Ghasia ni kubwa ya maandamano ya watu huko Kazakhstan wakati wanajeshi wakiwazuia. Ghasia ni kubwa ya maandamano ya watu huko Kazakhstan wakati wanajeshi wakiwazuia. 

Papa Francisko:Sala kwa ajili ya waathirika huko Kazakhstan

Papa Francisko anawaombea waathirika wa vurugu huko Kazakhstan kutokana na maandamano yaliyoibuka hivi karibuni.Ni matumaini kwamba wanaweza kupata maelewano ya haraka kijamii na kwa njia ya kutafuta mazungumzo ya haki na wema wa pamoja.Amekumbusha Misa ya Ubatizo wa watoto kadhaa katika Kikanisa cha Sistine Vatican na kuwaombea watoto ambao watabatizwa wakati wa kipindi hiki.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya  tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 9 Januari 2022 wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Ubatizo wa Bwana, akiwageukia mahujaji na waamini waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Francisko ameelezea uchungu kwa ajili ya waathirika wakati wa maandamano yaliyoibuka hivi karibuni huko Kazakhstan.  Kwa maana hiyo anasali kwa ajili yao na kwa ajili ya familia zao akiwa na matumaini kwamba wanaweza kupata maelewano  ya haraka ya kijamii kwa njia ya kutafuta mazungumzo, ya haki na wema wa pamoja. Amewakabidhi watu wa kazakhstan kwa Ulinzi wa Mama Malkia wa amani wa Oziornoje.

Maombi kwa watoto wachanga wamepokea au watapokea ubatizo

Papa Francisko  kawa kawaida hakusahau kuwasalimu watu wote, waamini kutoka Roma na mahujaji kutoka Italia na kutoka nchi mbalimbali. Hasa, salamu kwa  kikundi kutoka Frattamaggiore, karibu na Napoli, Italia. Akiendelea Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha tukio la Ubatizo katika Kikanisa cha Sisitine mjini Vatican asubuhi kabla ya sala  ya Malaika wa Bwana na kusema kwamba: “Asubuhi ya leo, kama kawaida katika Jumapili ya Ubatizo wa Bwana, nilibatiza baadhi ya watoto  ambao ni  watoto wa wafanyakazi wa Vatican. Ninatumia fursa hii kupanua sala zangu na baraka zangu kwa watoto wote wachanga ambao wamepokea au watapokea Ubatizo wakati huu. Bwana awabariki na Mama yetu awalinde".

Akikumbusha juu ya siku ya ubatizo

Papa Francisko amerudia tena kwa wote kuwahimiza wajifunze na kukumbuka tarehe ya ubatizo wao .” Je Nilibatizwa lini? Hii lazima msisahau na kukumbuka siku hiyo kama siku ya sherehe. Na kwenu nyote ninawatakia Jumapili njema. Tafadhali msisahau kuniombea. Mlo mwema na kwaheri ya kuonana”. Amehitimisha Papa Francisko.

TAFAKARI YA PAPA WAKATI WA SALA YA MALAIKA WA BWANA 9 JANAURI 2022
Waamini wakisikiliza tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Waamini wakisikiliza tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
09 January 2022, 14:52