Tafuta

2022.01.24 Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Notre Dame,yaani Mama Yetu  la Mtakatifu Agostino. 2022.01.24 Papa Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Notre Dame,yaani Mama Yetu la Mtakatifu Agostino.  

Papa Francisko:Kuelimisha ni tendo la tumaini linabadili na kukarimu

Akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Shirika la Notre-Dame la Mtakatifu Agostino,Papa Francisko amepembua mada ya elimu kwa ajili ya vizazi vipya na kuwaalika kuzingatia kwa namna ya pekee wale wasiojiweza na wale ambao wana madhara ya kisaikolojia kutokana na mgogoro wa kiafya uliotokana na janga la UVIKO-19.Elimu inabadili mantiki nyingi na kuleta uwezo wa kukaribisha katika nyumba yetu ya pamoja ya kuishi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 24 Januari 2022, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Notre Dame, yaani wa “Mama Yetu”, wa Mtakatifu Agostino, mjini Vatican ambapo amemshukuru Mkuu wa shirika kwa maneno yake na kuwashukuru kila mmoja wa shirika kupitia wawakilishi hao ili waonesha kwao ukaribu wake kiroho wote. Pamoja nao amemshukuru Bwana wa kazi ya Roho wake ambayo imejionesha katika karama yao ya elimu, katika kuhudumia kizazi kipya, familia, kwa ajili ya ubinadamu fungamani na ulimwengu wa kidugu zaidi.  Papa Francisko amebainisha jinsi ambavyo leo hii tunajikuta katika changamoto ya mafunzo na elimu ya mtu binadamu. Kwa imani na uelewa wa kiinjili wa mwanzilishi wao Mtakatifu Pierre Fourrier na Mwenyeheri Alix Le Clerc, wamejikita katika elimu ya watu, katika imani, elimu moja ya haki na ukaribu wa maskini.

Wawe wafuasi wamisionari na jumuiya za matumaini mahli walipo

Katika nchi mbali mbali wanapotenda utume wao, Papa anawatia moyo kuwa wafuasi wamisionari na jumuiya za matumaini na furaha kwa sababu hatari kubwa ya dunia ya sasa na mambo yake mengi yanazibwa na utumiaji hovyo ambao ni huzuni wa kibinafsi unaotokana na moyo uliojaa kujitosheleza na furaha binafsi za kijuu juu na dhamiri zilizojitenga.  Ikiwa maisha ya undani yanajifungia kwa maslahi binafasi, Papa amesema, hakuna nafasi kwa ajili ya wengine na hawaingii maskini(Eg 2). Baba Mtakatifu akigusia mada waliyoichagua kuongoza mkutano wao kuwa “Mkataba wa Elimu kwa Shirika la Notre –Dame” na kwamba ni mwaliko wa nguvu ambayo inatafakarisha juu ya njia mpya zinazowezekana kwa ajili ya kifikia vijana katika hali zao za kawaida kwa lengo la kuchangia maendeleo yao fungamani. Kwa hakika safari ya maisha inahitaji kuwa na matumaini yenye msingi juu ya mshikamano, na mabadiliko yanahitaji mchakato wa elimu, kwa kujenga mifumo mipya yenye uwezo wa kujibu changamoto na dharura za ulimwengu wa sasa, kuelewa na kupata suluhishi za dharura za kila kizazi, ili kufanya uchanue ubinadamu wa leo hii na wa kesho.

Mbele ya changamoto zinazo wakumba vijana waongeze nguvu ya Injili

Papa Francisko ameongeza kusema, mbele ya changamoto na hatari ambazo zinawakumba vijana ni matarajio yake kwamba jitihada zao na shauku zao kwa kuongoza na nguvu ya Injili zinaweza kurudisha kwao ladha ya maisha na shauku ya kujenga jamii yenye hadhi katika jina hilo (Fratelli tutti 71). Papa Francisko anawategemea wao na kuwa na imani nao, Kanisa pia lina imani kwao. Kwa maneno yao, matendo yao na ushuhuda wao, wao wanapeleka ujumbe wa nguvu katika dunia ambayo inakataa aina za wanyonge. Na kama shirika lao wanaweza kunyeshwa kwa njia ya sala, na kubudu katika kisima cha wema na ukweli na kupata muungano na Kristo aliyekufa na kukufukaile nguvu za kuweka mtazamo chanya, mtazamo wa upendo  wa tumaini juu ya ulimwengu , kwa kuwa na umakini hasa wale wasio na fursa katika jamii. Na kwa namna hiyo utume wao wa kuelimisha unaweza kuzaa matunda yenye mafao katika umbu la watu kwa ajili ya wema wa jamii.

Karama inajidhihirisha katika upendo wa Kristo

Shukrani kwa karama yao ambayo inajikitia kugundua upendo wa Kristo kwa kila mtu na wanaweza kuchangia kufungua peo mpya na kuunda nafasi za udugu. Kwa hakika kuelimisha daima ni tendo la tumaini ambalo liaalika kushiriki na kubadilisha mantiki tasa na iliyooza ya kutokujali katika mantiki nyingine tofauti ambayo ina uwezo wa kukaribisha katika nyumba yetu ya pamoja ambayo wote wanaishi. Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha amesema katika wakati huu ambao Janga la UVIKO-19 limezalisha mgogoro katika mantiki nyingi kwa namna ya pekee kuhusiana na elimu na juu ya vijana, ameaomba wawe karibu na watu ambao wanaishi na upweke, huzuni na kukata tamaa kisaikolojia. Kwa hakika jambo lilofaa kwa wakati huu ni lugha ya ukaribu, lugha ya upendo, uhusiano na kusaidia jambo ambalo linagusa moyo, na kufika maisha, linaamsha matumaini na shauku (Christus vivit 221). Amewakabidhi wote kwa Bwana na Bikria Maria na kuwabariki kwa moyo. Wasishau lakini kusali kwa ajili yake. 

24 January 2022, 16:21