2024.11.07 Kardinali Pierbattista Pizzaballa,Patriaki wa Yerusalemu. 2024.11.07 Kardinali Pierbattista Pizzaballa,Patriaki wa Yerusalemu.  (© LPJ)

Kardinali Pizzaballa:sala ya amani kwa Yerusalemu ni kilio cha amani kwa wote!

Ujumbe kwa washiriki wa Kongamano lililoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Yohane Paulo II cha Lublin nchini Poland kutoka kwa Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu kwamba:Mahusiano kati ya wakazi wa Nchi Takatifu yanapaswa kuwa sura ya uwepo wa Mungu na ukaribu naye.Kongamano hilo lilianza tarehe 5 na kuhitimisha tarehe 7 Novemba 2024.

Na Dorota Abdelmoula-Viet na Angella Rwezaula - Vatican.

Maombi ya amani kwa Yerusalemu kwa hakika ni kilio cha amani kwa ulimwengu mzima. Hivi ndivyo alisema Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Yerusalemu ya Walatini, katika ujumbe wake kwa washiriki wa mkutano wa kimataifa uliongozwa na mada: “Ombeni Amani kwa ajili ya Yerusalemu (Zaburi 122.6)”, ulioandaliwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Yohane  Paulo II cha Lublin (KUL) , nchini Poland, ambacho kiliona ushiriki wa wataalimungu  na wasomi wa Biblia kutoka duniani kote. Tukio hilo lilifanyika kuanzia tarehe 5 hadi 7 Novemba 2024  katika Chuo Kikuu kwa mpango wa Kituo cha Abraham J. Heschel cha Mahusiano ya Kikatoliki na Kiyahudi kwa ushirikiano na Taasisi ya Sayansi ya Biblia. Miongoni mwa wageni waalikwa, alikuwa ni Profesa Abraham Skórka, Mkuu wa Kiyahudi huko Argentina, na Kardinali Pirebattista Pizzaballa, aliyekuwa mgeni  heshima katika chuo kikuu hicho (KUL).

Mahusiano ya watu wa nchi Takatifu 

Katika ujumbe wake, uliosomwa kupitia kiungo kwa njia ya  video, Kardinali huyo alisema kwamba mahusiano kati ya wakazi wa Nchi Takatifu yanapaswa kuwa taswira ya uwepo wa Mungu na ukaribu naye. Alikumbuka kwamba kilio cha Kibiblia cha amani kwa Yerusalemu ni wito wa  wakati unaofaa katika muktadha wa hali ngumu na yenye shida katika Nchi Takatifu na kwa hivyo alisisitiza kwamba amani ni zaidi ya moja ya tunu zinazopendwa na waamini wa Kristo. "Kwetu sisi Wakristo, amani sio kipengele kimoja tu cha maisha ya Kanisa", lakini "ni sifa kuu za utambulisho na utume wa Kanisa," Kardinali huyo alisema. "Amani kwanza kabisa, kabla ya kuwa hatua ambayo Mungu anatualika kwayo, pia inatuambia kitu kuhusu utambulisho wa Mungu", aliongeza, akikumbuka vifungu vya Maandiko. "Utume wa Kanisa ni kumtangaza Mungu, na uso wa Mungu uko juu ya uso wote wa amani." Kisha akizungumza kuhusu utume wa Kanisa katika Nchi Takatifu, Kardinali Pizzaballa alirejea picha mbili za Mwisho wa Dunia ambazo zinahusu: hema na Bibi-arusi. "Ni aina ya utambulisho wa Yerusalemu," alisema.

Maandiko matakatifu:Yerusalemu ni mji ushukao kutoka Mbinguni

Yerusalemu ni mji "unaoshuka kutoka mbinguni", uwepo wa Mungu, unaofananishwa na hema, na urafiki wa karibu na Muumba, ambaye sura yake ni Bibi-arusi. “Hii inatuambia jambo fulani kuhusu maisha ya Yerusalemu yanapaswa kuwa. Jiji la Yerusalemu, Kanisa la Yerusalemu, linapaswa kuwa mahali ambapo uwepo wa Mungu unaonekana, wakati ukaribu na Mungu unapaswa kuonekana katika matendo yetu. Ombi la amani kwa ajili ya Yerusalemu pia ni sala ya amani kwa watu wote", Patriaki  alisisitiza, "kwa sababu mioyo ya watu wote huko Yerusalemu." Kardinali pia alikumbusha kwamba, wito wa wakazi wa Nchi Takatifu ni kushuhudia maisha na Mungu na uwezo wa kuleta maisha kwa wengine. "Hebu tuombe kwa hili na tujaribu kuwa mfano mdogo wa hilo. Najua jinsi tulivyo na mipaka, lakini hata hivyo, tunapaswa kukumbuka daima ushuhuda wetu ni nini kama wakazi wa Yerusalemu," alihitimisha.

08 November 2024, 16:56