2022.01.10 Papa na wanadiplomasia 2022.01.10 Papa na wanadiplomasia 

Papa kwa wanadiplomasia:hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe!

Papa Francisko akikutana na wanadiplomasia mjini Vatican katika utamaduni wa kutakiana matashi mema ya 2022 amegusia masuala muhimu ya kibinadamu kuanzia na mapambano ya janga la uviko na matokeo yake ya kiuchumi na kijamii,maendeleo fungamani,elimu,utunzaji bora wa mazingira,kupiga marufuku silaha za kinyuklia,uhamiaji,wanawake,ajira,hadhi,haki ya binadamu na vita ulimwenguni.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Francisko, Jumatatu tarehe 10 Januari 2022 amekutana  na kuzungumza na Mabalozi pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa mjini Vatican, mkutanao ambao umekuwa ni utamaduni wa kutakiana matashi mema katika kila mwanzoni mwaka. Kabla ya hotuba yake ndefu sana, ailitanguliwa na Hotuba ya Balozi Georgios F. Poulides kutoka Cyprus ambaye ni Dekano wa Mabalozi pamoja na wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu kwa kuanza hotuba yake amesema “Jana kimemalizika kipindi cha liturujia ya Noeli kipindi cha maendeleo cha kusitawisha uhusiano wa kifamilia, ambao nyakati fulani hutukuta tumekengeushwa na tukiwa mbali, kutokana na shughuli nyingi, kama tunavyokuwa mara nyingi katika mwaka  katika jitihada nyingine nyingi”.  Katika muktadha huo ameelezea shauku ya kuendeleza roho hiyo wakijikuta pamoja kama familia kubwa, ambayo hukutana na kuzungumza. Kimsingi ndiyo lengo la kidiplomasia, kusaidia kuweka pembeni mambo yasiyo na ladha ya kuishi kwa binadamu, ili kukuza maelewano na kufanya uzoefu hasa wanapokutana na migogoro mingi ya kichini chini, na wanaweza kujigundua maana ya hisia ya umoja wa kina katika ukweli.

Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022
Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022

Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru kufika kwao katika mkutano wao wa mwaka ambao ni wa kiutamaduni, fursa muhimu kwa kutakiana pamoja matashi mema ya mwaka mpya na kwa ajili ya kutazama kwa pamoja katika mwanga na vivuli vya wakati huu wetu. Shukrani kubwa kwa namna ya pekee kwa  Bwana George Poulides, Balozi wa Cyprusa anayewakilisha nchi yake mjini Vatican na Dekano wa Mabalozi wote kwa maneno mazuri sana ambayo amemwelekea kwa niaba ya Muhimili mzima wa Kidiplomasia. Kwa njia yao, Papa amependelea wawafikishie salamu zake za upendo kwa wakuu wao  na watu wao ambao wanawawakilisha. Uwepo wao daima ni ishara muhimu ya umakini ambao unatolewa na Vatican kwa ajili ya nchi zao na kwa ajili ya nafasi ya Jumuiya ya kimataifa. Wengi wao wamefika kutoka katika miji mikuu kwa ajili ya tukio la siku ili kuungana na kundi kubwa la wale wanaokaa Roma Papa amebainisha.

HOTUBA YA PAPA KWA WANADIPLOMASIA

Baba Mtakatifu  katika hotuba yake ameelezea jinsi ambavyo siku hizi wanaona mapambano ya janga bado yanahitaji nguvu kubwa kwa upande wa wote na ikiwa ndiyo mwanzo wa mwaka mpya na matarajio ya jitihada hizo. Virusi vya Uviko, vinaendelea kuunda upekwe kijamii na kuongezea waathirika na kati ya waliopoteza maisha, Papa amemkumbuka Askofu Mkuu Aldo Giordano, Balozi wa Kitume ambaye alikuwa anajulikana na kupongezwa ndani ya Jumuiya ya Kidiplomasia. Na wakati huo huo amebainisha kwamba mahali ambapo chanjo imekuwapo, hatari za maambukizi makubwa zinapungua. Kwa maana hiyo ni matumaini ya Papa kwamba jitihada za kampeni ya chanjo zinaweza kuendelezwa iwezekanavyo kwa watu.  Lakini hiyo inahitaji amesisitiza jitihada kwa ngazi zai binafsi, kisiasa na Jumuiya nzima ya kimataifa. Kila mtu ana uwezekano wa kupata matunzo binafasi na ya afya,  ambayo inajitafsiriwa kama hata kuheshimu afya ya yule aliye karibu.

