Tafuta

Papa Francisko:Jitihada za Papa Francisko kwa mwaka 2021

Mwaka kwa hakika wa Papa Francisko 2021 umeona jitihada nyingi uanzia na ziara tatu za kitume kimataifa na muhimu matukio ya ndani na nje ya Roma.Barua binafsi 8 za Motu proprio zilizochapishwa kwa mantiki ya kichungaji,mabadiliko mbalimbali,miito ya amani,mshikamano na udugu.Uhamasishaji wa kampeni ya chanjo na mengine mengi katika shughuli zake za kichugaji.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni safari tatu za Kitume kitamataifa, kuanzia na kwenye magofu nchini Iraq hadi nchini Slovachia na katika njiapanda ya mateso kwenye Kisiwa cha Lesvos. Barua binafsi 8 za Motu proprio, miongoni mwake ikiwemo ile ya  kutoa huduma altareni  kwa wanawake; mabadiliko ya mfumo wa mahakama wa Vatican, Na misa ya kizamani. Kuanzishwa kwa mara ya kwanza mchakato wa  Sinodi ambao unahusu majimbo yote ulimwenguni. Baadaye mikutano, Katekesi, matukio muhimu ya kimataifa nje na ndani ya Roma. Pamoja na hayo katikati, kulikuwa na operesheni kubwa kwenye utumbo mpana katika Hospitali ya Gemelli Roma. Kwa hakika inastahili kweli kurudia na kupitia mchakato wa mwaka mzima wa 2021, wa papa Francisko kwa kuzingatia ratiba yake na jitihada zake ambazo zilimwona akiwa mstari wa mbele kutimiza hayo kama Kharifa wa Mtume Petro, ambaye ameitwa kuchunga kondoo wake ulimwenguni kote.

Ni mwaka ambao huwezi kukataa jinsi ambavyo umekuwa na ukosefu wa uhakika, na vizingiti kutokana na dharura ya Uviko-19 na kwa kuzingatia hata hali halisi ya afya ya Baba Mtakatifu mwenye umri wa miaka 85 ambayo ilianza tayari kuonekana hasa kwa  kumletea matatizo ya mguu na kumsababishia maumivu ya kutokuweza kuongoza ibada ya shukrani  Te Deum, mnamo tarehe 31 Desemba 2020 na kuadhimisha Misa Takatifu ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu sambamba na siku ya Amani duniani mnamo tarehe Mosi Januari 2021. Kwa hakika mwaka ambao unafungw, na ambao ulifunguliwa na Papa akiwa ndani amefungwa kama alivyokuwa ameeleza mwenye akiwa katika Makataba ya Kitume kwa ajili ya sala ya Malaika wa Bwana za kila  Dominika na Katekesi, kwa sababu ya kuzuia mkusanyiko mkubwa ili kuzuia maambukizi ya virusi. Kutoka katika Jumba la Kitume, vyombo vya habari ulimenguni,na watu wake walikuwa wanachungulia 2021 wakiwa  nyuma yao na majeraha ya janga la UVIKO, ambapo Papa Francisko aliwambia: “ Ni matarajio ya mwaka huu ya kwamba inawezekana kuzaliwa kwa upya na tiba mpya, tusiache tiba. Zaidi ya chanjo ya mwili, kunahitajika chanjo ya moyo na ndiyo tiba. Utakuwa mwaka mzuri ikiwa sisi sote tutatunzana mmoja na mwingine…”

Neno la utunzaji kwa upande wa Baba Mtakatifu, ulitimilizwa kwa njia ya safari tatu za kimataifa katika sehemu ndogo za ulimwengu ulio jeruhiwa na vita, umaskini na uhamiaji. Mojawapo ya kwanza kati ya hizo , na si tu kwa kufuata orodha, ziara ya kitume nchini Iraq kuanzia tarehe 5-8 Machi 2021. Ziara ya Upapa, katika moja ya Nchi za Mashariki iliyokumbwa na vurugu za kijitahadi na wenye misimamo mikali. Uamuzi ambao ulikuwa umetangazwa mnamo 2020 na ambayo ilisimamisha kwa sababu ya maambukizi na usalama- Lakini pamoja na hayo Papa Francisko alipenda kwenda hadi mwisho na bila kuacha watu wakate tamaa ambao kwa miaka 20 kabla walishindwa kumkumbatia Mtakatifu Yohane Paulo II. Kati ya mateso ambayo yalimkaribishwa katika mtaa wa vumbi huko Baghdadi au barabara isiyo na rami ya Qaraqosh, Papa alijifanya kuwapo kama mhujaji, akikutana hata na kiongozi mkubwa wa ayatollah Ali al-Sistani, ambaye ni kitovu cha Uislam wa Kiishia. Na Kutoka Mosul mahali ambapo  janga la mateso na mauaji ya kikatili ya watu, Papa aliinua mbinguni kilio  dhidi yak ila aina ya vurugu zilizofanywa ka jina la Muungu.

