Tafuta

Misa ya Mazishi ya Padre Marcelo Perez  huko Mtakatifu Andres Larrainzar nchini Mexico aliuawa kwa sababu ya utetezi wa Watu wa Asili. Misa ya Mazishi ya Padre Marcelo Perez huko Mtakatifu Andres Larrainzar nchini Mexico aliuawa kwa sababu ya utetezi wa Watu wa Asili.  (ANSA)

Sinodi imeombea padre“shujaa wa amani”aliyeuawa huko Mexico

Wakati mkutano wa Sinodi ulifanya maombi ya kumuombea marehemu Padre Marcelo Perez,mtetezi wa haki za kijamii za kiasili huko Mexico,Sr.María de los Dolores Palencia Gómez alisema mauaji yake lazima yasikose kuadhibiwa.

Vatican News

Mnamo Dominika tarehe 20 Oktoba 2024 Padre Marcelo Pérez Pérez, Paroko wa parokia ya Cuxtitali huko Mtakatifu Cristóbal de Las Casas, nchini Mexico, aliuawa baada ya kuadhimisha Misa. Sista María de los Dolores Palencia Gómez, mtawa wa Mexico kutoka Shirika la Masista wa Mtakatifu Joseph na Mjumbe wa Rais wa Mkutano Mkuu wa 16 wa Sinodi, alizungumza na Renato Martinez wa Vatican News kuhusu mauaji hayo.

Kuhani kwa amani

Katika ufunguzi wa kusanyiko la sinodi mnamo Jumatatu Oktoba 21, sala ilitolewa kwa ajili ya roho ya marehemu kuhani huyo. Sr. María alisema wajumbe wa Sinodi walionesha mshikamano wao na Kanisa la Ulimwengu na watu wa Mexico. Alieleza Padre Marcelo kama shujaa wa amani ambaye alijaribu kuleta mazungumzo na haki kwa maskini zaidi. Akiwa mshiriki wa kabila la kiasili nchini Mexico, alikuwa ametetea haki za jamii ya Tzotzil na alizungumza dhidi ya ghasia nchini humo. Sr. María alifafanua mauaji ya padre  kuwa ishara kwamba kuna watu wanaojaribu kuleta migawanyiko katika jamii.

Mazishi ya Padre Marcelo huko Mexico
Mazishi ya Padre Marcelo huko Mexico

Chiapas: eneo lililo na alama za biashara na umaskini

Uhamaji wa kulazimishwa umesababisha kuongezeka kwa utamaduni wa vurugu nchini Mexico, hasa katika jimbo la Chiapas—ambapo Padre  Marcelo anatokea. Chiapas inapakana na Guatemala, ambako kuna mtiririko wa mara kwa mara wa wahamiaji kutoka Amerika ya Kusini, Asia, Afrika, na nchi za Ulaya.  Sr. María alisisitiza uhamiaji huu “si wa utalii, mahusiano, au masomo; ni uhamaji unaoendeshwa na ulazima,” na watu hufika wakiwa na mahitaji mengi. Chiapas ni mojawapo ya majimbo, Sr. María alieleza, ambayo yanakabiliwa na “jeuri kali kutokana na mapambano ya kimaeneo kati ya mashirika yanayosafirisha dawa za kulevya.” Kulingana na Insight Crime, shirika lisilo la kiserikali, linalihusiana na uchunguzi wa kihalifu, jimbo la Chiapas ni maarufu kwa usafirishaji wa dawa za kulevya, silaha na wahamiaji kuelekea Marekani. Sr. María alisema jeuri, mashindano, wizi, na utekaji nyara umesababisha uhamiaji wa ndani na, “katika visa fulani, migawanyiko kati ya jamii, mizozo, na kutoaminiana kati ya watu ndugu ambao wameishi pamoja kwa muda mrefu.”

Mazishi ya Padre Marcelo
Mazishi ya Padre Marcelo

Kukuza ufahamu

Sr. huyo  wa Mexico alisisitiza juu ya mauaji hayo ya  Padre Marcelo kuwa yasiende bure bila kuadhibiwa na kwamba haki itendeke na kuhakikisha kwamba kile kinachotokea katika maeneo haya hakisahauliki. Kifo chake cha hivi karibuni zaidi katika jimbo hilo mwaka huu kuanzia Januari hadi Agosti, kumekuwa na mauaji ya 500, kuongezeko kutoka idadi ya mwaka jana ya 309. “Tunahitaji kupiga kelele na kuufanya ulimwengu uelewe na usikie,” Sr. María alieleza, “kwamba kuna mfululizo wa hali zinazopinga ubinadamu na pia dhidi ya uumbaji.”

22 October 2024, 14:09