Mwenyehei Carlo Acutis:Yesu pekee,kwa kutuunganisha na yeye mwenyewe,hutufanya kuwa 'asili na sio nakala' na huru kweli. Mwenyehei Carlo Acutis:Yesu pekee,kwa kutuunganisha na yeye mwenyewe,hutufanya kuwa 'asili na sio nakala' na huru kweli.  

Ask.Sorrentino(Assisi),Mwenyeheri Acutis:sala kwa matazamio ya kuwa Mtakatifu,"Tabasamu la mbinguni"

Utakatifu wa Carlo Acutis ulipitia matendo madogo:kazi ya nyumbani,shuleni,mechi,kutembea milimani na kuunda clip kwenye mtandao.Alisema hayo Askofu Mkuu Sorrentino wa Assisi na kutoa sala ya kuomba ili atangazwe Mtakatifu:”Carlo,tabasamu la mbinguni kwa ajili ya nchi hii iliyojeruhiwa na isiyo na amani,tunamsifu Mungu kwa maisha yako rahisi."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi jioni tarehe 12 Oktoba 2024  Askofu Mkuu Domenico Sorrentino, Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Assisi-Nocera Umbra-Gualdo Tadino na Foligno, aliongoza Ibada ya Misa Takatifu ya kumbukumbu ya kiliturujia ya Mwenyeheri Carlo Acutis, katika Kanisa la 'Santa Maria Maggiore'- Mtamatifu Maria Mkuu, kwenye Madhabahu ya (Spogliazione), kuvua nguo hukoAssisi, ambapo Mwenyeheri wa Milenia amezikwa hapo. Katika mahubiri yake, Askofu Mkuu Sorrentino alisema: "Vurugu na vita, bado vinafanyika kwa kiwango kikubwa, inaonekana kutuambia kwamba utamaduni wa kifo unashinda utamaduni wa maisha duniani. Kiukweli, licha ya kila kitu, mwanadamu anahitaji lisilozuilika la maisha. Anataka maisha kamili, hasa yaliyojaa furaha. Na hajaridhika na wakati mdogo: anataka kuishi milele. Carlo, alipenda maisha katika kila maana. Kila kitu kilikuwa kipenzi kwake, kutoka katika asili hadi kwa mchezo, kutoka katika muziki hadi kwenye kompyuta. Hata hivyo, alielewa kwamba mambo ya dunia, ingawa ni mazuri, ni ya muda mfupi tu."

Gwiji wa Internet Carlo Acutis
Gwiji wa Internet Carlo Acutis

Askofu Mkuu Sorrentino aliendelea kusema kuwa: “Jibu la Yesu kwa kijana tajiri lilikuwa limeingia moyoni mwake: ukitaka uzima wa milele, zishike amri. Na Carlo alishika amri za Mungu. Aliziishi, jinsi zilivyo, na sio minyororo hiyo, bali ishara zinazohakikisha maisha yetu kwamba yana upeo na lengo! Carlo, kama Francis wa Assisi, alimchagua Yesu na kuhisi kwamba Mwenyeji Mtakatifu ni Yesu kweli, wa kukutana, kuabudiwa, kuliwa na kuwa mmoja naye. Unapokutana na Yesu, maisha yako yote hubadilika. Mambo tunayofanya hayabadiliki, yanabadilisha jinsi tunavyoyafanya. Mambo yanabaki sawa, lakini yananukia kama mbinguni.” Kadhalika aliongeza Askofu Mkuu huyo, kuwa: “Yesu ni harufu ya mbingu" Aidha akibainisha kuwa "Inawezekana kuwa, kama ilivyokuwa katika maisha ya Carlo, kazi ya nyumbani ya shule au mechi ya mpira wa miguu, wimbo unaochezwa kwenye saxophone au kutembea milimani, kuunda Clip ya video au kushiriki katika majadiliano, kupeleka mbwa matembezini au kuongozana na mama  yake kwenda kununua vitu sokoni, sawa Bi Antonia?” aliuliza Askofu Mkuu akimgeukia Mama wa Mwenyeheri Carlo aliyekuwepo kwenye Misa hiyo Takatifu.

