Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Presto
Ratiba Podcast
2021.10.07 Papa amekutana na Wajumbe wa Kikundi mchanganyiko cha Kazi cha waorthodox na Katoliki cha Mtakatifu Ireneo 2021.10.07 Papa amekutana na Wajumbe wa Kikundi mchanganyiko cha Kazi cha waorthodox na Katoliki cha Mtakatifu Ireneo 

Papa:amani ya Bwana sio amani inayoweza kujadiliwa

Papa Francisko amekutana na Kikundi mchanganyiko cha wachungaji wa Kanisa la Kiarothodox na Katoliki kiitachwa cha “Mtakatifu Ireneo”.Papa ametangaza uamuzi wa kumtangaza hivi karibuni Mtakatifu Ireneo wa Lion kuwa Mwalimu wa Kanisa kwa jina la “Doctor unitatis”,yaani mwalimu wa umoja.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko alhamisi 7 Oktoba 2021 amekutana na Kikundi mchanganyiko cha wachungaji wa Kanisa la Kiarothodox na Katoliki kiitachwa cha “Mtakatifu Ireneo. Wameunganika kwa mara ya kwanza kufanya mkutano wao wa mwaka mjini Roma. Papa anashukuru kazi yao ya kitaalimungu ambayo wanajikita nayo kuifafanua katika huduma ya Muungani kati ya wakatoliki na Waorthodox.  Amemshukuru Kardinali Kurt Koch Rais wa Baraza la Kipapa la Umoja wa Wakristo kwa hotuba yake ya Utangulizi. Ameshangazwa sana na kile ambacho ameelza kuhusuana na kazi yao ya kutafuta kwa pamoja njia tofauti za kiutamaduni ambazo zinaweza kutajirisha pamoja bila kupoteza utambulisho wao. Imekuwa ya kuvutia kile ambacho kimetafsiriwa kama “Gegensätze”, ameshukuru. Ni vizuri kukuza umoja ambao umetajirishwa na tofauti ambazo hazinguki katika vishawishi vya kufanana.  Daima huo ni mfano mbya sana ha siyo roho nzuri. Kwa kuhuishwa na roho hiyo wanao wanakabiliana ili kuelewa jinsi mantiki zilizopo zinazopingana katika tamaduni zetu, na badala ya kukuza mapingamizi hayo zinaweza kuwa fursa halali za kueleza imani ya pamoja ya kitume.

Papa Francisko amefurahishwa pia jina ambalo wamechagua, si kama Tume au kamati bali kikundi cha Kazi ambacho kinaunganisha katika udugu na uvumilivu wa mazungumzo, wataalam mbali mbali wa Makanisa na nchi tofauti, ambazo wanatamani kuzikuza  pamoja na kujifunza pamoja kwa ajili ya umoja. Msimamizi wao Mtakatifu Ireneo wa Lione ambaye kwa shauku Papa amethibitisha kwamba hivi karibuni  atamtangaza kuwa Mwalimu wa Kanisa kwa jina la doctor unitatis, yaani ‘Mwalimu wa Umoja’ ambaye alikuja kutoka Mashariki na kufanya uzoefu wa huduma ya kiaskofu katika Magharibi, alikuwa ni mtu wa kiroho sana  na kitaalimungu kati ya Wakristo wa mashariki na magaharibu. Jina lake Ireneo lina maana ya amani. Papa amesisitiza kuwa “Tunajua kwamba amani ya Bwana sio amani inayoweza kujadiliwa, matunda ya makubaliano ya kulinda masilahi, lakini ni amani inayopatanisha, ambayo inaungana tena kuwa umoja. Hii ndiyo amani ya Yesu. Mtume Paulo aliandikia kuwa Kristo: “Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha ukuta wa kati kilichotutenga ambacho ni uadui (Efe 2:14).

MKUTANO WA PAPA NA WAJUMBE WA KIKUNDI MCHANGANYIKO KATOLIKI NA KIORTHODOX
MKUTANO WA PAPA NA WAJUMBE WA KIKUNDI MCHANGANYIKO KATOLIKI NA KIORTHODOX

Papa amesema kwamba kwa msaada wa Mungu, wao wanajitahidi kubomoa kuta za utengano na kujenga madaraja ya ushirikiano. Papa Francisko amewashukuru kwa namna ya pekee kwa ajiili ya mafunzo waliyofanya na ambao siku chache imechapishwa kwa jina “kuhudumia muungano. Kufikiria tena uhusiano kati ya Ukuu na kisinodi. Tunaelewa vizuri kama ukuu na mchakato wa kisinodi katika Kanisa si mambo mawili tofauti. Kupitia uvumilivu wenye kujenga wa mazungumzo, hasa na Makanisa ya Kiorthodox, wanaelewa vizuri kwamba ubora na usawa katika Kanisa sio kanuni mbili zinazoshindana za kuwekwa sawa, lakini hali mbili ambazo zinaunda na kusaidiana katika huduma ya ushirikiano. Kama vile ubora unavyodhani zoezi la usawa, vivyo hivyo umoja ni pamoja na mazoezi yaliyo ubora. Kwa mtazamo huu, kile ambacho Tume ya Kimataifa ya Kitaalimungu ni ya kufurahisha, ikielezea kuwa umoja katika Kanisa Katoliki, kwa maana pana, inaweza kueleweka kama ufafanuzi wa vipimo vitatu: “wote” “wengine na umoja”. Kwa hakika umoja unamaanisha utekelezwaji wa hisia imani ya umoja wa ulimwengu wote, Huduma ya kuongoza kwa baraza la maaskofu, kila mmoja na baadhi ya makuhani na huduma ya umoja wa Maaskofu pamoja na Papa (Sinodi katika maisha na utume wa Kanisa, 2018, n.64).

Kwa hivyo njia yenye kuzaa matunda katika mazungumzo ya kitaalimungu na ya kiekumene inaweza tu kutegemea tafakari juu ya sinodi. Kiukweli, Papa ameeleza mara kadhaa imani yake kwamba katika Kanisa la sinodi, hata zoezi la ukuu wa Petro litaweza kupata nuru kubwa. Papa anaamini kwamba, kwa msaada wa Mungu, safari ya sinodi ambayo itafunguliwa katika siku chache kwenye majimbo yote Katoliki itakuwa fursa ya kuimarisha jambo hili muhimu pamoja na Wakristo wengine. Papa Francisko amehitimisha kwa kuwashuruku kwa ziara yao na kuwatakia matashi mema ya matunda ya kazi wanayoifanya jijini Roma katika Taasisi ya Mafunzo ya Kiekumene ya Angelicum. Amewawakabidhi utume wake katika sala na kuwabariki kwa Baraka ya Bwana na ulinzi wa Mama Matatifu wa Mungu.

07 Oktoba 2021, 17:48
Prev
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031     
Next
April 2025
SuMoTuWeThFrSa
  12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930