Watu wa Haiti wanajaribu kukimbia vurugu za magenge ya kihalifu katika mji wa  Port-au-Prince. Watu wa Haiti wanajaribu kukimbia vurugu za magenge ya kihalifu katika mji wa Port-au-Prince. 

Haiti,nyumba ya Wamisionari wa Upendo ilishambuliwa

Nyumba ya watawa na hospitali ya Masista wa Mama Teresa,katika mji mkuu wa Port-au-Price,viliharibiwa na kuchomwa moto na kundi lenye silaha.Watawa hawa walikuwa wakikaribisha na kutunza hadi watu elfu 30 kwa mwaka.

Na Marine Henriot na Angella Rwezaula– Vatican.

Hadi usiku wa Jumamosi tarehe 26 Oktoba 2024 kituo hiki kilikuwa ni moja ya sehemu za mwisho zinazoheshimika katika nchi ya Haiti iliyokumbwa na vurugu. Jioni hiyo,  genge la kihalifu lilipora nyumba ya watawa na hospitali ya Wamisionari wa Upendo,( Wajulikanao wa Mama Teresa wa Kalkuta)katika mji mkuu Port-au-Prince, kabla ya kuchoma kila kitu. Kwa bahati nzuri, hakuna mtawa yeyote aliyejeruhiwa. Mwishoni mwa Septemba polisi waliwataka watawa hao kuondoka eneo hilo na kufunga nyumba yao, kwani mapigano na magenge hayo yalizidi kuwa hatari kwa maisha yao. Mnamo tarehe 26 Oktoba 2024, waharibifu waliingia ndani ya nyumba hiyo, wakaharibu sehemu ya kuta na kumwaga chini kabisa nyumba ya watawa  hao na hospitali. Mabenchi, vitanda, vifaa vya matibabu, kila kitu kilichukuliwa na baadhi ya vitu tayari vimeuzwa kwenye soko kuu la jiji.

Kutokujali kwa magenge

Ni mara ya kwanza kwa Wamisionari wa Upendo kushambuliwa moja kwa moja nchini humo. Kufikia sasa, hata magenge hayo yalikuwa yakiheshimu misheni zao muhimu kwa idadi ya watu. Jimmy Chérizier, kiongozi asiye na shaka ya genge lililohusika na shambulio hilo, alisema  ni hatari sana: “Genge hilo la kihalifu limepoteza akili zote, heshima zote kwa watawa na watu, kwa sababu linajua vyema kwamba ni maskini zaidi wanaofaidika na huduma ya watawa na ambao wamefaidika nayo kwa miaka yote." Karibu watu elfu 30 walitibiwa kila mwaka katika nyumba ya watawa.” Katika majira ya kiangazi, usalama ulizidi kuwa mbaya katika kitongoji cha Bas Delmas huko Port-au-Prince, nyumba nyingi zilichomwa moto na raia wengi walilazimika kukimbia. Wamisionari kwa sasa wamekaribishwa katika jumuiya nyingine ambayo watawa wa Mama Teresa wanayo huko Haiti.

Nyumba iliyoanzishwa na Mama Teresa

Wamisionari hawakulazimika kuondoka kamwe katika nyumba yao, ambayo ilikuwa kitovu cha udugu. Ilikuwa imefunguliwa na Mama Teresa mwenyewe mnamo 1979, baada ya kuona wagonjwa wakiachwa kufa katika ua wa hospitali kuu huko Port-au-Prince. Tangu wakati huo, maelfu ya watu wa Haiti wamepitia mikono ya watawa hao wenye upendo, wakipokea msaada wa chakula, usaidizi, upasuaji au matibabu. Katika nchi iliyozama katika vurugu, shambulio hili la moja kwa moja kwa watawa linaweza kuhatarisha misheni yao yote nchini Haiti.

Papa kwa Wakatoliki wa Estonia:kuendekeza furaha ya kimisionari katika siku zijazo

Baba Mtakatifu alituma barua kwa Askofu Philippe Jourdan wa Tallinn,kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Usimamizi wa Kitume wa Estonia:“Adhimisho hili linaadhimisha tumaini lisilotikisika na imani kwa Mungu kwa miongo mingi ya mateso kazi,dhuluma.Vita ni chanzo cha uchungu na kukumbusha nyakati za giza za historia."

Uhalifu
04 November 2024, 16:12