Utunzaji wa afya, unawakilisha ulazima kimaadili Papa amesema. Lakini kwa  bahati mbaya, bado  wanaendelea kuona jinsi tunavyoishi katika ulimwengu uliojaa mawazo ya kiitikadi. Mara nyingi habari zinafika za kugushi au zilizorekodiwa kidogo. Kila thibitisho la kiitikadi, linagusa uhusiano wa sababu za binadamu na hali halisi ya vitu vya kawaida. Janga kwa hakika linatulazimisha kutunza ukweli na kututaka tutazame uso kwa uso matatizo na kutafuta suluhishi. Chanjo haziwezi kuwa zana za miujiza tu katika uponyaji, lakini zinawakilisha kwa hakika njia ya  kufikia tiba na ambazo zinapaswa kuongezwa ili kufikia suluhisho zaidi la kuzuia magojwa. Lazima kuwepo jitihada za sera za kisiasa kwa ajili ya wema wa watu kwa njia ya maamuzi ya kuzuia na kuponya na ambayo yanawahusu hata wazalendo ili waweze kuhisi washiriki na wawajibikaji kwa njia ya maasiliano na hatua muhimu za kukabiliana nayo. Ukosefu wa maamuzi stahiki na mawasiliano ya wazi yanazua mkanganyiko na yanaunda ukosefu wa imani na kusababisha hatari za kutoelewana kijamii na kuongezea mivutano mipya na vile vile mivutano ya kijamii iliyonzishwa ambayo inadhuru maelewano na umoja.

Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022
Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022

Papa Francisko amesema kwamba nia kwa ujumla ya Jumuiya ya kimataifa inahitajika, ili wakazi wote duniani wapate huduma muhimu za matibabu na chanjo. Lakini kwa bahati mbaya, ni lazima ieleweke kwa uchungu kwamba katika maeneo yaliyo mengi ulimwenguni upatikanaji wa huduma za afya bado unabakia kuwa mbaya. Katika wakati mzito kama huu kwa wanadamu wote, Papa ametoa wito wake tena kwamba Serikali na taasisi binafsi zinazohusika zioneshe hisia ya uwajibikaji, kuendeleza majibu yaliyoratibiwa katika ngazi zote (za mitaa, kitaifa, kikanda, kimataifa), kupitia mifumo mipya ya mshikamano na zana, kwa  kuimarisha uwezo wa nchi zinazohitaji zaidi. Papa Francisko hasa, amehimiza Mataifa, ambayo yanafanya kazi ya kuanzisha chombo cha kimataifa juu ya maandalizi na kukabiliana na magonjwa ya milipuko chini ya maelekezo ya Shirika la Afya Duniani, kupitisha sera ya kushiriki watu kama kanuni muhimu ya kuhakikisha kila mtu anapata uchunguzi, zana, chanjo na dawa. Vile vile, ni muhimu  kuwa taasisi kama vile Shirika la Biashara Ulimwenguni na Shirika la Haki Miliki Duniani zibadilishe vyombo vyao vya kisheria, ili sheria za ukiritimba zisiwe vizuizi zaidi kwa uzalishaji na ufikiaji uliopangwa na thabiti wa utunzaji ulimwenguni kote.

Papa akutana na wanadiplomasia 10 Januari 2022
Papa akutana na wanadiplomasia 10 Januari 2022

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake ameelezea jinsi ambavyo kutokana na kufuata sheria zilizowekwa kwa mwaka 2020, kutokana na janga,  aliweza kukutana na viongozi wakuu wa Nchi na Serikali lakini pia hata Mamlaka ya kiraia na Kidini. Miongoni mwa mikutano hiyo ametaja ule mwezi  Julai 1,  ambao ulikuwa umejikita kwa kutafakari na sala kwa ajili ya nchi ya Lebanon. Papa ameongeza kusema kwa ajili ya watu wapendwa wa Lebanon ambao wanalazimika kuishi katika mgogoro wa kiuchumi na kijamii na inakuwa vigumu kwao kupata suluhisho na ambapo leo hii pia amependa kupyaisha ukaribu wake na sala wakati akiwa na matumaini ya kwanza mageuzi ya lazima na msaaada wa jumuiya ya kimataifa uweze kusaidia Nchi ibaki kidete katika utambulisho wa mitindo ya kuishi kwa amani na udugu kati ya dini  zilizomo nchini humo. Mwaka uliopita, 2021, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha alivyoanza tena hija za kitume. Mwezi Machi kwa furaha kubwa alikwenda nchini Iraq, kwa sababu Mungu alipenda hilo litokee na kama ishara ya matumaini baada ya miaka mingi ya vita na ugaidi. Watu wa Iraqi wanayo haki ya kupata hadhi ambayo inawahusu na kuishi kwa amani. Mizizi yake ya kidini na kiutamaduni ni ya miaka mingi sana kuanzia na Misopotamia ambayo ni mama wa ustaarabu, na ni hapo ambapo Mungu alimwita Ibarahimu ili kuanza historia ya wokovu, Papa amesisitiza.

Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022
Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022

Mwezi Septemba aidha alikwenda  Budapest ili kuhitimisha Kongamano la Ekaristi kimataifa na kwa maana hiyo aliendelea na safari hadi Slovakia. Papa amesema ilikuwa ni fursa kwake kukutana na waamini katoliki  na madhahebu mengine ya kikrsto kama pia kufanya mazungumzo na Wayahudi. Ziara hiyo pia ilimwoana akielekea nchini Cyprus na Ugiriki ambapo bado  amesema kumbu kumbu ziko hai na aliweza kujikita kwa kina kuhusu uhusiano wa ndugu na Waorthodox na kufanya uzoefu wa udugu kati ya madhehebu mengine ya kikristo. Baba Mtamatifu Francisko ameelezea alivyogusa sana katika safari hiyo na eneo la kisiwa cha Levos, ambao alijionea mwenyewe ukarimu kwa wale wanaotoa huduma yao kwa ajili ya kukaribisha na kusaidia wahamiaji, lakini pia kuona nyuso za watoto na watu wazima wanaokaribishwa katika vituo vya makaribisho. Katika macho yao aliona uchovu wa safari, hofu ya wakati usiokuwa na  uhakika, uchungu kwa ajili ya ndugu waliobaki nyuma na kufikiria nchi zao ambazo wamelazima kuziacha. Papa ameongeza kusema:“ Mbele ya nyuso hizi, hatuwezi kubaki na sintofahamu na hatuwezi kuendelea kujenga kuta na nyaya za miiba kwa madai ya kujilinda na usalama au kuwa na mtindo wa maisha”.

Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022
Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022

Kutokana na muktadha huo Papa  amewashukuru wale wote ambao binafsi na serikali wanaendelea kuhakikisha mapokezi na ulinzi wa ahamiaji kwa kuchukua wajibu na hata kuhamasisha ubinadamu na ufungamanishwaji wao katika Nchi ambazo zinawapokea. Papa anao anatambua matatizo ambayo baadhi ya Mataifa wanakutana nayo mbele ya mtiririko huo wa watu. Hakuna ambaye anaweza kufikiri  kuwa haiwezekani kufanya, lakini kuna utofauti mkubwa kati ya kukarimu,  licha ya vizingiti na matatizo kuliko kuwasukuma kanisa wasiingie. Na ili kuwezekana Papa amesema lazima kushinda sntofahamu na kutupilia mbali wazo la kwamba wahamiaji ni matatizo ya wengine. Matokeo ya njia hiyo yanaonekana  wasi katika ukosefu wa ubinadamu wengine mbele ya wahamiaji kwa kuishia katika kile kiitwacho Hotspot, mahali ambamo wanaishi kwa rahisi kunyakuliwa na uhalifu na wafanyabiashara haramu wa binadamu au kutafuta kwa sababu ya mahangaiko ya kukimbia na wakati mwingine kuishia kwenye kifo. Kwa bahati mbaya, Papa amesema  inapaswa pia kuzingatiwa kuwa wahamiaji wenyewe mara nyingi hubadilishwa kuwa silaha ya usaliti wa kisiasa, kuwa aina ya bidhaa ya mazungumzo ambayo inawanyima watu hadhi yao. Kutokana na hili Papa amependa kwa mara nyingine tena kupyaisha shukrani kubwa kwa Mamlaka ya nchi ya Italia, kwa sababu kuna baadhi ya watu ambao aliweza kwenda nao katika hija yake ya kwenda Cyprus na Ugiriki. Hii ilikuwa ni ishara kwa urahisi lakini yenye maana. Kwa watu wa Italia ambao wameteseka sana mwanzoni wa Janga, lakini  vile vile ambao wameonesha ishara za kutia moyo ili  kuanza kwa upya, Papa amewatakia  matashi mema na ili waendelea namna hiyo kuwa na roho ya ufunguzi wa ukarimu na mshikamano  daima ambao unawatofautisha kama wazalendo.

Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022
Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022

Papa Francisko wakati huo huo, anaamini kwamba ni muhimu sana Jumuiya ya Ulaya ipate mshikamano wake wa ndani katika usimamizi wa uhamiaji, kwani imeweza kukabiliana na matokeo ya janga hilo. Kwa hakika, ni muhimu kuunda mfumo madhubuti na mpana wa kusimamia sera za uhamiaji na hifadhi, ili majukumu yashirikishwe katika kupokea wahamiaji, kukagua maombi ya hifadhi, kusambaza upya na kuunganisha wale ambao wanaweza kukubalika. Uwezo wa kujadiliana na kupata suluhisho la pamoja ni mojawapo ya nguvu za Umoja wa Ulaya na ni kielelezo halali cha kukabiliana na changamoto za kimataifa ambazo zinawasubiri kimawazo. Hata hivyo suala la uhamiaji halitazami Ulaya tu, Papa ameongeza na kwamba hata kama kwa namna nyingine unatazama mtiririko mkubwa kutoka Asia na Afrika. Katika miaka hii hata hivyo kumeonekana wakimbizi wa Siria ambao wameongezea siku zilizopita hata wale wa Afghanstan. Kwa maana hiyo pia Papa amesema hawapaswi kusahau wingi wa watu wanaotoka katika bara la Amerika ya Kusini na ambao wanagusa mpaka wa Mexico na Marekani. Wahamiaji wengi wanatoka Haiti kwa kukimbia mikasa mingi ambayo imeikumba nchi hiyo kwa miaka sasa.

Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022
Hotuba ya Papa kwa wanadiplomasia 10 Januari 2022

Masuala ya uhamiaji,  ya janga na mabadiliko ya tabianchi, yameonesha wazi kwamba hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe, kwa maana hata katika changamoto za wakati wetu ni changamoto za ulimwengu mzima. Inabaki kwa namna hiyo kuwa na wasi wasi ambao mbele yake kwa sehemu kubwa ya matatizo yanaongezeka zaidi na zaidi na kugawanyika katika  kupata suluhishi. Hata hivyo Papa amebainisha jinsi ambavyo mara nyingi kuna ukosefu wa utashi wa kutaka kufunga dirisha la mazungumzo na udugu,na hili husababisha kuongezea mivutano na migawanyiko ambayo uzaa ukosefu wa uhakika na msimamo thabiti. Kinyume chake inahitajika  kurudisha maana ya utambulisho wa pamoja wa familia ya kibinadamu. Badala yake kinaoonekana ni kuongezeka kwa kutengwa, kuzuiliwa na kufungwa kwa pande zote ambazo kiukweli zinahatarisha zaidi umoja kwa pande nyingi, ambazo ni mtindo wa kidiplomasia ambao umeonesha uhusiano wa kimataifa tangu mwisho wa Vita vya Kidunia vya pili. Diplomasia ya pande nyingi imekuwa ikipitia mgogoro wa kuaminiana kwa muda, kutokana na kupungua kwa uaminifu wa mifumo ya kijamii, na kiserikali. Maazimio muhimu na maamuzi mara nyingi huchukuliwa bila mazungumzo ya kweli ambapo nchi zote zina sauti. Ukosefu huu wa usawa, ambao umedhihirika kwa kiasi kikubwa hivi leo, unazua hali ya kutopendezwa na mashirika ya kimataifa kwa upande wa mataifa mengi na kudhoofisha mfumo wa kimataifa kwa ujumla, na kuufanya kuwa na ufanisi mdogo katika kukabiliana na changamoto za kimataifa, Papa Francisko amesisitiza.

Papa akutana na wanadiplomasia 10 Januari 2022
Papa akutana na wanadiplomasia 10 Januari 2022

Papa amesema kuwa si mara chache kiini cha mvuto kimehamia kwenye masuala ambayo kwa asili yake yanagawanya na hayahusiani kabisa na madhumuni ya shirika na matokeo ya ajenda zinazozidi kuamriwa na wazo linalokanusha misingi ya asili ya ubinadamu na mizizi ya kiutamaduni inayounda utambulisho wa watu wengi. Papa kama alivyopata nafasi ya kuthibitisha tena katika matukio mengine, anaamini kuwa hiyo ni aina ya ukoloni wa kiitikadi, ambayo haiachi nafasi ya uhuru wa kujieleza na ambao leo hii linazidi kuchukua sura ya utamaduni huo wa kufuta, unaovamia maeneo mengi na taasisi za umma. Kwa jina la ulinzi wa utofauti, Papa amesisitiza kuwa tunaishia kufuta maana ya kila utambulisho, kwa kusababisha hatari ya kunyamazisha nafasi zinazotetea wazo la heshima na usawa wa hisia mbalimbali. Wazo moja linaendelezwa, kulazimishwa kukataa historia, au mbaya zaidi kuiandika kwa upya kwa misingi ya mitindo ya  kisasa, wakati kila hali ya kihistoria lazima itafsiriwe kulingana na asili ya wakati huo.

