Mahangaiko ya wakimbizi Mahangaiko ya wakimbizi 

Papa atuma msaada kwa wahamiaji waliozuiwa Lithuania

Kupitia Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu,Papa Francisko ametuma msaada wa Euro 50elfu kwa Caritas Vilnius nchini Lithuania ili kusaidia wahamiaji na wakimbizi walioko mpakani.Mchango wa kununua madawa,nguo,bidhaa za chakula kwa watu hao wanaoteseka kwa baridi kali ya kipindi hiki.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu kupitia Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, ametuma mchango wa Euro 50elfu kwa ajili ya Caritas Vilnius nchini Lithuania ili kusaidia shughuli kwa ajili ya mahitaji ya wahamiaji waliopo kwenye mpaka wa mashariki ya Lithuania. Kwa kushirikiana na Ubalozi wa Vatican huko Lithuania, kiasi hicho kitaweza kutumika katika shughuli za kusaidia kununua madawa, bidhaa za chakula, nguvu za joto ili kuweza kusaidia hali ya amaisha nguvu ambayo watu hao wanaishi katika baridi kali ya sasa na hali ambayo imesababaishwa kwa bahati mbaya ya mgogoro wa kiafya wa janga la uviko.

Msaada huo inatokana na kielelezo cha haraka cha hisia za ukaribu kiroho na ubaba wa kutia moyo ambapo Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi ameuonesha hata katika matamko na miito mbali mbali kwa ajili ya yao hasa mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana mwishoni mwa 2021 na mwanzoni mwa 2022 kuhusu wahamiaji, wakimbizi na waombaji wa hifadhi ambao wanajikuta katika maeneo hayo.

12 February 2022, 15:56