Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Cyprus na Ugiriki:Mungu anaishi katika jangwa zetu

Papa Francisko wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu huko Atene katika Ukumbi wa Matamasha wa Megaron,amesema kwamba jangwa ni sehemu muafaka kwa ajili ya uongofu na kupokea uwepo wa Mungu katika historia ya watu na katika historia ya maisha ya kila mtu.Video fupi inaonesha tukio la Misa Takatifu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko akihubiri wakati wa misa Takatifu aliyoiongoza Dominika tarehe 5 Desemba kwenye ukumbi wa Matamasha wa Megaron huko Atene, Ugiriki, amewaomba waamini kuomba neema ya kuamini na kwa kwamba ukiwa na Mungu mambo yanabadilika na kwamba Yeye anaponesha hofu zetu, anatakasa majeraha yetu na kubadili sehemu kavu kuwa chemi chemi ya maji. Kwa hakika Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuwatembelea wakimbizi katika kisiwa cha Lesbos, ikiwa ni siku yake ya Pili akiwa katika ziara yake ya kitume huko Ugiriki ameendelea huko Atene, ambapo ameadhimisha misa hiyo katika eneo linalofikiriwa la urithi wa kiutamaduni wa kitaifa.

Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021

Ukumbi wa matamasha wa Megaron ni mahali ambamo pameweza kusikika sauti za kifonetiki za kisasa zilizofungamana na maneno ya kale ambayo, kwa karne nyingi za historia, yamesindikiza kwa hakika utangazaji wa Injili huko Ugiriki, Ulaya na nje ya bonde la bahari ya Mediterania. Tamaduni zilizoenea kati ya Mashariki na Magharibi zimeonekana hata hivyo katika adhimisho la Ekaristi Takatifu ya Kilatino katika sala za waamini watu wa Mungu kwa  lugha ya Kigiriki, Kiarmenia na Kiingereza. Huko Atene na Ugiriki, mahali ambapo ukristo ulienea katika bara zima la Ulaya, Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake Dominika ya Pili ya Majilio,  ameelekeza maneno mawili muhimu ya Injili hiyo  ya siku hasa jangwa na uongofu.

Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021

Kwenye ukumbi wa Megaron ambao umegawanyika katika kumbi mbili kuu zilizo karibu, waamini 2,000 wameshiriki katika adhimisho la Ekaristi ambapo Papa amekumbusha kwamba, kabla ya kuzungumzia juu ya jangwa, Mwinjili Luka anataja watu wakuu wa wakati huo, mfalme Tiberio Kaisari, gavana Pontio Pilato, Mfalme Herode na viongozi wengine wa kisiasa wa wakati huo. Papa amesema:“Neno la Mungu halielekelezwi kwao, kama jinsi ambavyo mtu angetarajia, bali kwa Yohane, mwana wa Zakaria, aliye nyikani". Kutoka katika mistari ya Injili Papa amethibitisha kuwa "zinaibuka kejeli za hila hasa kutoka katika mipango ya juu ambapo wamiliki wa mamlaka wanaishi, mtu  kwa ghafla kutoka jangwani anapita na ambaye alikuwa  hajulikani na mpweke".

Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021

Papa Francisko amesema:“Mungu anashangaza, chaguzi zake zinashangaza: haziingii ndani ya utabiri wa kibinadamu, hazifuati nguvu na ukuu ambao mwanadamu wa kawaida hushirikiana naye. Bwana anapendelea udogo na unyenyekevu. Ukombozi hauanzii Yerusalemu, Atene au Roma, lakini  jangwani. Mkakati huu kama kitendawili unatupatie ujumbe mzuri sana kwamba kuwa na mamlaka, kuwa na utamaduni na umaarufu sio hakikisho la kumpendeza Mungu; kinyume chake, inawezekana kusababisha kiburi na kumkataa. Badala yake, inahitaji kuwa maskini wa ndani, kama jangwa lilivyo maskini”.

Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
Misa ya Papa katika Ukumbi wa Tamasha Megaron,Atene Ugiriki tarehe 5 Desemba 2021
05 December 2021, 18:22