Diplomasia kimaitafa iwe jumuishi bila kufuta tofauti bali kuthamanisha

Diplomasia ya kimataifa kwa maana hiyo inaalikwa kuwa jumuishi na siyo kufuta lakini kuthamaisha tofauti na hisia za kihistoria ambazo zinawatambulisha watu. Kwa kufanya hivyo itawezekana kupata uaminifu na ukweli kukabiliana na changamoto zijazo ambazo zinahitaji ubinadamu wa kukutana kwa pamoja kama familia kubwa, ambayo kwa kuanzia na mtazamo wa utofauti, unakuwa na uwezo wa kupata suluhishi za pamoja kwa ajili ya wote. Ili kufanya hivyo Papa amesema inahitaji kuaminiana na uwajibikaji wa mazungumzo ikiwa ni pamoja na kusikilizana, kukabiliana, kukumbushana na kutembea kwa pamoja. Licha ya  hayo yote mazungumzo ni njia kuu ya inayofaa ili kufikia kutambua kile ambacho kinapaswa kuthibitishwa na kuheshumu ili kwenda mbali zaidi ya. Hatupaswi kusahau kuwa kuna thamani za kudumu. Si rahisi kila mara kuzitambua, lakini kuzikubali, kwani hutoa uthabiti na utulivu kwa maadili ya kijamii. Hata wakati tumezitambua na kuzikubali shukrani kwa mazungumzo na makubaliano, tunaona kwamba maadili haya ya msingi yanapita zaidi ya makubaliano yoyote. Papa amependa hasa kukumbusha haki ya kuishi, tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo cha asili na haki ya uhuru wa kidini.

Dharura ya utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja

Katika matazamio hayo, kwa miaka ya mwisho kumekuwa na kukua zaidi kwa utambuzi wa pamoja ambao unastahili dharura ya kukabiliana nayo hasa katika utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja ambayo inaendelea kuteseka kwa sababu ya utunzaji mbaya, na unyonyaji wa rasilimali zake.  Papa Francisko kutokana na hilo amefikiria nchi ya Ufilipini iliyokumbwa na kimbunga wiki iliyopita, kama  na vile nchi nyingine za Pasifiki ambazo ziko hatarini na mabadiliko hasi ya tabianchi, ambayo yanahatarisha maisha ya watu kwa sehemu kubwa wanazo tegemea kilimo, uvuvi na rasilimali asili.  Mtazamo huo kwa hakika, Baba Mtakatifu anasema unapaswa usukume Jumuiya ya kimataifa kutafuta suluhishi na kiziweka katika vitendo. Hakuna ambaye anaweza kuwa nje ya jitihada hizi kwa sababu wote wanahusuka na hatua hizo, amesisitiza. Mkutano wa hivi karibuni wa COP26 huko Glasgow, walifikia hatua fulani zenye mwelekeo hata kama ni dhaifu kulingana na tatizo kubwa la kukabiliana nalo. Njia ya kufuata kwa lengo la Mkataba wa Paris, ni ngumu na utafikiri liko mbali sana wakati muda uliopo ni kidogo, amesema Papa. Kuna haja kwa maana hiyo ya kufanya jambo kwa ajili ya 2022 ambapo utakuwa mwaka wa kuhakikisha msingi huo na kama walivyo amaua huko Glasgow kunaweza na lazima kuendelea kuongezea nguvu katika matazamio ya COP27 inayotazamiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka ujao  nchini Misri.

