MWENYEHERI CARLO ACUTIS. MWENYEHERI CARLO ACUTIS. 

Mama Carlo Acutis:Mtoto wangu ni mfano wa amani katika ulimwengu wa vita

Katika siku ya kumbukumbu ya kiliturujia ya kijanamwenyeheri Carlo Acutis tarehe 12 Oktoba,ambaye alitumia maisha yake kupenda Ekaristi na kuwahudumia wengine.Mipango ya Novena na sala duniani kote vilifanyika na vile vile mahali patakatifu huko Asisi,ambapo mwili wake unapumzika.Mama yake ametoa ushuhuda kwa Vatican News.

Na Federico Piana na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 12 Oktoba ni siku maalum ya kipekee kwa sababu Kanisa zima limeadhimisha kumbukumbu ya kiliturujia ya Mwenyeheri Carlo Acutis, kijana aliyenyanyuliwa kuwa Mwenyeheri katika Altare  ya Bwana, baada ya maisha mafupi ya kuwatumikia wengine na kupenda Ekaristi na Kanisa. Ni maalum kwa sababu katika sayari nzima, katika saa hizi, kuna parokia na makanisa mengi ambayo, kwa heshima yake, misa zinaadhimishwa na kusali rozari au novena zimefanyika kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu hii.

Misa na muziki

Katika Madhabahu ya kuvua nguo huko Assisi, ambapo mwili wake unapumzishwa kati ya sala na maombi katika ulimwengu, mipango ya kusherehekea na kumkumbuka ilianza siku nne kabla kwa kuwa na  wakati wa sala na tafakari, muziki na hata mazungumzo kwenye ya pande zote juu ya dhiki ya vijana. Kwa njia hiyo asubuhi tarehe 12 Oktoba 2024 katika Madhabahu hiyo, misa  iliadhimishwa na Ndugu Simone Calvarese (OFMcap ), Msimamizi wa Conventi wakati Mi nyingine ya jioni ni Askofu Mkuu  Domenico Sorrentino, wa Jimbo Kuu Assisi - Nocera Umbra - Gualdo Tadino na Askofu wa Foligno. Pia katika madhabahu hiyo, maombi na sala yalifuata tamasha la Martín Valverde, mwanamuziki mashuhuri anayezungumza Kihispania.

Nimefurahi kukumbuka uhusiano wake na Maria"

Uamuzi wa kuacha ukumbusho wa kiliturujia katika  siku hii haukuchukuliwa kukumbuka kuondoka kwake kuelekea Mbinguni tu ambako kulitokea katika tarehe 12 Oktoba 2006, wakati Carlo alikuwa na umri wa miaka 15, bali pia  tarehe hii  nchini Hispania ni maadhimisho ya Mama Maria wa  Pilar na huko nchini Brazil  pia  Mama Yetu wa Aparecida na inapendeza kutambua uhusiano huu kati ya Carlo na Maria ambao ulikuwa sifa yake katika maisha yake yote. Alisisitiza hayo Antonia Salzano, mama yake Carolo na ambaye ni shuhuda  mwenye shauku wa Kristo ambaye alieleza  kwa vyombo vya habari vya Vatican wakati  mtoto wake atatangazwa wakati wa Jubilei ya 2025.

Ibada isiyo na mipaka

Na ikiwa tarehe 11 Oktoba 2024 jioni Jimbo Kuu la  la Milano Italia pia lilitaka kumkumbuka na sherehe ya Ekaristi katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Siri  ambapo Carlo  alikuwa anakwenda kila siku na ambapo aliweza kukuza moja ya misemo maarufu na ya kina kwamba: "Ekaristi ni njia yangu kuu ya Mbinguni,"  mtu lazima akiri kwa furaha kwamba kujitolea kwa mwenyeheri kumevuka kila mipaka. "Kutoka Japan hadi China, kutoka India hadi Afrika, kutoka Amerika hadi Australia: katika mabara yote wanaomba na kumgeukia Carlo" alisisistiza mama yake Carlo na ambaye haachi kufikiria jinsi ambavyo maonesho ya miujiza ya Ekaristi iliyoundwa na mwanawe katika Tovuti sasa inaendelea kutua katika parokia nyingi kila kona ya Dunia, kwa mfano huko Marekani pekee kuna maelfu ambayo ni lazima tuongeze kampasi 100 za vyuo vikuu. "Mwanangu hakika atafurahi kwa sababu mara nyingi alirudia kusema kwamba ilimuumiza kuona picha hizo zikionesha foleni nyingi kwenye matamasha na viti vitupu mbele ya maskani."

Uwongofu wengi

Mama Antonia Salzano hata hivyo hatilii tena maanani juu ya  habari za madai ya miujiza na uongofu unaofurika wa chama cha Marafiki wa Carlo Acutis ambacho alianzisha ili kuunga mkono Mchakato wa kutangazwa kuwa mtakatifu: "Barua hufika kika siku. Sijui kama kweli ni miujiza au uongofu. Watu huandika kutoka  ulimwenguni kote ambao walikuwa na shida kubwa na ambao walitatua kwa kumgeukia Carlo: wanawake wengi ambao hawakuweza kupata watoto, wanandoa ambao walikuwa wakitengana. Lakini pia watu wanaodai kuwa wameponywa uvimbe. Bila shaka, hatuwezi kuzithibitisha lakini tunaweza kuzingatia jambo moja: ripoti zinazidi kuongezeka. Siku hii ambapo hakuna taifa lolote lisilo adhimishwa mwenyeheri," Alisema  mama yake Carlo na kwamba  kwa upande wa Carlo kama kielelezo cha amani kwa ulimwengu uliosambaratishwa na vita: “Alipenda kila mtu, hakutofautisha asili na dini. Katika mazishi yake, Kanisa lilikuwa limejaa, hata nje, na watu wasio na makazi, raia wasio wa Ulaya watu wa rangi zote. Carlo hakuzipatia uzito tofauti, alitazama kila mtu kwa macho ya Bwana na  Ulimwengu unapaswa kuzingatia na kufuata mfano."

12 October 2024, 16:00