Tafuta

Hija ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki: Lengo ni kujenga na kudumisha udugu wa kitume miongoni mwa Wakristo wa Makanisa mbalimbali. Hija ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki: Lengo ni kujenga na kudumisha udugu wa kitume miongoni mwa Wakristo wa Makanisa mbalimbali. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki: Udugu wa Kitume

Askofu mkuu Ieronymos II wa Kanisa la Kiorthodox la Athene na Ugiriki nzima akiwa ameambatana na ujumbe wake, Jumapili jioni tarehe 5 Desemba 2021 amemtembelea Baba Mtakatifu Francisko kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Ugiriki na kubadilishana mawazo na zawadi. Wametia saini kwenye kitabu cha wageni mashuhuri na kuombeana utume mwema, udugu na amani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa serikali, vyama vya kiraia na wanadiplomasia, Jumamosi jioni tarehe 4 Desemba 2021 alipata nafasi ya kumtembelea Askofu mkuu Ieronymos II wa Kanisa la Kiorthodox la Athene na Ugiriki nzima. Ni katika muktadha huu, Askofu mkuu Ieronymos II wa Kanisa la Kiorthodox la Athene na Ugiriki nzima akiwa ameambatana na ujumbe wake, Jumapili jioni tarehe 5 Desemba 2021 amemtembelea Baba Mtakatifu Francisko kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Ugiriki na kubadilishana mawazo na zawadi.

Wote kwa pamoja wakatia saini kwenye Kitabu cha Wageni Mashuhuri, huku Askofu mkuu Ieronymos II akimtakia Baba Mtakatifu safari njema ya kurejea mjini Vatican. Kwa upande wake, Baba Mtakatifu Francisko alionesha furaha yake kwa kukutana na kuzungumza na Askofu mkuu Ieronymos II wa Kanisa la Kiorthodox la Athene na Ugiriki nzima. Amemshukuru kwa wema wake wa kidugu, unyenyekevu na uvumilivu. Amemwomba Mwenyezi Mungu ili aweze kuwakirimia neema ya kutembea kwa pamoja katika udugu wa kibinadamu na amani. Mwenyezi Mungu aendelee kuyabariki Makanisa haya mawili na Bikira Maria Mama wa Mungu awasaidie katika maisha na utume wao!

Udugu wa Kitume
06 December 2021, 14:51