Siku ya kutangazwa mwenyeheri Carlo Acutis
Siku ya kutangazwa mwenyeheri Carlo Acutis

Askofu Mkuu wa Assisi alisema kuwa "ni mambo ya kila siku, yaani mambo madogo ya kila siku, ambayo kila mmoja wetu kwa njia moja au nyingine ameitwa kufanya, lakini zaidi maisha haya ya kila siku yanabadilishwa na ya milele. Kuweka umilele katika vitu vidogo na vinabadilishwa sura, kuwa mbinguni na kuiakisi, alisisitiza Askofu Mkuu Sorrentino kwamba hata kwenye kitanda cha hospitali, wakati unakaribia kufa kama ilivyotokea kwa Carlo, ndani ya majuma mawili. Kilichotokea hapa kinaweza kutokea, ambapo Francis, ambaye alikuwa amejivua kila kitu, alikaa siku nyingi mwishoni mwa maisha yake kabla ya kushuka Porziuncola kukutana na 'dada Kifo'. Hapa, aliwataka Ndugu Wadogo waliomzunguka kuimbawimbo wa ‘Ndugu Jua’ bila kuacha. Hata Carlo, aliyenyang'anywa ndoto zake zote na mali zake zote za kidunia na saratani ya damu, alijiachia na kukumbatiana na Yesu. Carlo aliombwa kujiruhusu kuvuliwa hata maisha na ujana wake, kufanya na Yesu kazi mbayo ni ya ajabu kutoka mbinguni, sio duniani, kama mshawishi wa utakatifu, wa furaha, na wa maisha kamili.”

Kipaumbele cha kuabudu kwa Mwenyeheri Carlo Acutis
Kipaumbele cha kuabudu kwa Mwenyeheri Carlo Acutis

Neema ya Mungu ilitaka kutangazwa kwa utakatifu kufanyike katika mwaka wa Jubilei ambao utaanza miezi michache ijayo alisema hayo  mahubiri Mwanzoni mwa misa kwamba kuna matarajio makubwa ya kujua tarehe ya Kutangazwa kuwa Mtakatifu mnamo 2025, ambapo Jubilei inaadhimishwa, itakuwa mwaka ambao tutalazimika kupona, kulingana na mada iliyooneshwa na Papa, tumaini lililowekwa kwa Yesu ndiye tumaini la kweli la wanadamu. Carlo bado ni Mwenyeheri. Lakini sasa ishara kutoka mbinguni imefika, ili aweze kutangazwa Mtakatifu. Ishara ambayo ilifika kwa kupona kwa msichana kutoka Costa Rica ambaye niliweza kukutana naye, kama mwimbaji kutoka Costa Rica, Martin Valverde, itatukumbusha baada ya saa chache."Carlo “kwa hiyo hivi karibuni atakuwa 'Mtakatifu' Carlo. Lakini hadhi hii haitatusukuma kwa urefu usioweza kufikiwa. Badala yake, tutaendelea kuhisi, kama vile rafiki anavyohisiwa kwa urahisi, yaani Carlo! Kwa sababu hiyo, Askofu Mkuu Sorrentino alisisitiza kuwa ni "vyema kutunga, kwa kuzingatia kutangazwa kuwa Mtakatifu, sala mpya, ambayo inamwonesha Carlo katika sifa za tabia yake. Maombi ambayo tunaweza kusali kuanzia wakati huu na kuendelea," alihitimisha  mahubiri kwa sala hii:

"Carlo, tabasamu la mbinguni kwa ajili ya nchi hii iliyojeruhiwa na isiyo na amani, tunamsifu Mungu kwa maisha yako rahisi, yenye furaha na matakatifu. Ulikaribisha kwa ujasiri kuvuliwa ujana wako ili kujiweka wakfu mbinguni, pamoja na Yesu na Maria, kwa utume wa upendo usio na mipaka. Kwa kupumzika mwili wako wa kufa mahali ambapo Francis wa Assisi alijivua kila mali ya kidunia, wewe unapiga kelele pamoja naye kwa ulimwengu kwamba Yesu ndiye furaha yetu sote. Kijana uliyejaa ndoto, ukivutiwa na maumbile, michezo, internet, lakini uliyevutiwa zaidi na muujiza wa Yesu aliyepo kweli katika Ostia Takatifu, utusaidie kuamini kwamba yuko hai na kweli, njia kuu ya fumbo iendayo mbinguni na kutufundisha kuitafakari pamoja na Maria, katika mafumbo ya Rozari Takatifu. Carlo Tufafanulie, kwamba, zaidi ya mitindo, ni Yesu pekee, kwa kutuunganisha na yeye mwenyewe, hutufanya kuwa 'asili na sio nakala' na huru kweli. Utusaidie kujua jinsi ya kukutana naye kwa  kila kiumbe, lakini zaidi kwa maskini, ili ubinadamu uwe wa haki zaidi na wa kidugu, wenye utajiri wa uzuri na matumaini, kwa utukufu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina".

Carlo Acutis
13 October 2024, 11:19