Uthibitisho wa Padre Patton kuhusu bomu lililoshambulia mji wa Aleppo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Padre Francesco Patton, Msimamizi wa Nchi Takatifu, baada ya shambulio la bomu lililotokea huko katika jiji la Aleppo, alisema kuwa “Leo mchana, Dominika tarehe 1 Desemba, wakati wa shambulio la bomu katika jiji la Aleppo, bomu lilianguka kwenye jumba la Wafransiscan la Chuo cha Nchi Takatifu. Tunamshukuru Mungu, hakukuwa na waathiriwa au majeruhi, ni jengo pekee lililoharibiwa. Ndugu zetu na waamini wa parokia wote ni wazima. Kutoka kwa katika makao makuu yetu tunawasiliana nao mara kwa mara. Kwa sasa wanatuambia juu ya kuongezeka kwa mvutano na hofu miongoni mwa raia wa Aleppo kutokana na maendeleo yasiyotabirika ya makabiliano yanayoendelea. Tunawaalika mapadre wetu, Wakristo wa Nchi Takatifu, na makanisa yote kuungana nasi katika maombi ya amani katika Siria inayoteswa na miaka mingi ya vita na vurugu. Neno la Mungu katika Dominika hii ya kwanza ya Majilio linatualika kuweka tumaini hai kwa matarajio ya amani. Tunakaribisha mawaidha haya, na tunaomba yatimie kwa ndugu zetu wa Siria."
Ujumbe kutoka kwa Padre Massimo Fusarelli (OFM) kwa Ndugu wa Siria na Libanon
Na katika Ujumbe kutoka kwa Padre Massimo Fusarelli,(OFM) Mkuu wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafranciskani akiwa huko Msalaba Mtakatifu wa Sierra nchini Bolivia, baada ya kupata tarifa mbaya za huzuni kutokea Aleppo nchini Siria, aliwaandikia tarehe 28 Novemba 2024, Ndugu Wadogo walioko Siria na Lebanon katika barua kupitia kwa Misimamizi wa Nchi Takatifu. Barua yake inaanza salamu za amani ya Bwana, kwamba akiwa katika ziara ya kutenmbelea Ndugu Wadogo hivi karibuni alisoma habari za kusikitisha zinazofika kutoka nchi zao zinazo teseka sana, leo hasa kutoka Aleppo. Kwa hiyo njia hyo anabainisha kwamba anatoa “neno la amani la Mtakatifu Francis, hata katika wakati ambao si rahisi kutumia neno hilo. Zaidi ya hayo, tunajua kwamba katika Maandiko Matakatifu amani ni zawadi kutoka kwa Mungu na sikuzote hubaki kuwa kitu chenye thamani na wakati huohuo ni kitu chenye kudhoofika sana. Hatimaye inabaki kuwa zawadi ya eskatolojia, leo hii tunaweza kujua hakikisho lake, pamoja na kilio na matumaini.”
Padre Fusarelli aidha anaandika kuwa “Baada ya kutembelea nchi zao mwaka 2023, alihisi kwa nguvu zaidi jeraha ambalo vita hufungua tena.” Anawafikiria kwanza hao ndugu wapendwa, na anawaomba “wajitunze kadri mwezavyo, kwa sababu mafadhaiko na kiwewe cha nyakati hizi hazipaswi kupuuzwa kamwe. Ninawafikiria watu wenu na waamini, kuanzia watu wazima hadi vijana hadi watoto. Nawakumbuka uchangamfu na tumaini, pamoja na ugumu wanaokabiliwa na wakati ujao ambao unaonekana kutokuwa na uhakika sana.” Vile vila Padre Fusarelli anabainisha kuwa “ Niko karibu nanyi kwa maombi na mapendo, ninawaomba mnifahamishe. Tuendelee kuombea amani kwa kutegemea maombezi ya Bikira Safi na Mashahidi Watakatifu wa Damasco ili matumaini na ujasiri wa kuvuka usiku huu wa giza zisizimwe.” Padre Fusarelli anahitimishwa kwa Baraka ya Mtakatifu Francis na kuwasalimia kwa mkumbatio wa kidugu ulio hai.