Kardinali Mteule,Bessi anawaalika watu kutembea katika roho ya Sinodi
Stanislas Kambashi, SJ na Angella Rwezaula-Vatican
Akiwa ndani ya chumba chake alipofikia na kufanyia kazi ya Instrumentum Laboris, Hati ya kitendea kazi ya Sinodi anayoshiriki, Askofu Mkuu Ignatiu Ignace Bessi Dogbo, wa Jimbo Kuu la Abidjan nchini Ivory Coast alishangazwa na simu zilizomwambia “Auguri" yaani "Hongera." Ilikuwa ni tangazo la habari kubwa ambayo hakuitarajia. Papa Francisko alikuwa ametoka mara tu kutangaza, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, kuteuliwa kwake kuwa Kardinali, alisema akihojiwa na vyombo vya Habari vya Vatican. "Nilishangaa," alibainisha Askofu Mkuu wa Abidjan, ambaye alitoa shukrani na kumshukuru Baba Mtakatifu kwa uaminifu katika nafsi yake. Mwitikio wake kwa mshangao huo ulikuwa Fiat voluntas tua, yaani Mimi hapa utakalo nalifanyike. Sote tuko kwenye huduma ya Kanisa. Kwa hivyo ikiwa Bwana anadhani kwamba mtu yuko karibu na Baba Mtakatifu kumpa ushauri na kuupokea kutoka kwake, anaweza kushukuru tu, pia kumshukuru Baba Mtakatifu kwa dhamana hiyo,” alisema Kardinali Mteule
Kujiamini, licha ya vizingiti
Askofu Mkuu wa Abidjan hakusahau hali yake ya kuwa na mipaka na anategemea neema ya Mungu. Kwa ucheshi, aliibua hali yake ya kimwili wakati wa kikao cha kwanza cha sinodi, cha Oktoba 2023. "Kati ya washiriki wa Sinodi, mimi ndiye pekee mwaka jana ambaye, kama Baba Mtakatifu, nilikuwa na kiti cha magurudumu." Licha ya matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kutokea, Kardinali wa baadaye alibakia kujiamini katika jukumu hili jipya ambalo linaweza kuhitaji kusafiri sana.
Furaha na msaada wa watu wa Ivory Coast.
Watu wa Ivory Coast hawakuficha furaha yao kuu kwa kutangazwa kwa habari hii. Majibu yalikuja kutoka pande zote. "Mwana anayestahili wa Ivory Coast aliondoka kwenda Roma akiwa amevaa zambarau, atarudi amevaa nyekundu," ndivyo tumeweza kusoma kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kijiji chake cha asili, bendi ilicheza kwa hafla hiyo.
Miongoni mwa simu za kwanza, kulikuwa na ile ya Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Robert Beugré Mambé, ambaye Askofu Mkuu Bessi alisema kuwa “amefariji sana". Wajumbe wa serikali na wengine wengi pia walituma salamu za pongezi. “Nchi nzima ina furaha na inasubiri kuona nini kinaweza kuleta mshikamano katika ngazi ya nchi, kwa ajili ya upatanisho," alibainisha mteule huyo. "Kuwa mshauri wa Papa kunafungua nafasi yako, mtazamo wako na moyo wako." Kwa kuona kile kinachotokea duniani kote, tunaimarishwa ili kuwa na manufaa zaidi katika ngazi ya nchi yetu, katika nyanja zote za maisha, kidini na kisiasa, anaamini Askofu Mkuu Bessi.
Ulimwengu ungefaidika kwa kudhibiti ugaidi
Akizungumzia Afrika Magharibi iliyo katika mtego wa ugaidi, Kardinali mteule, anakasirishwa kuona kwamba nchi tajiri kwa maliasili zinakabiliwa na mvutano huo daima. Kwake, alibainisha kuwa ugaidi ni kama adui asiyeonekana, Polyp aina ya samaki majini aliyefunikwa kichwa chini, hata ikiwa tunaweza kukisia zaidi au chini ambapo kichwa chake kiko.” Haya yote, anasikitika chini mtazamo wa Jumuiya ya kimataifa. Kwa mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko, washiriki wa Sinodi na waamini wengi walikusanyika jioni ya Dominika, tarehe 6 Oktoba 2024 katika Kanisa kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, kusali Rozari kwa ajili ya amani duniani.
Kwa upande wa Askofu Bessi, alisema ni faraja kuona kwamba, Baba Mtakatifu anashiriki mahangaiko ya kanda ndogo ya Afrika Magharibi anakotoka, na wasiwasi wa nchi zote zilizo katika hali ya vita. Zaidi ya hayo, hakuficha ukiwa wake kuona kwamba ulimwengu mzima hauwezi kudhibiti ugaidi, akijua kwamba amani katika maeneo haya yaliyoharibiwa itakuwa na manufaa kwa mahusiano na ushirikiano wa kushinda. “Tuna maoni kwamba ulimwengu wote umedhoofishwa na ugaidi. Mamlaka kubwa tunazozijua, ambazo zina uwezo wote wa kudhibiti kila kitu kwa sekunde chache, zijitahidi kufanya” hivyo alidokeza huku akitoa wito.
Askofu wa kisinodi
Askofu Mkuu Bessi ametajwa kuwa Kardinali huku Kanisa likitafakari juu ya sinodi, kwa ushiriki wake wa moja kwa moja. Kwake yeye, “ni ishara kwamba Bwana anamwalika kuendelea kuwa askofu wa kisinodi, na askofu anayesikiliza. Kusikiliza roho ambaye anazungumza na Kanisa lake na ambaye anazungumza kupitia, hata aliye mdogo kabisa.” Askofu hajui kila kitu, alitangaza, huku akiibua waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi, katika sura yake ya pili, aya tatu za kwanza: “Wahesabuni wengine kuwa bora kuliko ninyi wenyewe ...".(Fil 1,3...).
Mtazamo huu, anafikiri kwamba ni wa msingi, kwa kadiri ambayo Mungu ameweka ndani ya kila mtu uzuri fulani. Tunapoelewa hili, tunabaki kuwa wasikivu kwa wengine, mapadre, walei, watu waliowekwa wakfu, tunasikiliza kile ambacho Mungu anaweza kutuambia kupitia kwao na tunapokea kile wanacholeta kwa Kanisa,” alisisitiza. Roho hii ya sinodi iliambatana hasa na Askofu Mkuu Bessi alipokuwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Ivory Coast. Kisha alikuwa na akili ya kuwaleta pamoja wenzake wote kutafakari maono na mpango wa pamoja, badala ya kuendeleza mpango mkakati wowote wa kibinafsi. Ni katika kipindi hicho ambapo Baba Mtakatifu alitoa wito wa kutafakari utume wa Kanisa kama ushirika na ushiriki.