Mazungumzo ya udugu ili kushinda migororo ya kivita:Siria, Libia, Sudan, Sudan Kusini na Ethiopia

Mazungumzo na udugu ni mambo makuu muhimu ili kushinda mgogoro wa wakati huu. Papa Francisko amefikiriia  kwanza kabisa kuhusu Siria, ambako bado hakuna upeo ulio  wazi wa kuzaliwa kwa upya wa nchi hiyo. Hata leo watu wa Siria wanaomboleza vifo vyao, kupoteza kila kitu, na matumaini ya maisha bora ya baadaye. Marekebisho ya kisiasa na kikatiba yanahitajika, ili nchi iweze kuzaliwa upya, lakini pia ni muhimu kwamba vikwazo vilivyowekwa visiathiri moja kwa moja maisha ya kila siku, na kutoa mwanga wa matumaini kwa idadi ya watu, inayokaribia zaidi katika lindi la umaskini. Papa amesema “Wala hatuwezi kusahau mzozo wa Yemen, janga la kibinadamu ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka mingi kimya kimya, mbali na uangalizi wa vyombo vya habari na kutojali kwa Jumuiya ya kimataifa, kuendelea kusababisha wahanga wengi wa raia, hasa wanawake na watoto”. Aidha Papa amesema “Katika mwaka uliopita, hakuna maendeleo yoyote ambayo yamepatikana katika mchakato wa amani kati ya Israeli na Palestina” kwa maana hiyo Papa ni matashi na shuku  sana kuona mataifa haya mawili yanajenga kwa upya uaminifu kati yao na kuanza tena kuzungumza wao kwa wao,  moja kwa moja ili kupata kuishi katika nchi mbili wakiwa bega kwa bega, kwa amani na usalama, bila chuki na kinyongo, bali  walioponywa kwa kusameheana. Wasiwasi unakuzwa na mivutano ya kitaasisi nchini Libya; pamoja na matukio ya ghasia za ugaidi wa kimataifa katika eneo la Sahel na migogoro ya ndani ya Sudan, Sudan Kusini na Ethiopia, ambapo ni muhimu kutafuta njia ya upatanisho na amani kwa njia ya makabiliano ya kweli ambayo yanaweka mahitaji ya wakazi.

Ukosefu wa usawa, dhuluma, ufisadi na umaskini 

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amesema ukosefu mkubwa wa usawa, dhuluma na ufisadi uliokithiri, pamoja na aina mbali mbali za umaskini ambazo huchukiza utu wa watu, zinaendelea kuchochea migogoro ya kijamii hata katika bara la Amerika, ambapo migawanyiko yenye nguvu zaidi haisaidii kutatua shida za kweli na za dharura, wananchi, hasa maskini na walio katika mazingira magumu zaidi. Kuaminiana na kuwa tayari kwa makabiliano ya amani lazima kujumuishe pande zote zinazohusika ili kupata suluhishi zinazokubalika na za kudumu nchini Ukraine na Caucasus Kusini, na pia kuepusha kufunguliwa kwa machafuko mapya katika Nchi za Kibalkani, hasa Bosnia na Herzegovina. Vile vile mazungumzo na udugu ni ya dharura sana ili kukabiliana, kwa hekima na ufanisi, mgogoro ambao umeikumba  nchi ya Myanmar kwa karibu mwaka mmoja sasa, ambapo miji iliyokuwa mahali pa kukutana sasa ni eneo la mapigano, ambayo hayaheshimu hata maeneo ya ibada. Papa amebainisha kwamba bila shaka, migogoro yote inawezeshwa na wingi wa silaha zilizopo na machafuko ya wale wanaojaribu kueneza. Hi ni kutokana na kwamba wakati mwingine ni kuwa chini ya udanganyifu kwamba silaha hutumikia jukumu la kuzuia tu dhidi ya wavamizi wanaowezekana. Historia, na kwa bahati mbaya pia  hata taarifa za kila mara, zinatufundisha kwamba hivyo sivyo inavyotakiwa. Wale wanaomiliki silaha mapema au baadaye huishia kuzitumia, kwani, kama alivyosema Mtakatifu Paulo VI kuwa, “mtu hawezi kupenda akiwa na anamiliki silaha za kukera mkononi. Zaidi ya hayo, tunapojisalimisha kwa mantiki ya silaha na kuondoka kwenye zoezi la mazungumzo, tunasahau kwa huzuni kwamba silaha, hata kabla ya kusababisha wahathirika na uharibifu, zina uwezo wa kuzalisha ndoto mbaya.