Matukio ya Papa 2021

Kilio kama hicho kilisikia katika ziara ya Kitume nchini Slovacchia (12-15 Septemba) ambapo akiwa katika kumbu kumbu ya mnara wa maangamizi ya Wayahudi huko Bratislava,  Papa Francisko alizungumzia, kufuru hasa linapotumiak jina la Mungu katika kuharibu hadi ya binadamu, au kama ilivyo katika ghetto la Warom wa Luník IX, amabao wametelekezwa na ubaguzi, na ubaguzi wa kila aina. Kilio ambacho kilitoa wito na kisha kulaani kwamba "kuanguka kwa meli ya ustaarabu" ambayo inachukua sura ya waya zenye miiba na conatina zenye moto wakati wa kiangazi na baridi wakati wa kipindi cha baridi kali ambapo maelfu ya wahamiaji wanaishi katika hali ya kinyama katika Kituo cha Mapokezi na Utambulisho cha Lesvos, kilichotembelewa mwishoni mwa ziara yake ya kitume huko Cyprus na Ugiriki (2-6 Desemba). Kutokana na mshtuko huu kwenye milango ya Ulaya, baada ya kutazama machoni miili iliyojeruhiwa ya wanaume, wanawake na watoto, sauti ya Papa Francisko kilisikika kwa nguvu: “ tusiache bahari yetu, igeuke kuwa bahari ya vifo.

Papa akiwa katika mzunguko wa dunia, lakini mtazamo wake pia ni katika mageuzi ambayo yataanza ya Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium, ijayo ambapo Papa Francisko alichapicha tangu Januari hadi Novemba Barua Binnafsi za Motu Proprio kwa kutoa utangulizi wa mabadiliko na mapya katika muktadha wa shughuli za kichungaji, kiuchumi, na mahakama. Ya kwanza ilikuwa Spiritus Domini (11 Janauri ) ambayo ilikuwa inahuusu kwamba Huduma ya walei ya usomaji wa masomo Lector na kuhusumia alatareni ( Acolyte) wanaweza kukabidhiwa wanawake. Baadaye barua binafsi ya Motu proprio ya tarehe 16 Februari ambayo ilikuwa inasasisha sekta ya haki ya hukumu ambayo ilikuwa ni ya Katiba ya Kitume ya Pascite gregem Dei, iliyotiwa saini mnamo Mei 23, ambapo Kitabu kipya cha VI cha Sheria ya Kanoni za Kanisa kilitangazwa, kilicho na sheria ya vikwazo vya uhalifu katika Kanisa. Katika Barua yake binafsi Papa alisisitiza kuwa ni lazima kanuni zizingatie mabadiliko katika jamii na mahitaji mapya ya Watu wa Mungu, kwa sababu hiyo ni muhimu wakati fulani kurekebisha na kuzoea mabadiliko katika mazingira. https://www.vatican.va/content/francesco/en/apost_constitutions/documents/papa-francesco_costituzione-ap_20210523_pascite-gregem-dei.html

