Tafuta

Sherehe rasmi inaashiria kufunguliwa tena kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame Sherehe rasmi inaashiria kufunguliwa tena kwa Kanisa Kuu la Notre-Dame  (ANSA)

Kanisa Kuu la Notre Dama:linafunguliwa kwa upya baada ya kuunguzwa moto!

Kanisa kuu Bikira Maria Mama Yetu(Notre Dama)lenye zaidi ya miaka 860 linafunguliwa tena kwa ibada takatifu tarehe 7 Desemba,miaka mitano baada ya kufungwa kutokana na moto ulioliteketeza kwa kiasi kikubwa.Ni sherehe zilizojaa furaha,neema na matumaini kwa Jimbo Kuu la Paris,Ufaransa na wapendwa wote wa Notre-Dame.Mwakilishi wetu anafafanua kile kinachotazamiwa kwa dakika hizi na kuendelea.

Na Delphine Allaire - Mwakilishi Maalum huko Paris

Baada ya hofu ya moto, ni matumaini ya kuzaliwa upya. Katika mkesha wa Mwaka Mtakatifu wa 2025 uliowekwa wakfu kwa ajili ya matumaini, wakati waamini kutoka sehemu mbalimbali za dunia watakusanyika mjini Roma, Kanisa Kuu la Maria la Paris pia litaakisi wema huu muhimu kwa maisha ya Kikristo, likiwakaribisha mahujaji na wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia, karibu milioni 15, tayari nusu ya idadi inayotarajiwa jijini Roma. Kabla ya hapo, ushirika wa kiroho wa kitaifa na wa ulimwengu wote umekamilika katika siku hizi tatu za kufungua tena, ikifuatiwa na oktava maalum.

Uzuri wa kanisa Kuu la Paris kufunguliwa tena desemba 7
Uzuri wa kanisa Kuu la Paris kufunguliwa tena desemba 7

Kugoga kengele kama ishara ya umoja

Jimbo kuu la mji mkuu inatumaini kuwa siku hizi za tarehe 7 na 8 Desemba kuonesha umoja na furaha ya kusikika Notre-Dame. Kama ishara ya ushirika, kengele zote nchini Ufaransa liombwa kulia kwa pamoja  Jumamosi saa 12:30 jioni. Itakuwa vivyo hivyo ng'ambo ya Atlantiki nchini Marekani, ambapo uaskofu wa Kikatoliki umeamua kufanya hivyo juu ya ishara hii ya furaha ya pamoja. "Baada ya miaka mitano ya ujenzi, tunataka kuuambia ulimwengu wote nini maana ya jengo hili, zaidi ya ushawishi wake katika sanaa, uchoraji na fasihi," alisema Askofu Mkuu  Olivier Ribadeau-Dumas, akisisitiza unyenyekevu na ukaribisho usio na masharti kwamba: "Kutoka kwa wakuu wa nchi, kwa maskini, kuanzia wenye afya hadi wagonjwa, kila mtu ana nafasi yake katika Kanisa kuu.” Kulingana na mkuu wa Kanisa kubwa zaidi jijini Paris, inahusu kuruhusu kila mtu "kukutana na uzuri unaozungumza juu ya Mungu."

Wageni wa kisiasa, kidiplomasia na kidini

Hadhira ya kuvutia ya wageni wa serikali, wa kifalme na wa kidini wataweza kusali na kuvutiwa na jiwe la blondie, nuru uiliyogunduliwa upya na muundo wa mistari mipya ya usanifu ndani ya uzio wa jengo la enzi za kati. Balozi wa Vatican  nchini Ufaransa, Askofu Mkuu Celestino Migliore, atamwakilisha Papa na kusoma ujumbe wake. Mtu mwingine wa Vatican, aliye karibu sana na Papa  Fransisko, atakuwepo katika nafsi ya katibu wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini Bi Emilce Cuda, mtaalimungu wa Argentina na Metropolitan wa Kiorthodoksi ya Ugiriki Emmanuel na Patriaki wa  Mashariki wa Maronite Bechara Rai na Patirkia  Mar Awa III, Kardinali Timothy Dolan, Askofu Mkuu wa New York, Marekani na pia mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Andrea Riccardi, atakuwa miongoni mwa wageni Jimbo hilo , pamoja na marais wa Ukraine, Italia, Ujerumani, Poland, Congo, Georgia  Meloni Waziri Mkuu na Waziri Mkuu wa Armenia, miongoni mwa wengine, pamoja na rais mteule wa Marekani, Bwana Donald Trump.

