Katekesi ya Papa:Umoja hauondoi tofauti,unatufikisha mbele kama watoto wa Mungu!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Kabla ya katekesi ya Baba Mtakatifu tarehe 5 Juni 2019 katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa mahuaji na waamini waliofika kutoka pande zote za dunia, limesomwa Neno la Mungu kutoka Kitabu cha Waebrania 12, 1-2,: “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzungukayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu,mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake Ataifikia katika ukamilifu”. Baba Mtakatifu Francisko ameanza kuelezea juu ya ziara yake ya kitume aliyotimiza nchini Romani kwa mwaliko wa Rais wa nchi na Waziri Mkuu. Kwa njia hiyo anarudia kuwashukuru wote ikiwa ni pamoja na viongozi wote wa serikali na kidini na wahudumu wote walioshiriki kufanikisha ziara yake. Anamshukuru Mungu hasa kumruhusu mfuasi wa Mtume Petro kurudi katika nchi hiyo mara baada ya miaka 20 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II atembee nchi hiyo.
Ufafanuzi mfupi wa ziara yake iliyoongozwa na kauli mbiu tutembee pamoja
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwa ufupi, kama kauli mbiu ya ziara yake iliyokuwa inamwongoza kuwa ni “ kutembe pamoja”. Furaha yake ilikuwa si kuifanya kwa umbali au kutoka juu, bali kutembea katikati ya watu wa Romania kama mhujaji katika ardhi hiyo amesema. Mikutano mingi imeonesha thamani na mahitaji ya kutembea pamoja kati ya wakristo katika mpango wa imani na upendo ambao ni kati ya wazalendo na jitihada za raia wote.
Nchini Romania kuna wakatoliki, wakigiriki, walatino na waorthodox
Kama wakristo Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa: “tunayo neema ya kuishi kipindi cha mahusiano kidugu kati ya makanisa tofauti. Nchini Romania sehemu kubwa ya waamini ni wa Kanisa la Kiorthodox ambao wanaongozwa kwa sasa na Patriaki Daniel, ambaye amependa kumshukuru kindugu. Jumuiya ya Katoliki ya kigiriki na kilatino zina mwamko na ni hai kabisa. Umoja kati ya wakristo, japokuwa siyo kamili umesimikwa msingi wake mmoja katika ubatizo na kuwekwa mhuri wa damu na mateso ambayo wanateseka kwa pamoja katika kipindi cha giza nene la mateso, kwa namna ya pekee katika karne iliyopita, chini ya utawala uliokuwa unamkana mungu. Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Patriaki wa Sinodi Takatifu ya Kiorthodox nchini Romania anasema waliweza kuwa na mkutano mzuri ambao ulionesha mapenzi ya Kanisa Katoliki katika kutembea pamoja kwenye kumbu kumbu ya mapatano na kuelekea katika umoja kamili ambao kwa hakika watu wa Romania waliomba kinabiii wakati wa Ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II. Amesisitiza Baba Mtakatifu.
Umuhimu wa ukuu wa kiekumene wa ziara hiyo, uliitimishwa kwa sala ya maombi ya Baba Yetu ndani ya Kanisa kuu la Kiorthodox mjini Bucarest. Ulikuwa ni muda mwafaka na nguvu iliyojazwa na ishara maalum kwa sababu, Baba Yetu ni sala ya kikristo kwa dhati ambao ni urithi wa pamoja na kwa wabatizwa wote. Hakuna anayeweza kusema: “Baba yangu” na “Baba yenu”; hanapa: bali ni kusema “Baba Yetu” ambao ni urithi wa watu wote wabatizwa”. Amesisitiza Baba Mtakatifu na kuongeza kusema, katika sala hiyo waliweza kuonesha umoja ambao hauondoi utofauti kisheria. Na kwa maana hiyo “Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha kuishi daima kama wana wa Mungu na ndugu kati yetu”
Misa na Jumuiya Katoliki zilikuwa tatu wakati wa ziara ya Papa
Baba Mtakatifu akiendelea kuhusu ziara yake amesema kuwa, akiwa na Jumuiya Katoliki waliadhimisha Liturujia tatu za maadhimisho ya Ekaristi. Ya kwanza ilikuwa katika Kanisa Kuu la Bucarest, tarehe 31 Mei ikiwa ni sikukuu ya Bikira Maria Kumtembelea Elizabeth, ambayo ni picha ya Kanisa katika safari ya imani na upendo. Liturujia ya pili ya misa Takatifu ilikuwa ni katika Madhabahu ya Șumuleu Ciuc, kituo cha wanahija wengi. Mama Mtakatifu wa Mungu anawapokea watu waaminifu katika aina mbalimbali za lugha, utamadini na mila. Na liturujia tatu ya misa takatifu ilifanyika huko Blaj katika Kituo cha Kanisa la Kigiriki- Katoliki nchini Romania, kwa kuwatangaza wenye heri saba maaskofu wafia dini wa Kigiriki- katoliki. Baba Mtakatifu amesema kuwa, mashuhuda wa uhuru na huruma wanakuja kutoka katika Injili. Mojawapo ya wenyeheri ni Monsinyo Iuliu Hossu wakati akiwa gerezani aliandika: “Mungu ametutuma katika giza la mateso ili kutoa msamaha na kusali kwa ajili ya uogofu wa wote”. “Kwa kufikiri juu ya mateso mabaya ambayo walitendewa, maneno haya ni ushuhuda wa huruma”, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko.
Mkutano wa vijana na familia:kumkabidhi Mama Maria familia na vijana
Baba Mtakatifu aidha amebainisha kwa namna ya pekee kwamba kipindi mwafaka na cha sikukuu ilikuwa ya mkutano na vijana na familia uliofanyika huko Iaşi, mji wa zamani na kituo cha utumaduni ambacho ni muhimu, kipo katikati ya mashariki na magharibi. Ni mahlai panapotoa mwaliko wa kufungua njia za kutembea pamoja, katika utajiri wa utofauti na katika uhuru ambao haukati mizizi yake, bali ni katika kuchota mitindo ya ubunifu. Hata katika mkutano huo, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, ulikuwa na mtindo wa mama Maria na ambao ulihitimishwa kwa kumkabidhi Mama wa Mungu familia na vijana. Na hatimaye hatua ya mwishowa ziara yake ilikuwa ni kutembelea jumuiya ya warom wa Blaj. Katika Mji huo Warom ni idadi kubwa, kwa maana hiyo alipendelea kuwasalimia na kupyaisha wito wake dhidi ya kila aina ya ubaguzi na kwa ajili ya kuheshimu watu wa kila aina ya kabila, lugha na dini. “wapendwa kaka na dada, ninamshukuru Mungu kwa ajili ya ziara hiyo ya kitume na tumwombe yeye kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria ili ziare hiyo iweze kuleta matunda mengi kwa ajili ya Romania na kwa Kanisa katika ardhi hizo.