Muujiza wa 71 huko Lourdes watambuliwa:ni matumaini wa mkesha wa 2025
Vatican News
Mnamo mwaka 1923, John Traynor, mwenye umri wa miaka arobaini kutoka wilaya ya Liverpool nchini Uingereza ambaye alipigana Vita vya Kwanza vya Dunia katika safu ya askari wa akiba ya Jeshi la Wanamaji la Kifalme, ambapo katika vita vikali na vya umwagaji damu alijeruhiwa vibaya sana na miaka michache baadaye alifanyiwa upasuaji ambao katika sehemu zake zake za miguu yake iliyokuwa imepooza huku mashambulizi ya kifafa yakiwa yanamsumbua na kuendelea kumtesa. Majeraha yalikuwa kama bado yamefunguliwa baada ya mapigano ya moto na adui na ukosefu wa hisia katika mkono wake wa kulia. Katika mwaka huo hasa aliamua kushiriki katika hija ya Madhabahu Lourdes iliyoandaliwa na Jimbo lake la Liverpool, licha ya marafiki zake wengi, akiwemo Padre aliyejua udhaifu wake vizuri, walijaribu kumkatisha tamaa.
Imani bila mipaka
Safari ya kuthubutu kwa treni na meli kutoka Uingereza hadi Ufaransa, kwa ajili yake ambaye hakuweza hata kutembea, inawakilisha upendo ule kwa Mama ambao mama yake, Mkatoliki wa Ireland aliyekufa mapema wakati alipokuwa mtoto alikuwa ameridhisha imani. Kuogelea katika mabwawa ya madhabahu yalifanyika mchana wa Julai 25. Lakini ni baada ya maandamano ya Ekaristi ambapo jambo la ajabu lilitokea: wakati wa baraka na Sakramenti Takatifu, nguvu ilimvamia mwili wake. Miguu yake, ghafla, ilianza kuwa na nguvu, na mkono wake ukainuka hadi kufanya ishara ya msalaba.
Muujiza huja kweli
Siku iliyofuata, akiwa peke yake, alikwenda kwa miguu kwa Mama, kwenye pango. Hata majeraha ya kutokwa na damu yalikuwa yametoweka, pamoja na mshtuko wa kifafa ambao ulikuwa haumwachii. Madaktari watatu kutoka kwa raia wenzake ambao walikuwa pamoja naye wakati huo pia walithibitisha hili. Nao walishangaa.
Habari zaenea
Habari za uponyaji wa kimuujiza, ambao ulivuka mipaka na kufika Uingereza, ulivutia mara moja ofisi ya uchunguzi wa matibabu ya patakatifu hivi kwamba mnamo 1926, baada ya miaka mitatu ya uchunguzi, ilitoa tamko la pamoja la muda mrefu lililotiwa saini na wale madaktari watatu ambao walikuwa kwenye Hija na Traynor. Tamko ambalo litachapishwa katika Jarida de la Grotte, chombo rasmi cha waandishi wa habari cha Madhabahu, lakini ambalo halikutumwa katika Jimbo la Liverpool. Kisha giza, kwa karne moja.
Ugunduzi huo
"Ni mwaka 2023, katika hafla ya kuadhimisha miaka mia moja ya hija ya Liverpool, ambapo mwenzangu Kieran Moriarty, mjumbe wa Kiingereza wa Kamati ya Kimataifa ya Matibabu ya Lourdes, alinihimiza kuchimbua historia hii ambayo tulikuwa na ujuzi wa mdomo tu. Na cha kushangaza tuligundua ripoti ya kliniki kutoka 1926. Ndivyo alisema, mkuu wa sasa wa Ofisi ya Matokeo ya Matibabu, Daktari Alessandro de Franciscis, katika mahojiano yaliyotolewa kwa timu ya wahariri ya Kifaransa wa vyombo vya habari vya Vatican. Ambaye, baada ya kuunda upya historia nzima kwa undani, alituma hati hizo kwa Askofu Jean-Marc Misac, wa Jimbo la Tarbes na Lourdes ambaye, naye, alizipeleka kwa askofu mkuu wa Liverpool. Na alikuwa Askofu Patrick McMahon, ambaye tarehe 8 Desemba 2024 katika siku kuu ya Maadhimisho Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, alitambua rasmi uponyaji huu wa zamani." Kwa kutambuliwa huko, kunafikisha hadi sasa jumla ya miujiza ya Lourdes 71.
Upendo wa Mungu
Katika mahojiano hayo De Franciscis alihitimisha kwa usadikisho kwamba: “Yote haya yanawakilisha ishara ya wema wa Mungu na wa Mama Mkingiwa dhambi ya Asili na Mkamilifu. Na ni muhimu pia kwamba tangazo rasmi lilitolewa katika mkesha wa Jubilei ya 2025, iliyowekwa wakfu na Papa Francisko kwa matumaini ambayo mamilioni ya mahujaji wanaokwenda kwenye madhabahu hubeba mioyoni mwao."