Papa Francisko:mpango wa kufufuka baada ya janga covid-19!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Jiwe kubwa lilikuwa limewekwa kaburini na wanawake ambao asubuhiya Pasaka kwalikwenda makabarini wasingeweza kuliviringisha na kuliondoa. Lakini hilo halikuweza kuwasimamisha. Hata katikati ya giza na kukatishwa tamaa, walikuwa na mifuko yenye manukato kwa ajili ya kuupaka mwili wa Mwalimu. Lakini baadaye walipata mshangao uliowafanya wawe na furaha. Kwa ghafla Yesu alitoka nje kukutana nao na kuwasalimia akiwambia “furahini. Kuwaalika katika furaha mbele ya janga kubwa hili la matokeo ambayo tunakumbwa mayo kwa sababu ya COVID-19 inawezekana kuleta hisia na mbaya kama vile ni matani yasiyokuwa na hamu. Papa Francisko anatambua kuwa kufungua tafakari yake kwa kutumia Injili ya Pasaka, simulizi ya ufufuko wakati wa virusi vya corona vilivyo sababisha vifo vingi inawezekana kuwa ishara ya ujinga, au kutokuwajibika.
Kila sehemu inatambua na duniani kote wanaomba ni nani anaweza kuondoa jiwe hili la kaburi la janga ambalo kati ya maombolezi na uchungu kwa wakati ujao unaohatarishwa “kuzika kila matumaini”. Wazee walio peke yao wametengwa, familia ambazo hawajuhi ni jinsi gani ya kupeleka sahani ya chakula katika meza yao, ugumu wa wahudumu wa afya na wafanya kazi wa umma ambao wamechoka.Wanahisi kuelemewa na mzigo huo na sasa ndiyo kila kitu utafikiri ni chenye neno la mwisho”. Anabainisha Papa: “ ikiwa kuna jambo ambalo tumejifunza katika kipindi hiki chote ni kwamba hakuna anayeweza kujiokoa peke yake. Mipaka inaanguka, kuta zinapasuka na hotuba zote zenye mawazo ya kiitikadi zinayeyuka mbele ya uwepo wa maonyesho ya udhaifu huu ambao tumeomba nao”
Mpango wa kufufuka
“Hayupo hapa Amefufuka! Ndilo kwa hakika tangazo hilo la Injili” ambapo Papa Francisko anapata sababu ya kina, si tu imani lakini pia hata kibinadamu katika “Mpango kwa ajili ya kufufuka” uliotangazwa na “Vida Nueva”, Gazeti moja la Kispanyola la Kanisa, ili ni moja ya gazeti muhimu la Kanisa kwa lugha za nchi hiyo, hivyo Papa Francisko anatoa mapendekezo ya matazamio mapya yanayoweza kufanyika mara baada ya Covid-19. Ndiyo mpango katika ubinadamu wenye hofu ambapo Papa anatoa ushauri. Ubinadamu wa hofu ya mitume ambao walikuwa wamekimbia kwenda mbali na ubinadamu wa uzoefu wa wafuasi wake ambao kwa nema ya tabia isiyolinganishwa na akili iliyo barikiwa ya wanawake walikwenda katika kaburi, kwa ujanja” pamoja na hayo yote hayo. Hata katika Dunia iliyojeruhiwa na virusi vya corona, Papa Francisko anabainisha kwamba tumeona “wengi wakitafuta kupeleka mbele mpako wa uwajibikaji wao ili kutunza na siyo kuhatarisha maisha ya wengine”.
Papa Francisko anaorodhesha mambo:“tumeweza kugundua watu wangapi waliokuwa tayari wanaishi na wameweza kukumbwa na janga la kubaguliwa na sintofahamu ambazo wameendelea kupambana nazo, na wameweza kuwasindikiza na kuwasaidia”. Tumeona “mpango uliotumiwa kwa madaktari, wauguzi, watu wanaoenelea kujaza super market, watu wa kufanya usafi, walinzi, wasafirishaji, vyombo vya usalama, watu wa kujitolea, makuhani, watawa, babu na wazee, walimu na watu wengine wengi”. Wote hawa anathibitisha Papa Francisko, “hawakukosa kufanya kile ambacho walihisi kuweza kufanya na ambacho walitakiwa kutoa”.
