Tafuta

2022.01.28 Pana na wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari Kikatoliki,ambao unaendesha tovuti ya “Catholic fact-checking”. 2022.01.28 Pana na wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari Kikatoliki,ambao unaendesha tovuti ya “Catholic fact-checking”. 

Papa ametoa wito wa kupambana na habari za kugushi&kuheshimu watu

Papa Francisko amekutana na wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kikatoliki,ambao unaendesha tovuti ya “Catholic fact-checking”,”Ukaguzi wa ukweli wa Kikatoliki" na kukuza taarifa sahihi kuhusu chanjo za UVIKO-19 na matumizi yake ya kimaadili.Papa amekuwa na mtazamo wa Kikristo juu ya wale wanaoeneza habari za uwongo,na kuwataka waandishi wa habari kubaki waaminifu na kuheshimu watu daima.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 28 Januari 2022, amekutana na wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Vyombo vya Habari vya Kikatoliki ,ambao unaendesha tovuti ya “Catholic fact-checking”, yaani ya 'Ukaguzi wa ukweli wa Kikatoliki" ambao wanajikita juu ya matatizo ya mawasiliano na kuhamasisha taarifa sahihi kuhusu chanjo za UVIKO-19 na matumizi yake ya kimaadili. Papa  amewakaribisha na kumshukuru Bwana Montagne kwa utangulizi wa maneno yake na kuwasalimia kwa moyo wote. Papa Francisko amesema kwamba,  tayari Mtakatifu Paulo VI katika ujumbe wake wa Siku ya Upashanaji habari mnamo 1972,  alikuwa anathibitisha kuwa “Mwanadamu wa kisasa anaweza kutambua kwa urahisi kwamba mitazamo yake mingi, hukumu, misimamo, mshikamano na upinzani ni kwa sababu ya ujuzi unaozidi kuwa mkubwa na wa haraka wa maoni na tabia, ambayo alipokea kupitia zana za mawasiliano ya kijamii”. Na alikuwa amebainisha tena kuwa:  “Ubora wa kazi ya mtoa taarifa sio tu katika kugundua kile kinachoweza kugunduliwa mara moja, lakini pia katika kutafuta vipengele vya uainishaji na maelezo kuhusu sababu na mazingira ya ukweli wa mtu binafsi ambao lazima aripoti. Kwa maana hii kazi hiyo inahitaji ukali katika mbinu za udhibiti na tathmini muhimu ya vyanzo, katika uaminifu wa data inayozingatiwa na katika uwasilishaji wao muhimu. Wajibu basi ni mzito zaidi ikiwa mwasilishaji anaitwa, kama mara nyingi inavyotokea, kuongeza vipengele vya uamuzi na mwelekeo kwa ripoti rahisi ya ukweli.

Mkutano na Chama cha Kimataifa cha Vyombo vya habari Katoliki
Mkutano na Chama cha Kimataifa cha Vyombo vya habari Katoliki

Papa Francisko katika hili ameongeza kusema jinsi ambavyo mwaka mmoja uliopita alisoma somo la kuvutia kuhusu jinsi maudhui ya hadithi yanavyobadilika kutokana na umakini wa mwandishi kwa kile kinachowasilishwa. Inavutia. Hiyo kazi imefanywa na profesa, Simone Paganini, wa Chuo Kikuu cha Aachen na kwamba inafurahisha jinsi anavyojifunza shida hii ya mabadiliko yaliyomo katika upitishaji wa kitu. Kwa maana hiyo akiendela amesema Papa Montini  yaani Paulo VI alikuwa anazungumzia mawasiliano na habari kwa ujumla, lakini matokeo ya maneno yake yanakaribiana sana na uhalisia hasa kwa kufikiria kuhusu taarifa potofu zinazosambaa kwenye wavuti leo hii.  Kwa hakika, unakusudia kuangazia habari za uwongo na taarifa zisizo kamili au za kupotosha kuhusu chanjo dhidi ya UVIKO-19, na umeanza kufanya hivyo kwa kutumia mitandao mbalimbali za Kikatoliki na kuhusisha wataalamu mbalimbali. Kutokana na hili, Mpango wao ulizaliwa kama muungano unaolenga kuwa pamoja kwa ajili ya ukweli na kwa maana hiyo Papa amewashukuru. Kwa kufanya hivyo ameendelea kufafanua kuanza na  neno "pamoja", kwamba hata katika nyanja ya mawasiliano ni jambo msingi. Kufanya mtandoa na kuweka pamoja ujuzi, fahamu na mchango kwa ajili ya kuweza kutoa habari kwa namna inayostahili, inawakilisha yenyewe  tayari ushuhuda wa kwanza.