Mnamo tarehe 24 Machi, kwa kuzingatia upungufu ambao umeonesha usimamizi wa uchumi wa Vatican kwa miaka mingi na kuzidishwa kwa janga la Uviko, Papa aliamua kupunguza mishahara ya makardinali, wakuu na wa Watawa na kwa mtindo huo huo, mnamo Aprili 29 alianzisha udhibiti mkali wa kupambana na rushwa kwa kuthibitisha kwamba wasimamizi lazima watie saini tamko ambalo wanathibitisha kwamba hawana hatia au uchunguzi wa ugaidi, uchakachaji wa fedha, ukwepaji wa kodi, na kwamba hawataweza kuwa na mali katika maeneo ya kodi. Siku iliyofuata, tarehe 30 Aprili  uamuzi kwamba  Mahakama ya Mwanzo ya Vatican pia itafaa kwa kesi za jinai zinazohusu makadinali na maaskofu. Tena mnamo  tarehe 11 Mei 2021 Papa Francisko alichapisha  barua  yake Binafsi "Motu Proprio", "Antiquum ministerium" yaani “Huduma kale” ya Katekista. Katika barua hiyo ilikuwa inaonesha jinsi ambavyo Maandiko Matakatifu yanataja huduma mbalimbali zinazotolewa na Mama Kanisa. 

Katikati ya kiangazi, mnamo  tarehe 16 Julai, Papa akachapisha , Traditionis Custodes ili kufafanua kwa upya mbinu za kutumia Misale ya kale. Hati hiyo iliamsha hisia chanya kwa ujumla, lakini pia hata wasi wasi (dubia) kadhaa ambazo zilipokea jibu kutoka kwa Baraza la Kipapa la  Ibada na Nidhamu ya Sakramanto ya Kania  tarehe 18 Desemba 2021. Hatimaye mnamo tarehe 26 Novemba alichapisha Barua Binafsi, Motu Proprio, Mitis iudex Dominus Iesus” yaani ““Bwana Yesu Hakimu Mwema na Mwenye Haki. Kwa barua hiyo Papa ameanzisha Tume ya Kipapa ya Kuhakiki Utekelezaji wa Barua Binafsi kwa Kanisa Katoliki nchini Italia. Tume hii itakuwa chini ya Mahakama Kuu ya Rufaa ya Kipapa, “Rota Romana”.  Askofu jimbo anapaswa kutazama namna ya kupunguza gharama za uendeshaji kesi; inafuta ule utaratibu wa thibitisho la pili la hukumu, hivyo hukumu ya kwanza inatosha iwapo hakutakuwa na rufaa; na inamweka Askofu jimbo kuwa hakimu mwenyewe, ili kuamua kesi za ndoa zenye kuashiria ubatili ulio wazi wa ndoa. Kuhusu kesi, 2021 pia ulikuwa mwaka wa kesi mbili za kimahakama katika Mahakama ya Vatican: ile ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia katika Mahakama ya Mtakatifu Pio X, iliyoanza tarehe 14 Oktoba 2020 na kumalizika tarehe 6 Oktoba 2021, na kuachiliwa huru wa washitakiwa wawili, na kisha kesi inayoendelea kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za  Sekretarieti ya Nchi. Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Julai 27, ambayo hadi sasa imefikia kwa mara ya tano na imesalia katika mapambano ya kiutaratibu, na kuendelea mnamo tarehe 25 Januari 2022

Ni kuanzia mwanzo wa mwaka ambapo alikuwa anaumwa mguu na pia chanjo ya Pfizer ambapaoBaba Mtakatifu aliipokea mnamo tarehe 13 Januari. Ka maana hiyo katika historia ya Upapa, mwaka unaokaribia kuisha pia utakumbukwa kwa habari kuhusu afya ya Papa kulazwa katika hospitali ya Gemelli, tarehe 4 Julai, kwa ajili ya upasuaji wa utumbo mpana, ambapo aliweza kukaa kwa siku kumi na baadaya ya matibabu akarudi. Kutoka ghorofa ya kumi ya Hospitali ya Gemelli, Papa pia alichungulia kwa ajili ya kusali sala ya Malaika wa Bwana pamoja na baadhi ya watoto kutoka wadi ya Saratani na kutoa wito kwa huduma ya afya bora iweze kupatikana kwa wote. Operesheni hiyo ilitoa manano mengi hadi kufikia kwa baadhi ya uvumi juu ya kujiuzuru kwa Baba Mtakatifu. Kwa kujibu alikuwa mwenyewe katika mahojiano marefu na  Radio ya Uhispania ya Cope, huku akisema kwamba uamuzi kama huo haujawahi kuingia akilini mwake.

