Papa alitembelea Shule ya Wamisionari ya Irmas huko, Timor ya Mashariki. Papa alitembelea Shule ya Wamisionari ya Irmas huko, Timor ya Mashariki. 

Ziara ya kitume ya Papa,Dili:Moyo wa Injili uko kwenye miisho ya dunia

Papa Francisko alipitia mitaa ya Dili Jumanne asubuhi tarehe 10 Septemba na kutembelea shule ya wamisionari ya Irmas Alma ya watoto wenye ulemavu na kisha kwenye Kanisa Kuu la jiji ili kuwa na maaskofu,mapadre,wanaume na wanawake waliowekwa wakfu,waseminari na makatekista.

Na Linda Bordoni - Dili

Macho yangu yalipotazama kwa kina katika Kanisa Kuu la Dili siku ya Jumanne asubuhi, tarehe 10 Septemba 2024 nilichukua mazoea na kuona kanzu nyingi zikiniambia kwamba idadi kubwa ya waliohudhuria mkutano walikuwa ni mapadre na watawa wamisionari. Nilikuwa nimetoka kwenye ziara ya Papa Francisko tu kwenye kituo cha watoto walemavu kinachoendeshwa na Watawa wa Alma wa Timor ya Mashariki. Nilikuwa nikiwatazama kwa heshima na kuvutiwa walipokuwa wakiwasaidia kwa upendo watoto hao walioweza kuimba na kucheza, huku wakiwashikilia wengine karibu nao. Papa pia alikuwa karibu kwa ishara na maneno na akizungumza katika lugha ya Kihispania ambayo ni lugha yake ya asili, aliwashukuru watawa na watoto “kwa kutufundisha kutunza na kutunzwa.”

Papa wakati wa kukutana na watoto walemavu
Papa wakati wa kukutana na watoto walemavu

Tendo hilo lilikuwa linazidi kuwa dhahiri kwangu kwamba wamisionari, wanaume na wanawake, wanashirikisehemu muhimu katika kuweka pamoja muundo wa kijamii wa Taifa. Kuna maelfu yao, wa mashirikia mbalimbali, ambao huziba pia mapengo ambapo serikali inayumba na mengi zaidi. Wao ni wainjili, walimu, wauguzi na wa matabibu wanaowajali watu walio dhaifu sana katika jamii. Waliwakilishwa vyema katika Kanisa Kuu,na walikuwa na shauku  kutoa ushuhuda wao wa upendo kwa Mrithi wa Petro, ambaye aliwasifu na kuwashukuru kwa kuishi utume wao katika nchi ambayo iko “mwisho wa dunia.

Papa alipokutana na watoto walemavu
Papa alipokutana na watoto walemavu

Kwa kuwa hasa “kuwa kwenye miisho ya dunia, iko katikati ya Injili!” alirudia Papa Francisko. "Asante kwa kuwa pembezoni." Kwa ujumbe mzuri wa ukaribu, aliwaambia, “Ninafurahi pamoja nanyi na kwa ajili yenu kwa sababu ninyi ni wanafunzi wa Kristo katika nchi hii.” Kisha akaweka maandishi yake chini na ili basi kuendelea na mikutano mingine  iliyokuwa inamsubiri na kusema:  "Wanawake ndio sehemu muhimu zaidi ya Kanisa, kwa sababu wanatunza wale walio na uhitaji zaidi, wanawaponya na kuandamana nao." Akikumbuka ziara yake mapema asubuhi kwa "makazi hayo mazuri kwa ajili ya maskini na wahitaji zaidi kati ya kaka na dada zetu", Papa Francisko aliwageukia watawa, na wote waliowekwa  wakfu kuwa, "Kuweni mama wa watu wa Mungu!”

Papa alipokutana na watoto walemavu
Papa alipokutana na watoto walemavu
11 September 2024, 11:34