Papa Francisko ametoa wito wa kusali kwa ajili ya amani ya nchi za Mashariki!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Mara baada ya katekesi yake tarehe 5 Juni 2019, Baba Mtakatifu Francisko amesalimia mahujaji mbalimbali kutoka duniani wakiwa ni makundi ya maparokia, na wawakilishi mbalimbali. Zaidi mawazo ya Baba Mtakatifu Francisko yamewaendea vijana, wazee. Wagonjwa na wana ndoa wapya.
Baba Mtakatifu amekumbusha maadhimisho ya Sikukuu ya Pentekoste
“Dominika ijayo tutaadhimisha Siku kuu ya Pentekoste. Bwana awakute mko tayari kupokea kwa wingi wa mapaji ya Roho Mtakatifu, neema ya zawadi zake iwashukie ndani mwenu na kuwaongeza nguvu mpya katika imani na kuwaimarisha matumaini kwa kuwapatia nguvu za utendaji wa upendo”.Amesema Baba Mtakatifu.
Wito wa sala ya dakika moja kwa ajili ya amani tarehe 8 Juni saa saba mchana masaa ya Ulaya
Aidha, “Kutumia dakika moja kwa ajili ya amani kwa sala kwa waamini; kutafakari kwa pamoja na yule ambaye aamini. Wote pamoja kwa ajili ya dunia ya kidugu”. Ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko wakati anatoa salamu kwa waamini wa lugha ya kitaliano ambapo kwa kawaida ndiyo wanahitimisha Katekesi yake ya kila Jumatano wakati wa salam. Baba Mtakatifu Francisko anasema kwa ni tarehe 8 Juni ambayo inakumbusha mwaka wa tano tangu kukutana mjini Vatican na Rais wa Israeli na Palestina, nikiwa pamoja na Patriaki Bartholomew. Saa saba mchana tunaalikwa kutumia dakika moja kwa ajili ya amani, na wote kwa pamoja kwa ajili ya dunia ya kidugu zaidi. Hata hivyo ni shukrani kwa Chama katoliki cha vijana kimataifa ambao wanaamasisha mkesho huo wa sala!
Na katika kukumbuka sikukuu hii ya Pentekeoste, Baba Mtakatifu pia amerudia kuwakumbushia hata makundi ya lugha tofauti. Katika lugha ya kipoland amesema “Tufungue akili zetu na mioyo yetu katika matendo ya Roho Mtakatifundani mwetu ili iweze kututakatifuza na kutufanya tuwe mashuhuda wa Kristo mbele ya dunia ambayo tunaishi”.