Tafuta

Katika afla ya uzinduzi wa mwaka wa Masomo 2021/2022 wa Chuo Kikuu Katoliki cha Milano na kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzisha kwa chuo hicho Papa ametuma ujumbe wake Katika afla ya uzinduzi wa mwaka wa Masomo 2021/2022 wa Chuo Kikuu Katoliki cha Milano na kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzisha kwa chuo hicho Papa ametuma ujumbe wake 

Papa kwa Chuo kikuu Katoliki Milano:inahitajika wazo jipya kushinda ukosefu wa haki

Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu Milano katika fursa ya kutimiza miaka 100,kimezindua mwaka mpya wa masomo kwa ushiriki wa Rais wa Tume ya Ulaya Bi von der Leyen. Katika ujumbe kwa njia ya video, Papa Francisko anabainisha kuwa katika kukabiliana na dharura za sasa,inahitaji kupanga mitindo mipya ya mawazo.Kuelimisha sio kujaza vyungu vya udongo bali ni kuwasha moto.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Moto, matumaini na huduma ni maneno matatu yanayosikika katika ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya video ambayo yanaweza kuwakilisha Chuo Kikuu cha Moyo Mtakatifu cha Milano, Italia,  ambacho Dominika tarehe 19 Desemba 2021, kimezindua mwaka wake wa masomo 2021/2022, huku kikiwa na  fursa ya  kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa wake. Katika Afla ya kuzinduliwa mwaka wa masomo  ameshiriki hata Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Bi Ursula von der Leyen, ambapo ilitanguliwa na Misa Takatifu iliyoadhinishwa Katika Kinsa Kuu la Mtakatifu Mbrosi  Milano, kwa kuongoza na  Askofu Mkuu Mario Delpini.  Katika ujumbe wake kwa njia ya Video, wa Papa ambao umeoneshwa moja kwa moja katika Ukumbi Mkuu wa Chuo Kikuu, Papa ametoa matashi mema kwa siku  kuu hiyo muhimu na kubwa ya utamaduni wa kitaasisi ambacho  kilianzishwa na Padre Agostino Gemelli na wahudumu wake; pia kwa wazo la miaka hii 100 ya maisha ya Chuo Kikuu ambacho kinatambua utamaduni mmoja wa elimu msingi na kuwa na uhai wake,  shukrani kwa kujitolea kwa mamia ya wanawake na wanaume na kushuhudiwa na maelfu ya waliyopata digiri, shahada na tafakari kuhusu elimu kama moja ya njia muafaka kwa ajili ya ubinadamu ulimwengu wa historia.

Kabla ya kuonesha ukijuacho, jioneshe wewe ni nani kwa jirani

Mafundisho hayo  kwa mujibu wa Papa, ni kwamba Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, kilianza utume wake, shukrani kwa upyaisho wa kuthamanishwa kwa njia ya kizazi  urithi wa utamaduni na tasaufi ambayo inaunda utambulisho wao. Ni utambulisho ambao unaendelea na ambao haukati tamaa bali unaheshimu, na kukaribishwa kila toafuti, katika utambuzi ambao huko wazi na kuheshimu mwingine kwa kupelekea kuchanua hali ya kibinadamu. Kama msemo wa kizamani kwamba

 “kuelimisha sio kujaza vyungu vya udongo bali ni kuwasha moto” Na ndiyo moto huo ambapo Papa Francisko amejikita kuutafakari kwamba: Chuo Katoliki kialiwasha moto huo na kwa maana hiyo kuendeleza kwa sababu ndiyo moja ya mtindo wa kufanya ili kuwasilinao, kwa njia ya shuhuda binafasi na ile ya kijumuiya. Papa amesema “ Kabla ya kuonesha kile ambacho unajua, ni vema kuwasha moto kwa kushirikishana kile ambacho wewe ni nani. Mawasiliano hayo yanatokea shukrani kwa kukutana  kutokana na kujiweka karibu na mmoja na mwingine na kufanya chochote kwa pamoja”.

Anayeelimisha anatazama wakati ujao kwa imani na anatimiza tendo la elimu jumuishi

