Papa:Amri ya Nne inakumbusha heshima ambayo wazazi wapewe!
Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Wapendwa kaka na dada habari za asubuhi! Katika mwendelezo wa safari ndani ya maneno ya Amri kumi, leo hii ni amri kuhusu baba na mama. Wanazungumzia heshima ambayo lazima wapewe wazazi. Je nini maana ha heshima hiyo? Neno hilo katika kiyahudi lililionesha utukufu, thamani,na kwa urahisi “ uzito”, wa jambo halisi. Siyo suala la kijujuu bali ni ukweli. Kuheshimu Mungu katika Maandiko matakatifu, ina maana ya kutambua hali halisi hata kutambua uwepo wake; kwa maana hiyo kueleza hata katika liturujia, lakini pia inasisitiza zaidi kumpa Mungu nafasi halisi ya uwepo wake. Kuheshimu baba na mama ina maana ya kutambua kwa namna hiyo umuhimu hata wa matendo ya dhati ambayo yanajielezea katika kujitoa kwa upendo na kuwasaidia. Lakini pamoja na hayo kuna jambo kuu zaidi ya hilo!
Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 19 Septemba 2018 wakati wa katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika viwanja vya Mtakatifu Petro mijini Vatican. Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua amri ya nne ya Mungu anasema mari ya nne ina tabia yake na ni amri ambayo ina matokeo. Kwa hakika,“ Kuheshimu baba yako na mama yako kama Bwana, Mungu wako anavyokuagiza ili uishi miaka mingi na uwe na furaha katika nchi ambayo Bwana Mungu anakupatia (Kumb 5,16). Kuheshimu wazazi inakupeleka kuwa na maisha ya furaha. Neno “furaha” katika Amri kumi za Mungu linaonekana katika mahusiano ya wazazi.
Hekima ya sayansi ya binadamu: Kwa miaka elfu ya hekima hii inasema wazi juu ya kile ambacho sayansi za binadamu zimeweza kutambua na kufanya kidogo tu kwa nusu karne: yaani, alama ya utoto kwa maisha yote. Wakati mwingine inaweza kuwa rahisi na inatokea kutambua mtu aliyekulia katika mazingira bora na yenye msimamo. Na kama ilivyo rahisi kugunda mtu anayetoka katika uzoefu wa maisha magumu ì au nguvu. Utoto wetu kidogo ni kama wino, unaojieleza katika hali halisi kwa namna ya kuwa, hata kama baadhi ya wengine wanatafuta namna ya kuficha majeraha yao ya asili.
Lakini amri ya nne inasema jambo jingine zaidi tena. Haizungumzi juu ya wema wa wazazi na kutaka kwamba, baba na mama lazima wawe wakamilifu. Inazungumza juu ya tendo la watoto, kunzia ile heshima wanayostahili kupewa wazazi, na kusema jambo maalumu na la uhuru: hata kama wazazi wote siyo wema, na si maisha ya utoto wote yana utulivu, lakini watoto wote wanaweza kuwa na furaha, kwa maana kufikiria katika maisha makalifu na furaha ambayo inategemea na utambuzi wa kujua ni nani alikuweka katika dunia hii.
Vijana wanaotoka katika historia ya uchungu: Kwa kutoa mfano juu ya Neno hilo, Baba Mtakatifu amesema, “tufikirie ni jinsi gani Neno hilo linaweza kujengwa katika vijana wengi ambao wanatoka katika historia ya uchungu na kwa wale wote walioteseka katika maisha yao binafsi ya ujana. Wengi ni watakatifu na waristo wengi, kwani baada ya kupitia maisha yao ya utoto kwa uchungu wameishi maisha yenye mwanga kwa njia ya neema ya Yesu Kristo, wamejipatanisha na maisha yao. Tufikirie kijana leo hii kijana ambaye ni mwenyeheri mwezi ujao anatatangawa Mtakatifu Sulprizio. Kwa maana akiwa na umri wa miaka 19 hakukana Imani yake na alikabiliana maisha yake na uchugu mkubwa, na yeye moyoni mwake alikuwa na utulivu na daima hakukana wazazi wake. Tufikirie Mtakatifu Camillo de Lellis , ambaye katika utoto wake alijenga maisha yake juu ya upendo na huduma; Mtakatifu Josephine Bakhita, aliyekulia katika utumwa wa kutisha; au mwenyeheri Carlo Gnochi, yatima na masikini; wakati huo huo Mtakatifu Yohane Paulo II aliye mpoteza mama yake akiwa bado mdogo.
Binadamu yoyote anapokea amri hiyo: Binadamu katika historia yoyote anakotekea anapokea amri hiyo, na inayoelekeza kufika kwa Kristo, kwa maana ni kwake yeye, alimwonesha Baba wa kweli ambaye anatoa maisha na kuzaliwa upya ( Yh 3,3-8). Mambo mengi tusiyo yatambua katika maisha yetu Baba Mtakatifu anaongeza, yanaangazwa wakati tunapogundua kuwa Mungu daima ametuandaa kwa ajili ya maisha kama watoto wake, mahali ambapo kila tendo ni utume wa ujumbe uliopokelewa kutoka kwake. Majeraha yetu yanaanza kuwa na nguvu iwapo kwa neema tunagundua ukweli wa mambo tusiyo jua hayapo tena kwa sababu ipi? Kwa ajili ya nani?” na kwa nini imetokea jambo hili. Je ni kwa mtazamo wa kazi ya Mungu amepita historia yangu? Hapo ndipo kila kitu kinapinduka na kugeuka kuwa thamani, kila kitu kinageuka kuwa cha kujenga. Uzoefu wangu na hasa wa kusikitisha na uchuhgu, katika mwanha wa upendo, unageuka kuwa kwa wengine, kwa yule ambaye ni kisima cha wokovu na kwa maana hiyo ni kuanza kuheshimu wazazi wetu, na kwa uhuru kama wa watoto wakubwa na kwa huruma ya kupokea vikwazo vyao.
Kuheshimu wazazi: Ni kuheshimi wazazi kwa maana wametupatia maisha! Kama wewe umekwenda mbali na wazazi wako, jitahidi na urudi kwao; labda ni wazee… lakini wamekupatia maisha. Baba Mtakatifu pia amebainisha, “ kuna hata tabia za kusema mambo mabaya na kati yake hata matusi”… onyo , “tafadhali msitukane wazazi wowote wale”. “Kamwe msitukane mama na baba. Wekeni uamuzi huo kwa kina kwa kusema, “ tangu leo sitomtukana mama au baba au mtu mwingine. Hao wamewapatia maisha na hawatakiwi kutukanwa”, Baba Mtakatifu amethibitisha.
Lakini maisha ya mshangao ni yale tuliyopewa na hatukulazimishwa: kuzaliwa upya katika Kristo ni neema ya kupokea kwa uhuru( Yh 1,11-13), hiyo ni tunu ya Ubatizo wetu , ambapo ni kwa njia ya Roho Mtakatifu Baba yetu pekee aliye mbinguni (lej Mt 23,9; 1 Kor 8,6; Ef 4,6).