Padre  Giovanni Merlini wa Shirika la Damu Azizi ya Yestu atatangazwa kuwa Mwenyeheri tarehe 12 Januari 2025. Padre Giovanni Merlini wa Shirika la Damu Azizi ya Yestu atatangazwa kuwa Mwenyeheri tarehe 12 Januari 2025. 

Padre Yohane Merlin:Mkutano wa kitaalimungu kuhusu Mwenyeheri wa kwanza katika Jubilei 2025

Jumatatu alasiri tarehe 11 Novemba 2024 katika Chuo cha Kipapa cha Laterano,utafanyika mkutano wa mafunzo utakaojikita na sura ya aliyekuwa Mkuu wa III wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu aliyeishi katika karne ya 19.Ni katika fursa ya maandalizi ya kutangazwa kuwa Mwenyeheri,tarehe 12 Januari 2025 akiwa mwenyeheri wa kwanza wa mwaka Mtakatifu wa 2025.

Vatican News

“Mwenyeheri Padre Yohane Merlin: tasaufi ya mang’amuzi ya kiroho na mwongozo,” ndiyo itakuwa mada ya mkutano utakaofanyika tarehe 11 Novemba 2024, kuanzia saa 9.00, alasiri katika chumba cha 200 cha Laterano, jijini Roma. Tukio hilo lilihamasishwa na Kituo cha Utafiti cha Umoja  cha Damu Ya Yesu (Sanguis Christi Union), katika fursa ya kuelekea  kutangazwa mwenyeheri huyo Padre Yohane Merlini, ambaye ni  mmisionari wa Damu Azizi ya Yesu na aliyekuwa Mkuu wa Tatu wa Shirika hilo. Maadhimisho ya kutangazwa kwake yatafanyika tarehe 12 Januari 2025 saa 5:00 kamili  asubuhi saa za Roma katika  Basilika ya Mtakatifu Yohane wa Laterano, Jijini Roma.

Mwanzilishi wa shirika Mtakatifu Gaspare del Bufalo
Mwanzilishi wa shirika Mtakatifu Gaspare del Bufalo

Utafiti wa kisayansi wa kiroho

Yohane Merlini alizaliwa mwishoni mwa karne ya kumi na nane na kujiunga na Wamisionari wa Damu Azizi katika miaka ya mapema ya 1820, pamoja na mwanzilishi wa Shirika hilo na Mtakatifu wa baadaye Gaspare Del Bufalo. Mkutano uliopangwa kufanyika Jumatatu tarehe 11 Novemba 2024, kwa mujibu wa Padre Benedetto Labate, Mkuu wa Provinsi ya Italia ya Wamisionari wa Damu Azizi, katika barua yake anabainisha kuwa:  “Unawakilisha mapokeo yaliyounganishwa kwa ajili yetu sisi Wamisionari wa Damu Azizi, kwa ajili ya Waabuduo Damu ya Kristo na pia kwa familia zingine za  hali ya kiroho zinayohusishwa na kujitolea kwa Damu ya Kristo, tangu  miaka ya 1960, wamisionari wetu wamejishughulisha na utafiti wa kisayansi na uchunguzi wa kina wa hali hii ya kiroho.”

Shirika la damu Azizi
Shirika la damu Azizi

Padre Merlini, “Mtakatifu wa mang’amuzi”

Naye Padre  Giacomo Manzo, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti cha “Unione Sanguis Christi,” alieleza kwamba mkutano huo utakazia “kuhusu hali ya kiroho ya kufanya mang’amuzi na mwongozo” unaoshuhudiwa na Padre  Yohane Merlini, ambaye “anaweza kuonwa anafaa kuwa ‘Mtakatifu wa mang’amuzi, mtu ambaye, kwa shukrani ya utendaji wa Roho Mtakatifu, alijua jinsi ya kuishi na kufundisha jinsi ya kukabiliana na uchaguzi wa maisha ya mtu, na  jinsi ya kujitawala katika nuru ya  Neno la Mungu na mapenzi yake ya kimungu.”

Watakazungumza

Miongoni mwa wasemaji ambao watachukua fursa za kushika maikrofoni ni Padre Luigi Maria Epicoco, Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha  Laterano, Monsinyo Riccardo Ferri, Msimamizi Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Rosalba Manes, Profesa wa kawaida  wa Taalimungu ya Biblia katika Chuo Kikuu cha Gregoriana,  na mkuu wa Kitivo cha Falsafa cha Gregoriana Padre Gaetano Piccolo(SJ). Mbali na salamu kutoka kwa mkuu wa Chuo hicho cha kipapa Laterano, pia salamu zitatoka kwa Askofu Mkuu Alfonso Amarante na atakayetoa  utangulizi wa shughuli hizo zimekabidhiwa kwa Mwariri wetu  mkuu wa uhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Dk. Andrea Tornielli.

09 November 2024, 17:11