na kuongezeka kwa Dola ya Kiislamu kumewafukuza maelfu ya Wakristo wa madhehebu yote nje ya nchi. Kwa njia hiyo aida , Monsinyo Bashar Matti Warda mwenyewe, bila kuwepo kwa takwimu rasmi, alitangaza kwamba "katika Iraq yote kuna karibu Wakristo 300,000 waliosalia." Lakini matumaini bado hai licha ya kupungua kwa idadi ya kundi hili, kama tamasha la Ankawa linavyoonekana.

12 September 2024, 13:10