Tafuta

Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa:Kama wakristo nenda kinyume na dhana ya dunia hii!

Katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 13 Septemba wakati wa mahubiri ya Papa, amekumbusha kuwa wakristo hawafuati roho ya dunia, bali wanaishi kwa upendo wa silaha ya msalaba. Kuwa mkristo siyo rahisi, lakini inakufanya uwe na furaha

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Liturujia ya leo inaweka moto katika mambo makuu manne ili kuishi kwa maisha ya kikristo: kupenda maadui, kufanya wema kwa wale wanao wachukia, kuwabariki wanaochukia , kusali kwa wale wanaowatendea vibaya. Ndiyo Kiini cha mahibiri ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 13 Septemba 2018, katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican mahali ambapo ameongozwa na Injili ya Siku Ya Mtakatifu Luka (Lk 6,27-38), na kufafanua kuwa, wakristo hawapaswi daima kujiingiza katika masengenyo au katika dhana za kushutumu, kwani ni mambo ambayo yanazaa vita, badala yake wakristo watafute daima muda wa kusali kwa ajili ya watu wanao wasumbua.

Kwenda kinyume na dhana ya dunia hii: Kuwa mkristo siyo rahisi, lakini inakutafanya uwe na furaha, na hija ambayo Baba wa mbinguni anaelekeza ni ile ya huruma, ambayo ndiyo amani ya ndani. Papa anaongeza kusema, Bwana anaelekeza jinsi gani maisha ya mfuasi yanapaswa kuwa, hasa kwa mfano wa kuishi heri au matendo ya huruma. Huo ndiyo mtindo wa Kikristo na  huo ndiyo mtido wa  wa Mkristo anathibitisha Papa. Lakini je nikifanya mambo hayo manne ya kupenda maadui, kufanya wema kwa wale wanao wachukia , kuwabariki wanaochukia , kuwaombea wanao watendea vibaya je mimi si mkristo. Ndiyo wewe ni mkristo kwani umepokea Ubatizo lakini hauishi kikristo. Unaishi kama mpagani au kwa roho ya kidunia.

Upendo mkuu  wa msalaba: Hakika ni rahisi kusengenya maadui au wale ambao ni tofauti na chama chako, lakini dhana ya mkristo inakwenda  kinyume na kufuata upendo mkuu wa Msalaba. Papa anaongeza, hatimaye, itafikia hatua ya kuenenda  kama wana wa Baba Yetu”. Ni huruma peke yake inafanana na Mungu Baba. “ Muwe na huruma kama aliyo Baba yenu amabye ni mwenye huruma”. Ndiyo njia ambayo inakwenda kunyume na roho ya dunia inayofikiri kinyume, kwa maana roho ya Mungu ahishutumi wengine.  Hiyo ni kwa sababu, kati yetu kuna mshtaka mkubwa, ambaye daima anakwenda mbele ya Mungu ili kutuharibu. Huyo ni shetani mshtaka mkuu.  Iwapo wewe unaingia katika dhana ya kutushumu, kulaani, na kujaribu kufanya madhara kwa mwingine, ni kuingia ndani ya mantiki ya mshtaka mkuu ambaye ni mharibifu.  Ni yule ambaye hajui neno 'huruma', hajui, hajawahi kuishi. Baba Mtakatifu amethibitisha.

Huruma ya Mkristo: Maisha kwa namna hiyo uangukia katika mialiko miwili: ule wa Baba na ule wa mshtaki mkuu ambaye anatusukuma kuwashutumu wengine na kuwaharibu”. Akifoa mfano Papa Francisko anasema, “Lakini huyo anayeniharibu”! je wewe huwezi kufanya hivyo na zaidi. Wewe huwezi kuingia katika dhana ya kuwa mshitaki.  “Baba mimi ninataka kushtaki”. Ndiyo jishitaki mwenyewe. Hiyo itakuwa vema kwako. Kwa maana njia moja ambayo ni muhimu kwa wakristo ni ile ya kujihukumu wenyewe. Wengine itakuwa jukumu la  huruma kwa maana sisi ni wana wa Mungu ambaye ni mwenye huruma

 

 

13 September 2018, 14:29
Soma yote >