Mkutano na Chama cha Kimataifa cha Vyombo vya habari Katoliki
Mkutano na Chama cha Kimataifa cha Vyombo vya habari Katoliki

Katika wakati huu wa kujeruhiwa na janga na migawanyiko mingi hata maoni, tendo la kukaa katika mtandao kama muwasilishaji mkristo tayari ni ujumbe. Mahali pakuanzia, ni ujumbe, Papa amesisitiza.  “Hatuwezi kuficha ukweli kwamba kwa wakati huu, pamoja na janga hili, habari nyingi za uongo zinazoenea, ambazo ni, mabadiliko ya ukweli yenye msingi wa hofu, ambayo katika jamii ya kimataifa hufanya  maoni yasikike  juu ya habari za uwongo na ikiwa sio za kutungwa. Katika hali hii mara nyingi, bila kujua inawezekana pia kuchangia, kuzidisha na kuingiliana kwa habari na maoni yanayoitwa ya kisayansi, ambayo mwishowe husababisha mkanganyiko kwa msomaji na msikilizaji. Kutokana na hiyo ni muhimu kuwa mtandaoni na kufanya ushirikiano na utafiti wa kisayansi juu ya magonjwa, ambayo yanaendelea na inaruhusu wote kupambana nayo vizuri zaidi. “Uwezo lazima ushirikishwe, sayansi lazima ishirikishwe kwa pamoja. Hii inafaa hata kwa chanjo. Ni dharura kusaidia Nchi ambazo zina kidogo , lakini lazima kufanya mipango ya muda mrefu na siyo yenye mtazamo wa haraka ya mataifa tajiri kutaka kukaa na usalama zaidi. Dawa zinapaswa kusambazwa kwa heshima", Papa amekazia na kuongeza kusema "tafadhali, sio kama zawadi za kusikitisha". Ili kutenda mema kweli ni muhimu kukuza sayansi na matumizi yake muhimu. Kwa maana hiyo, kuwa na taarifa sahihi, kusaidiwa kuelewa kwa misingi ya takwimu za kisayansi na si habari za uwongo, ni haki ya binadamu. Taarifa sahihi lazima zihakikishwe zaidi ya yote kwa wale ambao wana uwezo mdogo, kwa wadhaifu zaidi na kwa wale walio katika hatari zaidi.

Neno la pili, ambalo Papa Francisko amependa kulieleza baada ya "pamoja", ni  "kwa pamoja". Papa amesema kuwa ni neno dogo sana lakini lenye kufichua. Linatukumbusha kwamba kama Wakristo tunapinga udhalimu na uongo, lakini daima kwa ajili ya watu. Hata kama dhumuni la muungano wao ni kupambana dhidi ya habari potovu, kupinga habari za uwongo (Fake news) na upotoshaji wa dhamiri za walio dhaifu, hatupaswi kamwe kusahau tofauti msingi kati ya habari na watu. Habari za uwongo lazima zipingwe, lakini watu lazima waheshimiwe kila wakati, ambao mara nyingi hufuata bila kuwa na onyo kamili na uwajibikaji. Mwasilishaji Mkristo anafanya mtindo wa kiinjili kuwa wake, anajenga madaraja, ni fundi wa amani pia na zaidi ya yote katika kutafuta ukweli. Mtazamo wake sio wa kupinga watu, hauchukui mitazamo ya kuwa na ubora, haurahisishi ukweli, ili asije akaingia kwenye imani ya kisayansi. Hakika, sayansi yenyewe ni njia endelevu ya kutatua matatizo. Ukweli siku zote ni mgumu zaidi kuliko tunavyoamini na lazima tuheshimu mashaka ya watu, wasiwasi, maswali, kujaribu kusindikizana nao bila kutowatendea vya kutosha. Papa Francisko ameshauri pia kuwa na mazungumzo na wenye shaka. Kama Wakristo ni lazima tuwe wa kwanza kuepuka mantiki za upinzani na kurahisisha, daima tukijaribu kuwakaribia, kusindikiza, kujibu kwa utulivu na hoja ya maswali na pingamizi.

