Tafuta

Masalia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu Msimamizi wa Utume wa Kimisionari duniani. Masalia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu Msimamizi wa Utume wa Kimisionari duniani.  (AFP or licensors)

Marekani:Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu kitovu cha Novena ya Siku ya Kimisionari

Katika kuelekea Siku Kuu ya Kimisionari tarehe 20 Oktoba 2024,Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa(PMS)kwa kuungana na Wakristo wa Marekani wanashirikisha programu ya maombi iitwayo‘Hallow’’yaani ruhusu’ inayotoa fursa ya kujiunga kimataifa tangu tarehe 11 Oktoba 2024,katika Novena maalum kwa maombezi ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu,Msimamizi wa Utume wa Kimisionari.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika maandalizi ya Dominika Kimisionari Ulimwengu, itakayofanyika tarehe 20 Oktoba 2024, Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa(PMS) kwa kuungana na Wakristo wa Marekani  wanashirikisha programu ya maombi iitwayo: ‘Hallow’ yaani ’ruhusu’ ambayo inatoa fursa ya kujiunga kimataifa kuanzia tarehe 11 Oktoba 2024, katika Novena maalum kwa mamombezi ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu, Msimamizi wa Utume wa Kimisionari hata bila kugusa nchi yoyote ya kimisionari na ambaye katika maisha yake yote yalilenga“kupenda na kumfanya Yesu apendwe.” Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu alikuwa na upendo Mkuu wa Kimisionari hadi kuandika maneno kwamba: “Ningependa kuwa mmisionari, sio tu kwa miaka michache, lakini ningependa kuwa mmoja tangu kuumbwa kwa ulimwengu na kuwa mmoja hadi mwisho wa dunia,”(rej. Historia ya Roho ya Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu.)

MTAKATIFU TERESA WA MTOTO YESU MSIMAMIZI WA UTUME WA KIMISIONARI
MTAKATIFU TERESA WA MTOTO YESU MSIMAMIZI WA UTUME WA KIMISIONARI

Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (Kitengo cha Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa maalum mapya), ataongoza Novena kwa lugha ya Kiingereza, akipendekeza tafakari za kila siku za kuambatana na sala. Miongoni mwa wale kutoka mtandao wa kimataifa wa PMS ambao watahusika katika Novena pia kuna Sr. Regina da Costa Pedro, Mkurugenzi wa kitaifa wa PMS, Brazil, ambaye ataongoza Novena kwa lugha ya Kireno na Padre José María Calderón, mkurugenzi wa kitaifa wa PMS Hispania, ambaye ataongoza Novena kwa  lugha ya Kihispania. Novena itaakisi maisha ya Mtakatifu Teresa na kujitolea kwake kwa kina katika kueneza Injili kupitia matendo madogo madogo ya upendo. 

Mtakatifu Teresa ajulikanaye kwa matendo kama "Njia Ndogo" ni kati ya watakatifu wanaopendwa sana kati ya Wakatoliki Ulimwenguni kote. Kwa njia hiyo itawezekana kushiriki katika Novena kwa kutumia programu ya ‘Hallow,’ ikiwaalika washiriki kutoka duniani kote kusali pamoja katika lugha zao za asili shukrani kwa ushirikiano wa mtandao wa kimataifa wa PMS.

MT.TERESA WA MTOTO YESU MSIMAMIZI WA UTUME WA KIMISIONARI DUNIANI
MT.TERESA WA MTOTO YESU MSIMAMIZI WA UTUME WA KIMISIONARI DUNIANI

Kwa kupakua programu, watumiaji wanaweza kufikia maombi ya kuongozwa, tafakari za kila siku na vipengele maalum kwa ajili ya safari ya kiroho na walinzi wa utume wa Kimisionari. Washiriki wanaweza pia kufuata novena kupitia njia za kijamii za Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa ya Marekani:(Instagram, Facebook, X e LinkedIn).  

09 October 2024, 10:52