Tafuta

Papa akukutana na vijana huko Atene:ndoto za udugu na uzuri wa Kanisa

Papa akizungumza na vijana huko Atene Desemba 6:“Sisi si Wakristo kwa sababu ni lazima,lakini ni uzuri.Kwa uthibitisho ili kuhifadhi uzuri huo,lazima tukatae kile kinachotaka kuuficha.Furaha ya Injili na mshangao wa Yesu hufanya kujikatalia na magumu huchukua nafasi ya nyuma.Kuwa Mkristo si kufanya mambo bali ni kumwachia Mungu akupende.Ni kutambua kwamba wewe ni wa pekee mbele ya upendo wa Mungu.

Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Papa ametoa wito mkubwa kwa vijana wa Ugiriki aliokutana nao huko Atene katika shule moja ya Shirika la Ursula,Jumatatu tarehe 6 Desemba 2021. Papa amenukuu moja ya bango lilik kuwa limeoneshwa na vijana wa Slovakia wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana mnamo mwezi Septemba iliyopita mwaka huu. Lilikuwa na maneno mawili tu: “Ndugu wote”. Papa amesema alivyopendezwa sana na kwamba mara kadhaa katika viwanja vya michezo kwenye mabango, au barabani wanaweka matangazo kwa ajili ya kujitangaza wao wenyewe, mawazo yao, timu zao, haki zao. Lakini bendera ya vijana hao ilisema jambo jipya. Papa ameongeza kusema kwamba: “ni vizuri kujisikia kama kaka na dada kwa kila mtu, kuhisi kwamba wengine ni sehemu yetu, si watu wa kujitenga nao”.

Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki

Papa hata hivyo amefurahia kuwaona pamoja wameungana kutoka katika nchi na historia tofauti na kwamba katika lugha ya kigiriki kuma msemo mmoja usemao:  fílos ine állos eaftós,’ yaani ‘rafiki ni mwingine kama mimi’. Kwa kuongezea amesema: “Ndio, mwingine ni njia ya kujijua binafsi. Bila shaka, ni vigumu kutoka nje ya eneo lako la faraja, ni rahisi kukaa kwenye sofa mbele ya Televisheni. Lakini ni mambo ya wazee na sio ya vijana. Kama vijana ni lazima kuguswa; wakati mtu anapohisi peke yake, ni kujifungua; wakati kuna kishawishi cha kujifungua binafsi ni kutafuta wengine, kufanya mazoezi katika 'gymnastics kwa  roho' hiyo”, Papa amewashauri vijana hao. Papa amesema: "Leo hii  kuna hatari ya kujisahau sisi ni akina nani na  kushughulikia ujuu juu kwa  kuoneshana maelfu ya meseji kadhaa zinazofanya maisha kutegemea jinsi tunavyovaa, kwa magari tunayoendesha na jinsi wengine wanavyotutazama".  Kutokana na mtazamo huo Papa kwa vijana hao amezindua kwa upya maneno ya  ushauri yaliyochongwa kwenye uso wa hekalu la Delphi yasemayo: “Jitambue binafsi”. Huo ni mwaliko  wa zamani zamani sana wa jitambue, ambao hata leo hii ni halali kabisa" kwa mujibu wa Papa.

Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Papa akutana na vijana wa Ugiriki
Papa akutana na vijana wa Ugiriki
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki

Papa akiendelea na hotuba yake kwa vijana amesema "Jitambue  kile unachostahili kuwa na sio kwa kile ulicho nacho. Wewe si wa hadhi  kwa sababu ya  chapa ya mavazi au viatu unavyovaa, lakini kwa sababu wewe ni wa pekee, wewe ni wa kipekee".  Taswira nyingine ya zamani na mpya aliyoichagua Papa Francisko ni ile ya ving'ora. Kwa kukumbuka historia ya kizamani kama  ile ya Ulysses katika safari ya kurudi nyumbani kwao, kwamba hata vijana pia katika maisha, ambayo ni safari ya ajabu kuelekea katika nyumba ya Baba, watakutana ving'ora. Kwa kufafanua zaidi amesema katika hadithi hiyo ilikuwa inawavutia mabaharia kwa wimbo wao wa kuwafanya wagonge miamba. Kiukweli, ving'ora vya leo hii,  amesema vinataka kuwavutia na kuwageuza kwa jumbe za kuvutia na zenye kusisitiza, ambazo huzingatia mapato rahisi, juu ya mahitaji halali ya uwongo, juu ya ibada ya ustawi wa mwili, ya kujifurahisha kwa gharama yoyote. Papa ameongeza: “Kuna fataki nyingi, ambazo huangaza angani kwa kitambo, lakini huacha moshi hewani tu”.

Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki

Papa Francisko ameendelea kusema kwa vijana kwamba: “ Sisi si Wakristo kwa sababu ni lazima, lakini kni wa sababu ni nzuri. Na kwa uthibitisho huo  ili kuhifadhi uzuri huo, lazima tukatae kile kinachotaka kuuficha. Furaha ya Injili na mshangao wa Yesu hufanya kujikatalia na magumu kuchukua nafasi ya nyuma. Kwa kuwashauri Papa amewaomba basi waanze kwa upya kuwa na mshangao. "Kuwa Mkristo si kufanya mambo bali ni kumwacha Mungu akupende; ni kutambua kwamba wewe ni wa pekee, wewe ni wa kipekee mbele ya upendo wa Mungu".

Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Mkutano wa Papa Francisko na Vijana
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki
Papa amekutana na vijana wa Ugiriki
06 December 2021, 11:50