Tafakari Liturujia ya Neno la Mungu: Upendo kwa Mungu na jirani ni muhtasari wa Amri kumi za Mungu. Tafakari Liturujia ya Neno la Mungu: Upendo kwa Mungu na jirani ni muhtasari wa Amri kumi za Mungu.  (Vatican Media)

Tafakari Neno la Mungu Dominika 31 ya Mwaka B: Upendo Kwa Mungu Na Jirani

Upendo kwa Mungu na jirani kimsingi ni muhtasari wa Amri kuu ya upendo ambayo Kristo Yesu amewaachia wafuasi wake, yaani kumpenda Mungu na jirani na kwamba, huu ni wito wa hali ya juu kabisa kwa Wakristo na ni chimbuko la furaha ya matumaini ya Kikristo! Changamoto kwa waamini ni kuondokana na chachu ya unafiki katika upendo kwa kuhakikisha kwamba, upendo wao unakuwa ni safi pasi na mawaa mbele ya Mwenyezi Munguu na mbele ya jirani zao!

Na Padre Joseph Herman Luwela, - Vatican.

UTANGULIZI: Karibu sana mpendwa msikilizaji na msomaji wetu katika Kipindi cha Liturujia ya Neno la Mungu, Dominika ya thelathini na moja ya Mwaka B wa Kanisa. Tazama ni pendo la namna gani kuitwa wana wa Mungu na kweli ndivyo tulivyo leo karibu katika tafakari yetu, leo mama kanisa mtakatifu anatunafundisha amri ya kwanza na kuu zaidi ya amri zote ni upendo kwa Mungu na jirani. Maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu katika hatua mbalimbali za maisha na utume wa Kanisa ilinogeshwa na kauli mbiu “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume.” Watu wa Mungu wakajitambua kuwa wao ni sehemu ya Kanisa la Kisinodi na Kimisionari tayari kutangaza na kushuhudia Ufalme wa Mungu, kwa kushirikiana na binadamu wote, kwa kujenga utamaduni wa kusikiliza kwa makini kile ambacho Roho Mtakatifu anataka kuyaambia Makanisa.   Dominika ya 31 ya mwaka B, tunaendela kujengwa na kuimarishwa katika mpango wa Mungu wa Kupendana. Tutasikia  mazungumzo kati ya Yesu na mwandishi huyu yanavyofanyika. Lakini moja ya waandishi, anamwendea na kumuuliza, ni ipi  amri kuu kuliko zote, lilikuwa swali gumu, na mtego kwa Yesu Kwani kwa Wayahudi rabbi au mwalimu aliulizwa maswali ya mtego hadharani ili ajibu maswali mengine, alijaribiwa ili kuweza kusema maandiko yote, akiwa amesimama kwa mguu mmoja, aliinua mguu mmoja kutoka ardhini na kusema, sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu. Bwana ni mmoja, umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, akili na nguvu zako zote. Kisha akaweka mguu wake chini, na hiyo ndiyo amri. Matumaini ya Kikristo yanafumbatwa katika furaha ya Injili, dhiki na subira; kwa kudumu katika sala; kuwa kujisadaka kwa ajili ya mahitaji ya watakatifu wa Mungu; kwa kujikita katika ukarimu kwa wageni pamoja na kujibu kilio cha wahitaji. Kimsingi huu ni muhtasari wa Amri kuu ya upendo ambayo Kristo Yesu amewaachia wafuasi wake, yaani kumpenda Mungu na jirani na kwamba, huu ni wito wa hali ya juu kabisa kwa Wakristo na ni chimbuko la furaha ya matumaini ya Kikristo! Changamoto kwa waamini ni kuondokana na chachu ya unafiki katika upendo kwa kuhakikisha kwamba, upendo wao ni safi pasi na mawaa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Upendo kwa Mungu na jirani ni muhtasari wa Amri kuu za Mungu
Upendo kwa Mungu na jirani ni muhtasari wa Amri kuu za Mungu

UFAFANUZI: Hapa tunaona msisitizo wa Neno la Mungu ni juu ya  kusikiliza, yaani, uhusiano halisi na Mungu, ambao hupita katika masikio zaidi hasa masikio ya mioyo yetu kuliko kupitia masikio ya kawaida, na huzungumza juu ya upendo kwa Mungu na jirani haswa kwa kiumbe wake huyu wa pekee yaani  mwanadamu ambaye ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na akajaliwa akili, utashi dhamiri na mwili, kuna mambo mawili kati ya nafsi na akili katika inijili ya Marko. Hapana, roho ndio itiayo uzima mwili haufaikitu , akili humsaidia binadamu kutafuta ukweli na mantiki kisha kuuachia utashi kufanya maamuzi yakinifu n mwili ndio hekalu la Roho Mtakatifu ambapo ndipo humuwezesha mwanadamu kutenda baada ya kusikia kwa sauti au kupitia milango ya fahamu kupambanua na kisha kutenda nguvu zote, Yesu alipoona jinsi yule mwandishi amejibu kwa ufasaha na busara baada ya kumsikiliza alipotoa fundisho juu ya amri kuu ya upendo anahitimisha kwa kusema: “Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu.” Hivyo kumpenda Mungu kwa moyo na akili zote pia na uhusiano wetu na Mungu, huanza kutokana kusikiliza, Neno lake. Na kwa hivyo inamaanisha uhusiano ambao unagusa kila kitu.

