Jishitaki binafsi mbele ya Mungu na tusiwe wanafiki!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Unafiki ndiyo mada iliyozungukia mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 15 Oktoba 2019. Ni katika kuangaziwa Injili ya siku ambayo inasimulia Yesu aliyekaribishwa katika chakula na mfarisayo na kushurumiwa na mwenye nyumba kwa sababu kabla ya kukaa mezani hakutawaza kama utamaduni wao. Baba Mtakatifu anasema, kuna tambia mabzo Bwana hawezi kuvumilia na hasa unafiki. Ndilo hili linatojitokeza katika Injili. Yesu aliakwa katika chakula lakinini wanamuhuku na siyo kufanya urafiki. Unafiki ni ule wa kujionesha kwa namna nyingine ambayo sivyo ulivyo. Ni kufirikia umejificha tofauti na jinsi unavyoonekana.
Unafiki unatoka kwa shetani aliye mwongo
Yesu havumilii unafiki anasema Baba Mtakatifu. Na maara nyingi anawaita wafarisayo wanafikia kama makaburi yaliyoakwa rangi.Hilo siyo tusi, ni ukweli Baba Mtakatifu anasisitiza kwani, kwa nje wewe ni mkamilifu, na unaye ng’aa , kwa usahihi tu, lakini kwa ndani wewe ni jambo lingine. Na anasema kwamba, tabia ya unafiki inatoka kwa yule mwongo mkubwa, Ibilisi. Yeye ndiye mnafiki mkubwa na wanafiki ni warithi wake. Unafiki ni lugha ya ibilisi, ni lugha ya ubaya inayoingia katika moyo wetu na kupandwa na ibilisi anasema Baba Mtakatifu Francisko. Haiwezekani kuishi na watu wanafiki, japokuwa wapo wengi. Kwa upande wa Yesu anapenda kuwaibisha unafiki huo. Yeye anatambua kwamba, itakuwa ndiyo tabia hiyo ya unafiki itakayompeleka hadi mauti kwa sababu unafiki haufikirii iwapo utumie njia halali au hapana unakwenda mbele, kwa wa mfano anasema: “Tunafanya kejeli; Shahidi wa uwongo? Tunatafuta shahidi wa uwongo”.
Unafiki ni sumu inayoua
Baba Mtakatifu Francisko amesema inawezekana mwingine akapinga kwamba kwetu hakuna unafiki. Lakina kufikiria hivyo ni makosa. Lugha ya unafiki, Baba Mtakatifu amesema hawezi kusema ni kawaida bali ni ya kawaida na ya kila siku. Huonekana kwa namna moja na kuwa kwa namna nyingine. Katika kugombania madaraka, kwa mfano, wivu hufanya uonekane kwa namna ya kuwa kijujuu tu na ndani kuna sumu ya kuua kwa sababu kila wakati unafiki huua, kila wakati, mapema au baadaye huua, amebainisha Baba Mtakatifu Francisko.
Dawa ni kujihukumu binafsi
Ni lazima kuponesha tabia hii, Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza na kuuliza kuwa,je dawa yake ni nini? Jibu lake ni kusema ukweli mbele ya Mungu na kujihukumu wewe binafsi. Sisi lazima kujifunza namna ya kujihukumu. Kwa kusema kuwa :nimefanya hilo, nimefikiria namna hii na kwa ukatili…Nina wivu mimi, mimi ninataka kuharibu huyo… kile ambacho kipo ndani mwetu na kusema mbele ya Mungu. Hili ni zoezi la kiroho ambalo silo la kawaida na lisiwe la kasumba, bali ni kujaribu kulifanya. Kujishitaki sisi wenye na kutazama dhambi ya unafiki katika uovu tulio nao ndani ya mioyo yetu. Kwa sababu shetani hupanda uovu na umwambia Bwana kuwa: tazama Bwana, mimi nikoje! na useme kwa unyenyekevu!
Petro alijitambua kuwa ni mdhambi
Tujifunze kujishitaki sisi wenyewe, Baba Mtakatifu amerudia kuhimiza hilo na kuongeza kusema “ni kitu labda chenye nguvu sana, lakini hivi ndivyo ilivyo. Mkristo ambaye hajui kujishtaki mwenyewe siyo Mkristo mzuri, anayo hatari ya kuangukia kwenye unafiki. Na kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka maombi ya Petro wakati alipomwambia Bwana:“ondoka kwangu kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi”. Hii iweze kutufanya kujifunza kujishitaki sisi wenyewe.