Kufungua tena kwa masifu ya jioni

Kila mtu atahudhuria ibada ya kufungua tena Jumamosi tarehe 7 Desemba 2024 ambapo itaanzia  katika Uwanja kabla ya Askofu mkuu kutekeleza ibada "rahisi na ya kiasi" ya kufungua milango saa 1:00, jioni masaa ya Ulaya. Askofu Mkuu  Laurent Ulrich, atagonga  mlango uliofungwa wa Notre-Dame huko Paris. Kisha atamkaribisha rais, akisindikizwa na mkuu wa idara. "Kipindi cha kwanza kitaanza, Jimbo kuu la Ufaransa likiwa mmiliki wa majengo kulingana na sheria ya 1905 na Jimbo lililopewa. Emmanuel Macron atazungumza kwa ufupi ndani ya Kanisa kuu saa 1.30 jioni. Kanisa kuu litapata Askofu wake mkuu, aliyeteuliwa mnamo tarehe 26 Aprili 2022, miaka mitatu baada ya moto huo kuunguza Kanisa Kuu,  Askofu Mkuu Laurent Ulrich atazungumza katika  hotuba, kisha ujumbe wa Papa utasomwa na mjumbe wake, Balozi wa Vatican na ibada itaanza. Inaundwa na sehemu tatu. Ni Kanisani kubwa nchini Ufaransa ambapo litakuwa na chombo kikubwa cha kuzungumzia na mara nane, askofu mkuu atahutubia na kufuata  Wimbo wa masifu  unaojumuisha wimbo, zaburi, wimbo wa Magnificat, nia ya maombi kwa ulimwengu wote, sala ya Baba Yetu. Baraka ya mwisho ya askofu mkuu na uimbaji wa Te Deum itahitimisha liturujia hiyo.

Misa ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu mpya na masalia ya watakatifu 5

Dominika tarehe 8 Desemba 2024 ikiwa ni Dominika ya II ya  Majilio, itafanyika misa ya uzinduzi na kuwekwa wakfu kwa madhabahu kuu saa 4:30 asubuhi. Takriban Maaskofu 170 kutoka Ufaransa na duniani kote watashiriki katika maadhimisho haya, pamoja na Mapadre kutoka kila parokia 106 za Jimbo kuu la Paris, na maadre kutoka katika kila moja ya makanisa saba ya Mashariki ya Kikatoliki, wakisindikizwa na waamini kutoka kila moja wa jumuiya hizo. Wakristo wa Mashariki pia watakuwa na Kanisa lililowekwa wakfu katika kanisa kuu hilo, lililopambwa kwa picha maalum, lililozinduliwa Siku ya Kimataifa ya Wakristo wa Mashariki, mnamo Mei 25.

Kutazama kwa mbali Kanisa Kuu la Paris
Kutazama kwa mbali Kanisa Kuu la Paris

Ibada za kuweka wakfu madhabahuni zitafanyika katika hatua tano. Masalia ya watakatifu watano yanawekwa na kutiwa muhuri madhabahuni. Masalia haya, ya wanawake watatu na wanaume wawili ambao wameweka alama ya historia ya Kanisa la Paris, ni yale ya Mtakatifu Marie Eugénie Milleret, Mtakatifu  Madeleine Sophie Barat, Mtakatifu  Catherine Labouré, Mtakatifu  Charles de Foucauld, na Mwenyeheri Vladimir Ghika. Kisha sala ya wakfu inasomwa, ikifuatiwa na upako wa mafuta, wakati wa kati wa kuwekwa wakfu. Sadaka ya uvumba itafuata, kabla ya madhabahu kupambwa na kuashwa mishumaa. Misa hii itafuatiwa na ushiriki wa chakula cha kidugu ya kuwakaribisha walionyimwa zaidi na wale wanaowasindikiza nao kila siku ndani ya mashirika ya Upando jijini  Paris. Dominika jioni, saa 12:30, misa ya pili itafanyika, iliyofunguliwa kwa waamini baada ya kujiandikisha.

Miezi sita ya sherehe hadi siku kuu ya Pentekoste

Misa ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu inaashiria mwanzo wa oktava, ambayo itawaleta pamoja waamini wa Paris katika utofauti wao mkubwa, pamoja na idadi nzuri ya watu ambao wameruhusu Notre-Dame kuweza kuwakaribisha tena, wakati wa misa inayoongozwa na askofu mkuu. Mpango huo mkubwa wa ujenzi na ukarabati utakuwa umekusanya kampuni 250 pamoja na mafundi 2,000. Walinzi na wafadhili watakuwa na misa maalum mnamo Desemba 11, kikundi chaa wazima moto siku ya Dominika  tarehe 15. Kanisa kuu  haliwezi kuchukua zaidi ya watu 40,000 kwa siku na kwa kuzingatia shauku ya ulimwengu wote, sherehe za kufungua tena zitapanuliwa hadi siku kuu ya Pentekoste, itakayofanyika tarehe 8 Juni 2025.

07 December 2024, 14:56