Matukio ya Papa 2021

Kwa 2021 pia ulikuwa mwaka ambao Papa Francisko alianzisha moja ya uvumbuzi muhimu zaidi kutoka kwa mtazamo wa kikanisa, kwa maana hiyo ufunguzi wa mchakato wa sinodi, itakayodumu  miaka mitatu, ambayo ilianzia chini hasa , kutoka kwa waamini na si tu hiyo pekee lakini kkutoka ulimwenguni kote hadi kufikia kilele chake mnamo 2023 kitakachowaona maaskofu katika mkutano mkuu jijini Vatican. Awamu tatu za mchakato wa safari hii mpya iliyotangazwa mwezi wa Mei na kufunguliwa kwa Misa katika takatifu Kanisa la Mtakatifu Petro mnamo tarehe 10 Oktoba 202i ni katika majimbo, bara, na kwa watu wote. "Sinodi si mkutano, kongamano la kikanisa, kongamano la masomo au kongamano la kisiasa, ... si bunge bali ni tukio la neema, mchakato wa uponyaji unaoongozwa na Roho Mtakatifu" alisema Papa Francisko akifungua mchakato wa Sinodi ma kuhimiza kusikiliza, kukutana na Bwana na wengine, bila kuzuia sauti. Kwa mwaka 2021, miito mingi sana imesikika ya Papa Francisko kuanzia na zile zinazopendekeza chanjo ya kupambana na UVIKO-19. Kwa upande mmoja, wito wa usambazaji sawa na upatikanaji wa haraka, hasa katika maeneo maskini zaidi duniani: Papa alisema: “Kila mtu, bila ubaguzi, hivi karibuni atapewa fursa ya kujikinga kupitia chanjo” wakati akiongoza Rozari kuomba neema ya kumalizika janga katika Bustani ya Vatikani mnamo tarehe 31  Mei 2021. Kwa upande mwingine, kutia moyo kutokubali kuwa na mashaka, habari za uongo au kugushi na itikadi na ili kupata chanjo kwa sababu kufanya hivyo ni tendo la upendo. Fursa hiyo ilithibitishwa tena na Makao makuu Vatican  mnamo  tarehe 22 Desemba, ilipoanzisha masharti mapya ya kuingia katika Jiji la Vatican kwa kuwa na cheti (Green pass) kinachoonesha kupata chanjo

Hatua kwa hatua, pia wito kwa ajili ya dunia na uhifadhi wa nyumba yetu ya pamoja, mazingira na ikolojia safi. Shauku ya kuendeleza Laudato iliyozinduliwa kwa upya katika Waraka wa Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu. Hasa katika siku ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa waraka huo, Papa Francisko aliwakutanisha wanasayansi na viongozi wa dini mbalimbali mjini Vatican kwa ajili ya mkutano uliokuwa unatazama  Cop26  ambayo ilifanyika huko huko Glasgow nchini Scotland ambao ulimalizika kwa kutiwa saini kwa ushirikiano katika hati ya kupunguza hewa ya uchafuzi hasi ziro .Miezi miwili kabla, tarehe 7 Septemba, akiwa na Patriki wa Constantinople, Bartholomew, na askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby, Papa alikuwa ametia saini wito  juu ya uharaka wa uendelevu wa mazingira na umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa wa nguvu kama hiyo pia, Papa Francisko ameweka mazingatio mengi juu ya  mada ya amani na upokonyaji silaha. Hatuwezi kusahau maneno yaliyosemwa, tarehe 7 Oktoba 2021, kwenye Ukumbi wa Colosseum, wakati wa  mkutano ulioandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio pamoja na wawakilishi wa dini mbalimbali. Baba Mtakatifu aliomba kupunguza fedha nyingi zinazotumika kununua silaha  na kupunguza matumizi ya kijesh na "kubadilisha zana za kifo kuwa zana za maisha, na kuwekeza katika elimu na afya.