Upendo wa dhati unasimikwa katika unyenyekevu
Upendo wa dhati unasimikwa katika unyenyekevu

Sio kwamba mtu anamsikiliza Mungu na kuuelewa ujumbe husika, hii  haitoshi kama hatutakwenda kutenda vema kwa kutumia akili na utashi sahihi.  Ikiwa haya yote hayatafsiriwi katika matendo, kwa nguvu, katika mazoezi ya vitendo, yote haya ni matunda ya upendo wa kimungu. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, roho yako yote, akili yako yote, nguvu zako zote. Lakini Yesu anaongeza kitu ambacho hakuulizwa juu yake. Alikuwa ameulizwa kuzungumzia kwanza na anaongeza, ya pili ni, lakini atasema kuwa ni sawa na ya pili ni hii, umpende jirani yako kama wewe mwenyewe. Jambo linahusu uhusiano na wengine, halipaswi kupuuzwa.. Inatokea mara nyingi sana, tunaweza pia kufikiria kinyume, kama tulivyokuwa tayari kuhusiana na uadilifu wa mtu wa wengine bila kuangalia  uadilifu wao. Uhusiano na Mungu, ambapo imani ya usawa tu inafanywa, ambapo bila matendo hakuna uhusiano na Mungu, kweli, ili kumpenda Mungu lazima tumpende jirani yetu. Mtu hawezi kamwe kumpenda Mungu bila kumpenda jirani yake. Ikiwa unampenda Mungu na humpendi jirani yako, humpendi Mungu kwani jirani ni kielelezo halisi cha Mungu asiyeonekana kwa macho.

Waamini wanaalikwa kuwa ni vyombo vya huruma na upendo kwa Mungu na jirani
Waamini wanaalikwa kuwa ni vyombo vya huruma na upendo kwa Mungu na jirani

Leo hii tunashuhudia chuki na uhasama kati binadamu tunavyoshambuliana katika nafasi mbali mbali, na kupafanya duniani hapa kuwa sehemu isiyo salama kwa binadamu kuishi kwa sababau tumekosa upendo thabiti na kutokusikiliza sauti ya Yesu ya kumpenda Mungu na jirani kwa moyo wote , tunashuhudia leo uhai unashambuliwa kila kona kwanjia mbali mbali ndoa na familia hakuna upendo mashambulizi ni makubwa jamii inapokea matunda hatarishi kutoka katika familia zilizopoteza upendo, zimejengwa katika dhana ya ubinafsi, chuki, mapigano kujilimbikizia mali na madaraka yote haya ni mazao ya kukosa na kujifunza tabia ya upendo kwa Mungu na kwa jirani, kanuni na taratibu ndio huongoza na kuratibisha mtindo wa maisha ya jamii yoyote na mmoja  au kundi linapokiuka na kuvunja kanuni na taratibu huleta fujo na kutoeleweka, katika jamii ya watu wa Israeli walioamini katika Mungu mmoja katika somo la kwanza Kumb, 6,2-6 Torati ya Musa inawakumbusha watu kuzingatia maagizo ya Mungu wao ìli waweze kuishi katika Nchi ya waliyopewa na Mungu  na kwa kuzishika amri na kumpenda Mungu watapata mafanikio mengi zaidi hasa kuishi katika nchi ijaayo maziwa na asali. Hata wewe ndugu yangu unaye nisikia Je, mimi na wewe tunampenda nani na tunasikiliza ya nani na kutenda ambayo ndio uzima na usalama wetu.

Upendo kwa Mungu, Jirani na Kazi ya Uumbaji
Upendo kwa Mungu, Jirani na Kazi ya Uumbaji

Tunapaswa kumsikiliza Mungu na kutenda yale Mungu anayotuamuru. Ni wazi lazima kusikilizana sisi binadamu, watoto lazima wawasikilieze wazazi wa na walezi wao kwa yale mahusia na mfundisho mema katika malezi na makuzi yao kwani sio wazazi wote huweza kuwafundisha watoto kweli na tunu za makuzi hasa kumjua Mungu, tabia njema na utu wema kwani wapo baadhi ya wazazi na walezu wachache huwafundisha upotovu au hata kuwatelekeza katika kuwasaidia watoto na vijina katika makuzi na kuwaeleza njia sahihi za maisha bora. Viongozi wa dini watimize wajibu wao wa kuwapenda waamini wa ona watu wote wakifundisha kwa mfano wa maisha yao juu ya kumpenda na kumjua Mungu na namna ya kuishi maisha ya kimaadili, na kuwafanya binadamu wote wawe mabalozi wa haki na mani. Nao viongozi wa serkali lazima watumie nguvu na mamlaka yao kuwapenda rai wao na kuwahudumia kwa haki na usawa bila upendeleo wakipinga kila aina ya ubadhirifu na chuki na migawanyiko, wao wenyewe wakiwa mstali wa mbele katika kuishi ukweli wakizinatia na kutii sheria za nchi zao. Hata wewe msikilizajia na msomaji huajaachwa nyuma zingatia kuwa Bwana Mungu ni mmoja unapaswa kumpenda kwa nguvu zote, akili zote na utashi zote, kama mzaburu katika wimbo wa katikati anavyosema “wewe Bwana nguvu zangu nakupenda sana Ngao yang una pembe ya wokovu wangu, Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa na Hivyo nitaokoka na adui zangu (Zab 18,2).

LITURUJIA D 31
02 November 2024, 10:03