Tafuta

Kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia unaohusiana na Migogoro uupitia Elimu:Mbinu yenye Msingi wa Imani ndiyo mada ya mkutano tarehe 6 Novemba mjini Vatican. Kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia unaohusiana na Migogoro uupitia Elimu:Mbinu yenye Msingi wa Imani ndiyo mada ya mkutano tarehe 6 Novemba mjini Vatican. 

Imani na Vitendo:Kongamano dhidi ya nyanyaso za kingono zinazohusiana na migogoro

Ubalozi wa Uingereza katika Vatican na Huduma ya Wakimbizi ya Kijesuit unajiandaa kongamano la kujadili mgogoro wa kimataifa wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro na jinsi ya kukabiliana nao kupitia elimu na utetezi unaoendeshwa na imani utakaofanyika tarehe 6 Novemba 2024.

Na  Francesca Merlo – Vatican.

Suala la unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na migogoro (CRSV)linaendelea kusumbua ulimwengu, na athari zake kwa watu na jamii ulimwenguni kote  ni mbaya. Ili kuakisi ukweli huu mbaya, Ubalozi wa Uingereza unaowakilisha nchi hiyo jijini Vatican, kwa ushirikiano na Shirika la Huduma ya Wakimbizi ya Kijesuit (JRS), wameandaa Kongamano Roma kushughulikia suala hilo. Limepewa mada “Kukabiliana na Ukatili wa Kijinsia Unaohusiana na Migogoro Kupitia Elimu: Mbinu yenye Msingi wa Imani,” tukio hili litafanyika  Jumatano, tarehe 6 Novemba 2024 ambalo litawaleta pamoja mashirika ya Kikatoliki na waokokaji, yote yakilenga kuangazia athari mbaya za CRSV kwa jamii ulimwenguni  kote na kuchunguza majibu yenye ufanisi ya msingi wa imani kupitia elimu na utetezi.

CRSV ulimwenguni kote

Katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari Ubalozi wa Uingereza na JRS waliandika kwamba mpango huo unaibuka huku unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro ukiendelea kuongezeka katika maeneo mengi, ukiwaathiri wanawake na wasichana. Kwa mujibu wa Ripoti ya hivi karibuni,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, 2023 ilishuhudia ongezeko la kutisha la 50% la kesi zilizothibitishwa duniani kote, huku wanawake na wasichana wakichangia 95% ya matukio yaliyoripotiwa. Idadi halisi inatarajiwa kuwa kubwa zaidi, kwani matukio mengi hayaripotiwi. Janga la CRSV ni kubwa zaidi katika nchi kama vile Sudan, Ukraine, Myanmar, Haiti, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambapo zaidi ya wanawake na wasichana milioni 612 wanaishi chini ya tishio la ukatili la mara kwa mara huku kukiwa na migogoro inayoendelea.

Wazungumzaji mashuhuri wakishiriki katika mkutano huo Victor Setibo, Mkurugenzi wa Nchi wa  Shirika la Kijesuit la Wakimbizi (JRS) nchini DRC, atahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba kuu katika kongamano hilo. Nchini DRC, Shirika la Kijesuit (JRS) limekuwa likiongoza programu za kibunifu ambazo huwapa waathirika elimu muhimu na mafunzo ya jamii, inayotoa njia ya maisha kwa wale wanaokabiliana na athari kubwa za CRSV. Watakaoshirikiana na Setibo watakuwa ni pamoja  Sr Elena Balatti, Sista Mmisionari wa Comboni anayeishi Sudan Kusini; Erica Hall, Mkuu wa Sera na Mahusiano ya Serikali katika Dira ya Dunia Uingereza; na Mónica Santamarina, Rais wa  Umoja wa Kimataifa wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki.

CRSV inasambaratisha maisha

Akizungumza kabla ya hafla hiyo, Balozi wa Uingereza anayewakilisha nchi yake mjini Vatican  Christopher Trott, aliakisi jukumu la kipekee na muhimu la mashirika ya kidini katika kushughulikia shida hii ya ulimwengu."Kiwango cha changamoto ambayo unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro unaleta duniani kote ni kubwa,” alisema Balozi Trott. “Inasambaratisha maisha na kuharibu jamii. Uingereza ni kiongozi wa muda mrefu duniani katika kukabiliana na unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro… Kanisa Katoliki na jumuiya za kidini ni washirika wakuu katika kazi hii muhimu.”

JRS kwenye mstari wa mbele

JRS, pamoja na mashirika mengine ya Kikatoliki, yamekuwa mstari wa mbele katika utetezi na usaidizi kwa waathirika, kuendeleza programu zinazolenga kuelimisha jamii na kusaidia uponyaji na upatanisho. Ndugu Michael Schöpf, Mkurugenzi wa Kimataifa wa JRS, alikazia uhitaji wa kuchukua hatua shirikishi, akisisitiza kwamba “mgogoro wa haki za kibinadamu unaoendelea wa unyanyasaji wa kingono unaofanywa katika hali za migogoro umeruhusu kuanzishwa kwa utamaduni wa kutoadhibiwa, kuwalinda wahalifu na kuzidisha mateso ya mamilioni ya watu ulimwenguni pote.” Matokeo muhimu ya kongamano hilo yanatarajiwa kuwa kutiwa saini kwa Tamko la Ubinadamu na Viongozi wa Imani na Viongozi wa Imani, taarifa ya pamoja inayothibitisha utu wa asili wa manusura na watoto waliozaliwa kutokana na ukatili huo, huku pia wakiazimia kuchukua hatua za kuzuia na kurejesha utu.

Mkutano kuhusu nyanyaso
05 November 2024, 15:47