Miongoni mwa mikutano mingi, licha ya janga linaloendelea alikutana na wakuu wa Nchi mbali mbali miongoni mwake akiwemo Rais wa Marekani Bwana Joe Biden, Bwana Emmanuel Macron wa Ufaransa, rais wa Tume ya Ulaya,  Bi Ursula von der Leyen, na hatimaye na Rais anayetimiza muda wake Rais wa Italia  Bwana Sergio Mattarella), pamoja na  viongozi wa kisiasa au mashirika ya kiraia, Papa Francisko hakuwasahau wale ambao katika Mkutano iliyomchagua mwaka 2013 alichagua jina la Maskini wa Assisi yaani  maskini. Hasa katika mji wa Mtakatifu Umbria, mnamo tarehe 12 Novemba 2021, Papa alikutana zaidi ya watu 500 katika hali ya umaskini na shida kutoka Italia na Ulaya, katika ziara yake ya pekee ya faragha nchini Italia, huko Assisi. Miongoni mwa shuhuda zenye kusisimua, nyimbo, sala, katikaKanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika, Papa alinyooshea kidole umaskini mpya kama vile wanawake wanaotendewa vibaya kwa kuzwa kama biashara, watoto watumwa, wenye njaa, wanaotupwa huku na huko katika ajali za meli, familia zinazoteseka na ukosefu wa usawa wa wafanyakazi wa kijamii, watu wasio na ajira, na akaomba kwamba maskini warudishiwe sauti na ut una hadhi yao.

Katika hali hiyo hiyo, ujumbe kwa njia ya video wa tarehe 16 Oktoba 2021 ulielekezwa kwa washiriki katika Mkutano wa IV wa Harakati za watu ambamo Papa Fransisko alizindua wito wa nguvu kwa wenye nguvu wa sayari ili kufanya kazi kwa ajili ya ulimwengu wa haki zaidi, unaounga mkono, wa kindugu, na kuomba kufutwa kwa deni la nchi maskini, kupiga marufuku silaha, kukomesha uchokozi na vikwazo, ukombozi wa hati miliki ili kila mtu apate chanjo, na kuzindua tena mapendekezo mawili ya kutekelezwa mara moja: mshahara wa chini na kupunguzwa. Kwa siku ya kazi. Matukio mawili muhimu yamepangwa kwa mwaka mpya 2022: Mnamo tarehe 27 Februari kutakuwa na mkutano ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu Italia CEI huko Firenze  na maaskofu na mameya mia moja wa nchi zinazopakana na Mediterania; tarehe 22-26 Juni, Mkutano wa 10 wa Familia Duniani jijini  Roma wenye kaulimbiu "Upendo wa Familia: wito na njia ya utakatifu". Kuhusu safari za kimataifa, ziara ya Canada imetangazwa (tarehe bado haijatolewa), katika muktadha wa mchakato wa maridhiano kati ya uaskofu na wenyeji, walioshtushwa na ugunduzi wa makaburi ya halaiki katika shule za makazi zilizokabidhiwa na serikali zamani kwa Makanisa mbalimbali ya Kikristo, likiwemo hata  lile la Kikatoliki.

Katika baadhi ya mahojiano, Papa Francisko pia alioneesha nia yake ya kusafiri  kwenda hadi Congo, Papua Guinea Mpya, Timor ya Mashariki na Hungaria, kwa siku zijazo, vile vile  mahojiano ya mwisho yalitolewa ambayo yalikuwa ni ya  mwezi Septemba wakati wa  Kongamano la Kimataifa la Ekaristi huko Budapest. Shauku nyingine ya hija ya Lebanon,  yenye lindi la mzozo mkubwa wa kibinadamu, kisiasa na kiuchumi na  shauku hiyyo haikupungua, katika nchi ambayo aliiombea pamoja na wakuu wa Makanisa ya Mashariki katika siku ya maombi ya kiekumene tarehe 1 Julai katika Kanisa la Mtakatifu Petro pamoja na shauku ya kwenda pamoja na Mkuu wa Kianglikan Welby, hadi Sudan Kusini, ambapo hivi karibunu Katibu wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, alikwenda  kuandaa mazingira ya kuwasili kwa Papa pengine mwaka ujao. Katika safari ya kurudi kutoka Atene, Papa hatimaye alisema kwamba kila wakati yuko tayari kwenda Moscow  Urusi kukutana tena, baada ya mahojiano ya 2016 huko Cuba, na Patriarki wa Moscow na Urusi yote Cyril (Kirill).

31 December 2021, 18:04