Washington,Kard.D.Gregory:kama watu wa imani na nia njema,tumeitwa kutafuta ukweli
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Wilton Gregory, Askofu Mkuu wa Washington, alitoa taarifa ifuatayo tarehe 6 Novemba 2024 kufuatia uchaguzi mkuu wa 2024 uliofanyika kwamba “Leo, wakati taifa letu linapojiandaa kuchukua mwelekeo mpya katika utawala, ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu kukumbuka kwamba, kama watu wa imani na nia njema, tumeitwa kufanya kazi pamoja kutafuta ukweli, haki na amani katika nchi yetu, nyumbani, katika jamii zetu, na katika taifa letu.”
Mungu ibariki Nchi ya Marekani
Askofu Mkuu wa Jiji la Washingtoa aidha aliongeza: “Baadhi ya watu leo wanapumua kwa utulivu kutokana na matokeo ya uchaguzi wetu wa kitaifa, majimbo na mitaa, hata kama wengine wanakabiliwa na wasiwasi kuhusu maisha yetu ya baadaye. Njia yetu ya kusonga mbele iko katika heshima yetu kuheshimiana sisi kwa sisi na katika hadhi tuliyopewa na Mungu tunayoshiriki, ambayo inayotolewa bure kwa sala, subira, fadhili na tumaini.” Kwa kuhitimisha Kardinali Gregory alisema: “Mungu ibariki Nchi ya Marekani.”
Maneno ya kwanza ya Trump
Rais wa zamani Donald Trump alichaguliwa kwa muhula wa pili katika Ofisi ya Oval miaka minne baada ya kupoteza muhula wake wa pili mfululizo, kulingana na makadirio mengi. Uchaguzi wa Trump uliofanyika Novemba 5 unaashiria hitimisho la msimu wa kampeni wenye misukosuko uliojumuisha hata majaribio mawili ya kumuua. “Nataka kuwashukuru watu wa Marekani kwa heshima kubwa ya kuchaguliwa kuwa rais wenu wa 47 na rais wenu wa 45,” Trump aliwaambia wafuasi wake huko West Palm Beach, Florida, mwendo wa saa 8:30 asubuhi ya Novemba 6, na kuongeza, “Hii itakuwa kweli enzi ya dhahabu ya Amerika.”