Wasi wasi juu ya matumizi ya silaha zinazojiendesha pia za kinyuklia

Wasiwasi huu unafanywa kuwa halisi zaidi leo hii kwa kuwepo na matumizi ya silaha zinazojiendesha, ambazo zinaweza kuwa na matokeo ya kutisha na yasiyotabirika, wakati zinapaswa kuwa chini ya wajibu wa jumuiya ya kimataifa. Miongoni mwa silaha ambazo ubinadamu umetengeneza, ni silaha za nyuklia zinahusika sana, Papa ameeleza. Mwishoni mwa mwezi Desemba iliyopita, kwa sababu ya janga la kiafya, Mkutano wa 10 wa Mapitio juu ya Mkataba wa Kuzuia Kueneza kwa Nyuklia, ambao ulipangwa kufanyika jijini New York katika siku za hivi karibuni, uliahirishwa tena. Ulimwengu usio na silaha za nyuklia unawezekana na ni muhimu,  Papa amesisitiza.  Kwa maana hiyo ni matumaini yake kuwa jumuiya ya kimataifa itachukua fursa ya Mkutano huo ili kuchukua hatua muhimu katika mwelekeo huu. Vatican kwa maana hiyo  bado limesimama kidete kwa hoja yake kwamba silaha za nyuklia ni zana duni na zisizofaa kujibu vitisho vya usalama katika karne ya 21 na kwamba milki yao ni kinyume cha maadili. Utengenezaji wao huelekeza rasilimali kutoka katika matarajio ya maendeleo shirikishi ya binadamu na matumizi yake, pamoja na kutoa matokeo mabaya ya kibinadamu na mazingira, na kutishia uwepo wa wanadamu. Vatican inaona kuwa ni muhimu  kuanzishwa tena kwa mazungumzo huko Vienna juu ya Mkataba wa Nyuklia na Iran (Mpango Kamili wa Utekelezaji wa Pamoja) kunaweza kupata matokeo chanya ili kuhakikisha ulimwengu unakuwa salama na wa kindugu zaidi.

Nafasi msingi katika elimu kwa vizazi vipya kwa ajili ya mazungumzo na udugu

Papa Francisko amekumbusha kuwa katika ujumbe wake wa Siku ya Amani duniani,  tarehe Mosi Januari alitafuta kubainisha mambo ambayo aliona ni msingi kwa ajili ya kusaidia kukuza utamaduni wa mazungumzo na udugu. Nafasi muhimu imetawaliwa na elimu, ambayo inaunda vizazi vipya ambavyo ni matumaini na wakati ujao wa ulimwengu. Elimu kwa maana hiyo ni Injini msingi wa maendeleo fungamani ya binadamu kwa sababu inamfanya mtu kuwa huru na muajibikaji. Mchakato wa elimu ni wa pole pole ambao unahitaji kazi na kwa wakati mwingine kufanya ukate tamaa,  lakini kamwe bila kuuacha. Elimu ni kielelezo kikuu cha mazungumzo, kwa sababu kuna ukweli wa elimu ambao unahitaji muda  wa mazungumzo.  Elimu inazaa baadaye utamaduni na kujenga madaraja ya kukutana na watu. Vatican imeweza kusisitiza thamani hata kwa njia ya ushiriki waEXPO DUBAI 2020 katika Nchi za Uarabuni kwa kuanzishwa kwabanda lililoongozwa na mada ya maonesho: “Kuunganisha akili, kuunda siku zijazo”.

Kanisa katoliki linatambua na kuthamanisha nafasi ya elimu

Kanisa Katoliki daima limetambua na kuthamanisha nafasi ya Elimu kwa ajili ya kukua kiroho, kimaadili na kijamii kwa vizazi. Papa ameonesha uchungu wake kuendelea kuona kuwa baadhi ya maeneo ya elimu kama vile maparokia, shule ndimo kumekuwapo na manyanyaso ya kijinsia kwa watoto na kusababaisha matokeo mabaya ya kisaikolojia na kiroho kwa watu waliopata hali hiyo. Huo ni uhalifu ambao lazima uthibitiwe na kwa kutafuta kugundua wahusika ili wawajibishwe na kuzuia unyama huo usirudiwe katika siku zijazo. Licha ya ugumu wa vitendo hivyo, hakuna jamii inayoweza kutengua jukumu la kuelimisha. Papa ameonesha uchungu kwamba: “Ni uchungu kujua hilo, hata hivyo, ni mara ngapi, katika bajeti za serikali, rasilimali chache zimetengwa kwa ajili ya elimu. Inazingatiwa sana kama gharama, wakati ni uwekezaji bora zaidi”. Hata hivyo Papa amesema janga la kiafya limewazuia vijana wengi kupata taasisi za elimu, na kuhatarisha mchakato wao wa ukuaji wa kibinafsi na kijamii. Wengi, kwa kutumia zana za kisasa za kiteknolojia, wamepata kimbilio katika ukweli halisi, ambao huunda vifungo vikali sana vya kisaikolojia na kihemko, na matokeo ya kujitenga na wengine na ukweli unaowazunguka na kubadilisha sana uhusiano wa kijamii.