Papa Francisko akifafanua juu ya neno tumaini na kwamba ili kuweza kuweka wazi kile ambacho kinachangamotisha hasa katika elimu sasa, amesema utamaduni wa kibinafsi, ambao unajionesha kuwa ni  kinyume na ile ya sisi na kuhamasisha sintohafahamu ambazo zinapunguza thamani ya mshikamano na kukuza ule utamaduni wa kibaguzi. Kwa maana hiyo anayeelimisha, anatazama wakati ujao kwa imani na anatimiza tendo la elimu ile ambayo inajumuisha wadau wengi wa kijamii kwa namna ya kuweza kuwa na mafunzo na elimu fungamani. Papa amesisitiza kwamba kuna haja ya kujifungulia matumaini na maswali ambayo leo hii yapo bila kuogopa. Matumaini hayo yanahakikisha wakati ujao kwa kushinda misukumo inayozaliwa na woga mwingi ambao unahatarisha kushinda, kutazama sehemu moja na kujifungia ndani na uongo wa wakati ujao. Kujifunga wazi na ukarimu kwa mwingine ndiyo muhimu sana, kwa sababu inawezesha kuwa na uhusiano kamili kati ya kizazi na kupambana na adui zitokanazo na ubinafsi na ambo upo katika utamaduni wetu Papa amesisitiza. Hasa kwa kujenga kuanzia na madarasa ya Chuo Kikuu, uzalendo jumuishi ulio tofauti na utamaduni wa kubagua.

Chuo Kikuu kimekuwa na mipango ya ushirikiano kimataifa

Papa Francisko amesema mantiki hiyo anakumbusha mkataba wa elimu kimataifa uliohamasisha kukuza kwa wote usikivu wa maswali makuu yenye maana katika wakati wetu kuanzia na vizazi vipya mbele ya ukosefu wa haki kijamii, ukiukwaji wa haki na uhamaji wa kulazimisha.  Kwa maana hiyo kuna masuala ambayo Chuo Kikuu hakiweza kubaki kiziwi. Badala yake Chuo Kikuu Katoliki kinapongezwa na Papa Francisko kwa mipango ya ushirikiano wa Kimataifa, ambao umewahusisha watu mbali mbali katika sayari, msaada wa kiuchumu, kila mwaka wanafunzi wenye kuhitaji, kwa umakini kueleza walio wa mwisho na kuelekeza kwa wagonjwa ambao wanashuhudia jitihada za dhati na kuwatia moyo waendelea mbele katika njia hiyo.

Inahitajika wazo jipya la ubunifu ili kwenda mbele

Papa Francisko vile vile ametazama dunia ya sasa ambayo kwa ujumla inajitigemea kwa kubainisha kile ambacho kilifanya kutafisriwa wakati uliopita na ambacho kwa sasa hakuna matumizi ya kuelewa wakat ulipo na hivyo inahitajika kufanya mipango mipya ya mitindo ya mawazo ili kufafanua suluhishi katika dharura ambazo tunaitwa kukabiliana nazo, kuanzia na zile za mazungira hadi za kiuchumi, zile za kijamii, kama ilivyo hata za idadi ya watu. Papa amesema “sisi tunaweza kwenda mbele kwa tabaka la walioangaziwa. Lakini inahitajika wazo jipya na bunifu! Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, kinaweza kuwakilisha mahali muafaka kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano wa utamaduni. Ili kufanya hivyo inahitajika kurudi katika uhusiano wa dhati kati ya mkufunzi na mwanafunzi ambayo ni muhimu sasa na ndiyo uhusiano unaoendelea kwa njia ya wakati uliopo na wakati ujao, lakini kwa pamoja ambao wanaalikwa kufikiria, kupanga na kutenda wakiwa na maono ya nyumba yetu ya pamoja ya kesho kwa kuanzia na hali halisi ya dhati ya sasa.

Uvumilivu shauku na ujasiri vyote vinakwenda pamoja

Papa Franciko amewalekea wanafunzi kwamba katika enzi  hii iliyokanganyikiwa na kuwa na ugumu sana wa janga wasikate tamaa na kuacha kuibiwa matumaini  na kuacha wambukizwe na virusi vya ubinafsi, amewahimiza wasigeuze mizizi asili lakini kwa kujikita zaidi katika mizizi asili  ili kuendelea mbele kwa katika maisha. Na hatimaye, Neno la mwisho la Papa Francisko kwa ajili ya Chuo kikuu katoliki cha Moyo Mtakatifu ni kutafakari juu ya huduma ambayo amesisisitiza katika kufikisha miaka hii 100 , imejionesha  kuwa ni fursa ya kuwa waaminifu katika huduma ya Kanisa na kijamii, akiwatakia  kwamba roho ya huduma ibaki daima kuwa ndiyo utambulisho wa Jumuiya Katoliki cha Chuo Kikuu. Aidha ameshauri wandelee mbele katika utume wao wa elimu kwa ujasiri na uvumilivi, kwa kubeba mapingamizi na mambo ambayo haendi. Lakini kwa uvumilivi, shauku na ujasiri, vyote hivyo vinakwenda pamoja. Watafsiri ndani mwao na ujasiri na uvumilivi kama shauku kubwa ya huduma kwa ajili ya jamii nzima na hata kwa Kanisa.

UJUMBE WA PAPA KWA NJIA YA VIDEO KWA CHUO KIKUU KATOLIKI CHA MILANO
19 December 2021, 12:10