Habari iliyoletwa na wanawake katika hali isiyo tarajiwa
Habari mpya ilikuwa ya kushangaza sana ya Ufufuko ambayo iliwafikia wanawake katika halis sawa wakati tulikuwa tunajikita kufanya jambo la haki. Ishara yao ya huruma inabadilika. Mpako wa mafuta yao Papa anasisitiza , “ siyo kwa ajili ya kifo, bali kwa ajili ya maisha”. Habari ile inawaruhudu kuvunja mzunguko ambao ulikuwa unawazuia wao kutazama kuwa jiwe lilikuwa limeviringishwa tayari. Hali kama hii kwa mujibu wa Papa Francisko ni “ tumaini letu” ambalo linafungua mpasua katika hali ya sas ana kuturuhusu “kutafakari hali halisi ya mateso kwa mtazamo uliopyaishwa”. Mungu anasema, “ hawaachi watu wake, daima yuko nao hasa wakati wa uchungu anakuwapi karibu zaidi”.
Kadhalika Papa Francisko anarudia tena kusema “ Ikiwa tumejifunza kitu katika kipindi chote hiki, ni kwamba hakuna yoyote anaweza kujiokoa mwenyewe”, kwa maana hiyo anasisitiza “ ni dharurua kuchagua na kupata pigo la Roho “ lile linaloweza kutoa msukumu pamoja na wengine katika mwendelezo ambao unaweza kushuhudia na kutathimini maisha mapya ambayo Bwana anataka kutoa katika kipindi hiki dha thadi cha kihistoria. Kwa mujibu wa Papa Francisko “ kipindi hiki ni mwafaka cha Bwana, ambaye anataka kwetu tusiridhike au kutofurahia lakini huu ni wakati mzuri wa Bwana, ambaye anataka tusiridhike au kutofurahia na hata kidogo kuturekebisha kwa mantiki ya vitu mbadala au vya ubunifu wa kishufaa, vinavyotuzuia kuchukua umakini wa athari na matokeo mabaya ya kile ambacho tunakiishi. Huu ni wakati sahihi wa kutia moyo na kuhimiza mawazo mpya ya uwezekano na ukweli kwamba ni Injili pekee yake inaweza kutoa”
Mshikamano ni kinga ya kwanza ya kuzuia
“Dharurua kama ya COVID-19 inashindwa awali ya yote na dawa ya kinga ambayo ni mshikamano, anakumbusha Papa kwa kutumia maneno yaliyomo katika Hati ya “janga na udugu wa ulimwengu” iliyotangazwa na Taasisi ya Kipapa ya Maisha kunako tarehe 30 Machi 2020. Mshikamano ni fundisho ambalo litavunja imani mbaya ambazo tulizamishwa na ituruhusu tuhisi kwa upya kama mafundi wataalam na wahusika wakuu wa historia ya pamoja na kwa hivyo, kujibu pamoja dhidi ya mabaya mengi ambayo yanatesa mamilioni ya ndugu ulimwenguni kote. Hatuwezi kuruhusu kuandika historia ya sasa na ya baadaye katika migongo yetu kwa kwa mateso ya wengi”.
Uhakika wa Papa ni kuwa na umoja
Papa anao uhakika kuwa “Ikiwa tutakuwa na mwenendo wa kutenda kwa, hata mbele ya majanga mengine yanayotusumbua, tutaweza kuwa mantiki halisi”. Hata hivyo anajikita kutoa mlolongo wa maswali ambayo majibu yake yanaweza kutolewa na sayari hii. “ Je tutaweza kutenda kwa uwajibikaji mbele ya njaa ya watu wengu wanaoteseka kwa kutambua kuwa kuna chakula cha kutoka wote? Tutaendela kutazama sehemu nyingine kwa ukimya wa makusudi mbele ya vita vinavyokuzwa tamaa za kutaka kutawala na madaraka? Tutakuwa tayari kubadili mitindo maisha ambayo yanachochewa na hamu ya kutawala na nguvu? Tutakuwa tayari kubadilisha maisha ambayo husababisha wengi kuzama kwenye umaskini, kuhamasisha na kututia moyo wa kuishi maisha mema zaidi na maisha ya wanadamu ambayo yanaruhusu usawa usambazaji wa haki za rasilimali
Kama jamuiya ya kimataifa, je! “Tutachukua hatua muhimu za kumaliza uharibifu wa mazingira au tuendelee kukataa ushahidi huu unaoonekana? Utandawazi wa kutokujali utaendelea kutishia na kujaribu njia zetu ... kwamba tunatakiwa tupate kinga muhimu za haki, upendo na mshikamano . “Hatuogopi – anahitimisha Papa Francisko - kuishi njia mbadala ya maendeleo ya upendo, ambayo ni “ustaarabu wa tumaini: dhidi ya huzuni na hofu, uchungu na kukata tamaa, uzembe na uchovu. Ustaarabu wa upendo hujengwa kila siku, mfululizo usiokatika. Inahitaji jitihada kwa wote. Kwa namna hiyo jumuhiya yenye kujikita kisimamia katika jitihada za ndugu”.