Umakini katika zana za kiteknolojia zisichukue nafasi ya mahusiano ya kweli

Kutokana na suala hili la kiteknolojia Papa amesema hamaanishi kukataa manufaa ya teknolojia na bidhaa zake, ambazo zinawezesha kuunganisha kwa urahisi zaidi na kwa haraka zaidi, lakini anakumbusha  udharura wa haraka wa kuhakikisha kwamba zana hizi hazichukui nafasi ya mahusiano ya kweli ya kibinadamu, kwa mtu binafsi, kwa ngazi ya familia, kijamii na kimataifa. Ikiwa mtu atajifunza kujitenga tangu akiwa na umri mdogo, itakuwa vigumu zaidi katika siku zijazo kujenga madaraja ya udugu na amani. Katika ulimwengu ambamo umeenea umimi, hakuna hakuna nafasi ya sisi. Jambo la pili ambalo Papa Francisko amependa kubainisha ni juu ya ajira kitu  ambacho ni muhimu kwa ajili ya kujenga na kuhifadhi amani. Ni kieleleza cha binafsi na zawadi binafsi lakini hata jitihada, ugumu, kushirikishana na wengine, kwa sababu kazi ambayo inatoa heshima na hadhi ya mtu. Katika mtazamo huo wa kijamii, kazi ni sehemu muhimu ambayo inawezekana kujifunza kutoa mchango kwa ajili ya ulimwengu wa kuishi na mzuri.

Janga kuleta jaribio gumu la kiuchumi na umaskini kikithiri

Papa Francisko katika hotuba yake amebainisha jinsi ambavyo janga la Uviko, limeleta jaribio gumu  la uchumi duniani kwa kuwaangukia juu ya familia na wafanyakazi ambao waliishi katika hali mbaya ya kisaikolojia, mapema kabla ya matatizo ya uchumi. Matatizo hayo yamewaonesha zaidi ukosefu wa usawa ambao tayari ulikuwapo kwa mantiki kijamii na kiuchumi. Kuwa kufikiria upatikanaji wa maji safi, chakula, elimu, matibabu. Idadi ya watu waliojumuishwa katika kundi la umaskini uliokithiri imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Aidha, mgogoro wa afya umesababisha wafanyakazi wengi kubadili aina ya kazi, na wakati mwingine kuwalazimisha kuingia katika uchumi wa kivuli, hivyo kuwanyima mifumo ya ulinzi wa kijamii inayotolewa katika nchi nyingi. Papa Francisko amesema katika hayo, utambuzi wa thamani ya kazi unaonesha umuhimu mkubwa kwa sababu hakuna maendeleo ya kiuchumi bila kazi na wala huwezi kufikiria mtindo mpya wa kiteknolojia unaweza kuondolea mbali thamani za pamoja zilitokanazo na kazi ya binadamu.

Kazi ni fursa ya kujigundua hadhi binafsi

Kazi ni fursa ya kujigundua hadhi binafsi, kukutana na kukua kibinadamu, ni njia mwafaka kambayo kila mmoja anashiriki kwa wuhai kwa ajili ya wema wa pamoja na kutoa mchango wadhati wa kujenga amani. Katika mantiki hilo ni lazima kushirikiana kati ya wadau wote kwa ngazi mahalia, kitaifa, Kikanda na kimataifa katika kipindi kichacho na changamoto zinazotakiwa kuwa na uongofu wa kiikolojia. Miaka ijayo itakuwa ni kipindi cha kutafuta kwa ajili ya maendeleo mapya ya huduma na mashirika ambayo yanapaswa kuongeza hupatikanaji wa kazi yenye hadhi ili kudumisha haki ya binadamu kwa ngazi zinazotakiwa kuchangia na ulinzi wa kijamii. Nabii Yeremia anakumbusha kuwa  Mungu  anasema: “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. (Yer 29:11). Kwa maan hiyo hatupaswi kuogopa kutoa nafasi kwa ajili ya amani katika maisha yetu, kwa kukuza mazungumzo na udugu kati yetu. Amani ni nzuri inayoambukiza, ambayo huenea kutoka kwa mioyo ya wale wanaoitamani na kutamani kuiishi, kufikia ulimwengu wote. Kwa kuhitimisha Papa mewabariki wao na wapendwa wao huku akiwatakia mwaka wa utulivu na amani.

10 January 2022, 17:33