Mkutano na Chama cha Kimataifa cha Vyombo vya habari Katoliki
Mkutano na Chama cha Kimataifa cha Vyombo vya habari Katoliki

Papa Francisko amehimiza wataalamu hao wajaribu kufanyia kazi taarifa sahihi na za ukweli kuhusu UVIKO-19 na chanjo, lakini bila kuchimba kama mitaro na bila kubagua. Janga hili linatualika kufungua macho yetu kwa kile ambacho ni muhimu, kwa kile ambacho ni cha thamani sana, kwa hitaji la kujiokoa pamoja. Kwa hivyo tujaribu kuwa pamoja na kamwe dhidi ya, bali pamoja kwa ajili ya. Papa Francisko aidha amesema wakumbuke kwamba upatikanaji wa chanjo na matibabu lazima uhakikishwe kwa kila mtu, hata maskini zaidi, kwa maana: “tutapona ikiwa tutaponywa pamoja”. Katika hili, Papa Francisko amependa kusisitiza jambo ambalo amekuwa akisema kila mara: "huwezi kutoka kwenye mgogoro peke yako; ama kwenda pamoja, au hakuna atakayetoka vizuri. Hatutatoka sawa: tutatoka tukiwa bora au mbaya zaidi. Kwa sababu mgogoro unatuweka katika matatizo na tunahitaji kutafuta ufumbuzi. Lakini shida, ni mtego wa kisaikolojia, ni wakati mzozo unaogeuka kuwa mzozo na mzozo haujatatuliwa bali lazima kupamba kwa na  umbali,lakini si kufanya upinzani, na hii ni kurudi nyuma kila wakati na sio kufanya mazungumzo, kwa ujumla".  Papa amesisitiza "Tusiruhusu kamwe mgogoro ugeuke kuwa mzozo. Hapana, ni mgogoro. Tuko kwenye mgogoro, tujaribu kuondokana nao pamoja”.

Hatimaye, tafakari fupi ya mwisho ni juu ya neno "ukweli".  Papa amesema wasicheke  kuangalia habari, kuwasilisha data au takwimu  ipasavyo, kuwa wao wenyewe kila mara wanap zitafuta. Utaftaji wa ukweli hauwezi kuelekezwa kwa mtazamo wa kibiashara, kwa masilahi ya wenye nguvu, kwa masilahi makubwa ya kiuchumi. Hapana! Kuwa pamoja kwa ajili ya ukweli pia kunamaanisha kutafuta suluhsho la kanuni zilizoundwa ili kuongeza faida ya kibiashara, inamaanisha kukuza jamii yenye taarifa, haki, afya na endelevu. Bila marekebisho ya kimaadili, zana hizi huzalisha mazingira ya itikadi kali na kuwaongoza watu kwenye misimamo hatarishi na huu ndio mzozo. Dawa ya aina yoyote ya uwongo ni kujiruhusu kutakaswa na ukweli. Ni kweli, na ukweli hutakasa. Kwa Mkristo, ukweli kamwe sio dhana tu kuhusu hukumu juu ya mambo, hapana; hii ni sehemu tu ya ukweli. Ukweli ni juu ya maisha yote. Katika Biblia, inabeba maana ya utegemezo, uthabiti na uaminifu. Ukweli ni kile kinachoweza kuegemewa ili kuepuka kuanguka. Katika maana hiyo ya uhusiano, yule anayetegemewa pekee  na kutegemewa kiukweli, na ambaye mtu anaweza kutegemewa "kweli", ni Mungu aliye hai.

Papa Francisko amesema hapo kuna uthibitisho wa Yesu:  “Mimi ndiye ukweli"(Yn 14: 6). Mwanadamu, basi, hugundua na kujigundua tena ukweli anapo upitia ndani yake kama uaminifu na kutegemewa kwa wale wanaompenda "(Ujumbe kwa Siku ya 52 ya Mawasiliano ya Kijamii 2018). Kufanya kazi katika huduma ya ukweli kwa maana  hiyo humaanisha kutafuta kile kinachopendelea muungano na kuhamasisha mema ya wote, si kile kinachotenga, kugawanya na kutofautisha. Sio kile kinachotuleta kwenye migogoro. Kwa kuhihimitimpa Papa Francisko ameaambia kwamba katika maombi yao wazingatie na kuwakumbuka  waathika  wa janga hili na familia zao. Na kuwakumbuka wale ambao, bila kuwa na virusi, walikufa wakitoa huduma ya wagonjwa. Ni mashujaa wa siku zetu, mashujaa wengi waliofichwa. Papa amewatakia wao na wahudumu wao kazi njema na kuwabariki sana, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.

HOTUBA YA PAPA KWA VYOMBO KATOLIKI
28 January 2022, 11:56