2024.09.20 Mkutano Med24  huko Tirana nchini Albania. 2024.09.20 Mkutano Med24 huko Tirana nchini Albania.  (Arcidiocesi di Tirana)

Kutoka Tirana vijana wanaitwa kuchukua hatua kwa mustakabali wa kidugu

Mkutano "Med24 -Mahujaji wa matumaini ulimalizika nchini Albania ambapo kama"Wajenzi wa Amani", wanapaswa wakabiliane na hatua nne:mpango wa amani na mazungumzo,kukataa ghasia,migogoro na vita.

Na  Beatrice Guarrera na Angella Rwezaula – Vatican

Wito wa kuchukua hatua kwa vijana wa tamaduni tofauti waliokutanika ili kujenga mustakabali wa umoja na udugu zaidi katika Bahari ya Mediterania, ndiyo maana ya mkutano wa Med24 unaomalizika Jumamosi tarehe 21 Septemba 2024 mjini Tirana nchini Albania kufuatia makongamano yaliyopita huko Bari, Firenze na Marseille. Mpango huo unaoitwa Mahujaji wa Matumaini, Wajenzi wa Amani, ulifanyika miaka kumi baada ya Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Albania, uliofanyika tarehe 21 Septemba. Pamoja na programu iliyojaa matukio ya kuendeleza mazungumzo na kushirikiana, kwa Juma la vijana hamsini kati ya umri wa miaka 20 na 35, wa tamaduni tofauti, imani na ukweli, wanaotoka pwani tano za Mediterania ambapo walijadiliana na maaskofu na viongozi wa Kanisa na Kanda.

Udugu ni njia bora za kushida migogoro na sintofahamu

Ikumbukwe Papa katika ujumbe wa video uliotumwa kwa washiriki wa mkutano huo alisema: “Udugu ndio jibu bora tunaloweza kutoa kwa migogoro na kutojali kunakoua", na kwamba ni maneno ambayo yaligusa mioyo ya Waalbania wengi ambao, katika tukio hili, walifungua milango yao kwa wageni wa mkutano huo, na kuthibitisha kuwa "mahali pa maabara ya amani ambayo yanajitokeza kama pekee ya uzoefu wake wa kidini", kama ilivyoelezwa na Askofu mkuu Arjan Dodaj wa Tiranë-Durrës.

Vijana kupokea ujube wa Papa kwa shauku

“Ni furaha kubwa kuona na kusikiliza ujumbe kutoka kwa Papa hasa kwa ajili yetu," alisema Lenida, kijana wa Kialbania mshiriki katika mkutano huo, akizungumza na vyombo vya habari vya Vatican. Lenida alizungumza juu ya ukarimu wa familia unaotolewa na Waalbania wengi kwa vijana waliotoka mbali kushiriki katika Med24 na kwamba alipitia tukio hili kwa shauku nyingi. Kila mtu alifanya alichoweza ili kusaidia: wengine kwa kupanga usafiri, wengine kwa kuwakaribisha nyumbani, na wengine kwa kusafiri hadi majiji mbalimbali nchini Albania. Tumeingoja wiki hii kwa upendo na furaha kubwa." Labda hii ni furaha sawa ambayo inaweza kuonekana machoni pa washiriki mwishoni mwa siku. "Ninaona kuwa wana furaha hata kama wamekuwa na siku nyingi sana," Lenida alisema: "Kwa hivyo, kuwa mahujaji wa matumaini ni kuchukua kitu, kama uvumilivu, amani, uzuri katika mambo rahisi na kuleta ukweli huo mahali unapoishi, kuleta mabadiliko, yaani, kuona mambo kwa njia tofauti, kwa njia nzuri, bila mateso au vita."

Kujenga Ulimwengu wa haki

Njia ya tafakari ya pamoja ya kujenga ulimwengu wenye haki zaidi, kulingana na Padre Massimiliano Maria Spezia, katibu wa Askofu Mkuu Dodaj, inawakilisha "mbegu ndogo iliyotupwa ndani ya mioyo ya vijana hawa ambayo kwa mantiki ya Mungu, kubwa zaidi kuliko mantiki ya mwanadamu, itafanya kuleta matunda yale ambayo Bwana anataka. Lakini tayari tunaziona, tayari tunazifurahia katika udugu, kwa furaha, katika usahili mzuri sana wa udugu. Mkutano huo ulioanzishwa kati ya Makanisa ya Mediterania ni shule ambayo unajifunza hatua kwa hatua na ambapo uzoefu hupitishwa sio sana na mikutano au masomo lakini zaidi ya yote katika mawasiliano ya kibinafsi na uhusiano."

Matembezi katika sehemu za misikiti,makanisa ya Kiorthodox na Katoliki

Viongozi wa dini nyingine, wasomi na mamlaka za kisiasa pia walishiriki katika mpango huo, kama vile spika wa Bunge na waziri mkuu wa Albania. Aina mbalimbali za kidini za Albania pia zilikuwa kitovu cha kutembelea sehemu muhimu za kitamaduni, misikiti na makanisa ya Orthodox na Katoliki, ambayo ilifungua njia ya mazungumzo juu ya amani na mazungumzo kama sehemu muhimu ya maisha ya kijamii. "Kupitia mazungumzo - alielezea Rasha, mhitimu wa Sayansi ya Elimu kutoka Damasco, tunaweza kubadilishana maoni na uzoefu zaidi ya madhehebu, dini na tamaduni. Ni ufikiaji wa kweli wa kiini cha kile ambacho ni binadamu na kwa hivyo mawasiliano ya kweli ya kibinadamu ambayo yanakataa vurugu, migogoro na vita na inakaribisha upendo, amani na kuishi pamoja." Siku ya mwisho ya mkutano ilitengwa kwa ajili ya kutafakari juu ya uzoefu wa wiki; vijana wameandaa orodha ya ahadi za kufikia na kudumisha kwa sababu, kama ilivyoelezwa katika taarifa ya mwisho ya tukio, udugu ni kitu kinachoishi, si tu kinachozungumzwa au kuonekana kwenye televisheni. Ni kitu kinachohisiwa na moyo na kushirikiwa na maisha."

Mkutano wa MED24 umehitimishwa huko Tirana
24 September 2024, 11:03