Ziara ya Papa nchini Papua New Guinea inaweza kubadilisha utamaduni wa mfumo dume!
Na Lisa Zengarini na Claudia Torres - Port Moresby
Baada ya kuhitimisha ziara yake nyeti nchini Indonesia, Baba Mtakatifu Francisko amefika siku ya Ijumaa tarehe 6 Setemba 2024 huko Papua New Guinea, kituo cha pili cha Ziara yake ya 45 ya Kitume Barani Asia na Oceania. Atakaa katika nchi ya kisiwa cha Oceania hadi Jumatatu tarehe 9 Septemba 2024, wakati ataondoka kwenda huko Timor-Leste. Sr Daisy Anne Lisania Augustine ni katibu wa Tume ya Mawasiliano ya Kijamii ya Baraza la Maaskofu Katoliki Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon (CBCPNGSI), pamoja na mratibu wa vyombo vya habari kwa ziara ya Papa.
Sr Daisy alizungumza na Claudia Torres wa Vatican News, mwakilishi wetu katika ziara hiyo kuhusu maandalizi na matumaini yake kutokana na ziara hiyo. Katika kusimulia Sr huyo alishiriki msisimko wake na kusema kwamba alifurahishwa na ukweli kwamba Papa Francisko alichagua Papua New Guinea kama moja ya maeneo yake manne katika Asia na Oceania. Alisema hii kwa mara nyingine tena inaonesha ukaribu wake wa 'Ulimwengu wa pembezoni' ambazo mara nyingi huzungumza juu yake. Kwangu mimi, ni muhimu sana, kwa sababu anachosema ni kwamba "Ninakwenda ambapo watu wangu wako. Nataka kuwa huko pamoja nao." Hivyo anakuja hapa kwa sababu ananipenda kama Mkatoliki." Alisisitiza Sr. Daisy, na kwamba Baba Mtakatifu ambaye amesisitiza mara kwa mara haja ya kutoa utambuzi kamili zaidi wa karama na miito ya wanawake katika Kanisa, anaweza pia kuacha alama chanya katika suala hili kwa jamii ya Papua ambayo bado ina mfumo dume."
Papa anathamini kazi ya wanawake katika Kanisa
Alikumbuka jinsi alivyoshangazwa na maneno ya Papa Francisko na mtazamo wa kirafiki kwake wakati wa ziara ya ad limina ya Maaskofu wa Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon mwezi Mei 2023. Alipogundua kwamba Maaskofu walikuwa wamefika na Mtawa, Papa alimkaribisha kushiriki katika Mkutano wao, ambao kwa kawaida huwekwa kwa maaskofu pekee yao. “Haijawahi kutokea hapo awali,” Sr Daisy alisema. Wakati wa mkutano huo mjini Vatican, alisema, Baba Mtakatifu kwa matani kuwa alikiri uwepo wake, akiashiria umuhimu wa jukumu lake kwa Kanisa la Papua. Alisema kwamba “Mawasiliano huwasaidia watu kuelewa maaskofu wanafanya nini hapa kama wachungaji wa Kanisa,” Sr. Daisy alikumbuka.
Matumaini ya matokeo chanya ya ziara hiyo kwenye jamii ya Wapapua
AKiendelea kueleza alisema "Hafla hiyo, ilinipa matumaini kwamba Papa Francisko anathamini kazi ambayo wanawake wanafanya katika Kanisa. Anaonesha ufuasi kamili, uongozi kamili wa kiongozi mtumishi ambaye anakumbatia kila mtu, hata kama wewe ni mwanamke.” Kwa sababu hiyo, anaamini kuwa ziara ya Papa inaweza pia kuwa na matokeo chanya kwa jinsi wanawake wanavyozingatiwa katika jamii ya Wapapua, ambapo bado hawafurahii usawa na wanaume. “Ninahisi kwamba ziara hii itatuletea matumaini, hasa kwa wale wanawake ambao bado wanakandamizwa katika jamii yetu, kwamba sauti za wale ambao haki zao haziheshimiwi zitasikika, kwa sababu anakuja kwa kila mmoja wetu. Papa Francisko anakuja kusema, nyote ni sawa, nyote ni kitu kimoja. Ninyi nyote ni wa maana machoni pa Mungu.”