Tafuta

2021.09.15 ;isa katika madhabahu ya Mama maria wa Mateso saba nchini Slovakia:Mapadre wakiwa katika misa 2021.09.15 ;isa katika madhabahu ya Mama maria wa Mateso saba nchini Slovakia:Mapadre wakiwa katika misa 

Slovakia:Baada ya ziara ya Papa ni msaada kwa ajili ya Cuba

Jumapili tarehe 26 Septemba, 2021 Makanisa yote nchini Slovakia,itakusanya sadaka kwa ajili ya wenye kuhitaji nchini Cuba.Hii ni kutaka kuweka kwenye matendo ya kile ambacho Papa Francisko aliacha amewashauri katika ziara yake ya kitume ya hivi karibuni.Lengo lao ni kushirikishana kama wengine walivyowasaidia wakati uliopita.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maaskofu katoliki nchini Slovakia, wametangaza kuanza kukusanya sadaka ya  ufadhili kwa ajili ya kusaidia wenye kuhitaji nchini Cuba. Dominika tarehe 26 Septemba 2021 makanisa yote nchini humo yatafanya makusanyo hayo. Maaskofu wamewageukia waamini wote kwa uthibitisho wa barua yao iliyosomwa tarehe 19 Septemba 2021 na mapadre wa makanisa yote. Ukusanyaji wa fedha hizo unataka kuwa ni moja ya tunda ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu ambaye alirudia kutoa mwaliko ju ya kuwa umakini kwa ndugu kaka na dada wanaoishi katika matatizo na mara nyingi wanabaki wamesahauliwa.

Katika taarifa yao kwenye ofisi ya vyombo vya habari ya Baraza la Maaskofu nchini Slovakia. Inasema kuwa “kwa kutiwa moyo na ziara na ushauri wa baba Mtakatifu Francisko, maaskofu nchini Slovakia wameamua kufanya makusanyo ambayo yatafanyika katika makanisa yote nchini Solakia Dominika ijayo tarehe 26 Septemba 2021 ili kusaidia wenye kuhitaji nchini Cuba. Makusanyo hayo yanatakauwa kuwa moja ya matunda ya ziara ya Baba Mtakatifu ambayo amerudia na kukazia mwaliko wa umakini kwa kaka na dada kwenye matatizo na ambao wanabaki wamesahauliwa. Kuhusiana na matatizo nchini Cuba yamezidi kuwa makubwa zaidi kufuatia na janga la sasa la UVIKO.

Hali halisi imezidi kukua kwa umaskini wa vifaa katika chi hiyo na ambayo inakumbusha kuwa sisi tunayo mengi ambayo tunapaswa kushukuru, na wakati huo huo hatupaswi kuwasahau wale ambao hawana fursa ya namna hii. Lengo letu ni lile la kushirikishana kama wengine ambao wameshirikishna nasi wakati uliopita wakati sisi tulikuwa tunahitaji”.

Kwa maana hiyo Donimika ijayo maaskofu wa makanisa yotewatafanya makusanyo hayo  kwa ajili ya maskini wa Cuba na wanaomba ukarimu wao katika roho ya kutiwa moyo ambayo wao wanayo na wamehisi wakati wa ziara ya Baba Mtakatifu. Kwa kutanguliza shukrani ya dhati, wanawabariki na kwamba Mungu awakirimie kwa yote.

20 September 2021, 15:50