Papa Francisko achangamotisha vijana kuhusu vurugu zinazoharibu

Papa Francisko alizungumza zaidi ya saa moja na vijana wa vyuo vikuu vya Kaskazini,Kusini na Kati,Marekani.Janga la uhamiaji,utunzaji wa kazi ya uumbaji na Kanisa la Sinodi ni kati ya mada msingi katika maswali na majibu na vijana.Baba Mtakatifu ameshutumu vurugu ambazo zinaharibu,kama zilivyojionesha udikteta katika historia.Amemtaja Gandhi:"Ni vigumu kugeuza shavu jingine.Ukarimu ni moja ya mambo mazuri ya ubinadamu.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kutokutumia vurugu, uhamiaji, mazingira, uhusiano na wazee na teknolojia mpya na sala ya kwanza kwa Mama Maria, Malkia wa Amani ili aweze kulinda nchi ya Ukraine, familia, vijana na waathirika wa mashambulizi yaliyoanza usiku wa kuamkia Alhamisi, ndivyo Papa Francisko alianza kuzungumza kwa zaidi ya saa moja na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani yote kwa ajili ya mkutano wa Sinodi, uliokuwa unaongozwa na kauli mbiu: “Kujenga madaraja Kaskazini hadi Kusini, ambao ulifikiriwa na kuandaliwa na Kitengo cha Kitaalimungu cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Loyola huko Chicago, kinachoendeshwa na Wajesuit, kwa kushirikiana na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini.

Papa alizungumza na wanavyuo vikuu
Papa alizungumza na wanavyuo vikuu

Baba Mtakatifu Francisko akianza mazungumzo tarehe 24 Februari 2022, jioni aliwasalimia kwa salamu ya asubuhi na usiku kutegemea na masaa mbali mbali ya ulimwengu kwa wote waliokuwa wanafuatilia. Kuanzia saa 1.00 hadi 2.00 usiku na  waliendelea na majadiliano huko nyumba ya Mtakatifu Marta na majibu na mwandesha kipindi Lorena, Leo, Paco, Alejandro, Priscilla, Jefferson na vijana wengine. Hawa wote walikuwa wanatoka katika sehemu mbali mbali za Brazil, Canada, Marekani, Argentina na baadhi walikuwa na wahamiaji waliokimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine au wamehama kutoka vijijini kwenda mjini kwa kutafuta fursa ya maisha bora. Walikuwa wameounganika kwa njia mbali mbali za kisasa kuanzia na smartphone, tablet na Kompyuta. Wakiwa wamegawanyika katika sehemu nne na walisimulia Papa kwa ufupi juu ya historia zao, na walieleza dharura za Nchi zao na kuwakilisha mipango yao kwa miaka hii na ijayo.

Papa alizungumza na wanavyuo vikuu
Papa alizungumza na wanavyuo vikuu

Ujenzi wa madaraja ni sehemu fungamani ya Kikristo

Kushirikisha mawazo na mipango ya maendeleo mbali mbali katika bara la Marekani ni namna ya kujenga daraja yale kama inavyopendekeza kauli mbiu ya mkutano wao. Na Baba Mtakatifu Francisko, alizungumzia kwa dhati kuhusu madaraja, katika maneo yake ya kwanza, ambayo yalitanguliwa na salamu za Kardinali Blaise Cupich, Askofu Mkuu wa Chicago na Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Amerika Kusini (CAL), Askofu Emilce Cuda.  Baba Mtakatifu Francisko alibainisha kwamba: “kujenga madaraja  ni sehemu fungamani ya utambulisho wa kikristo. Kristo anakuja ili kujenga madaraja kati ya Baba na sisi”.

Kutojibu bila kutumia vurugu

Kwa kipindi chote ambacho vijana walikuwa wanauliza maswali, Baba Mtakatifu aliweza kuandika kwenye karatasi.  Walizungumza kwanza vijana na baadaye yeye akatoa hotuba yake kwa kuwapatia ushauri na maelekezo ya kufuata ya wakati ujao. Baba Mtakatifu amebainisha kuwa ingekuwa vizuri sana  nafasi hiyo ya Sinodi ikaweza kugeuka daima kama  ya mazungumzo kati  ya vijana wanafunzi na Baba Mtakatifu. Na baadaye alijibu swali la msichana wa Brazil ambaye alikuwa anashutumu vurugu, nguvu na za kinyama ambazo aliishi na bado zipo katika Nchi yake. Papa kwa  upande wa vurugu amebainisha kuwa lazima kujibu bila kutumia vurugu. Hii ndiyo changamoto kubwa ambayo inawasubiri vijana, kukataa vurugu. “Vurugu inaharibu, vurugu haijengi na tunaona katika udikteta wa wanajeshi na wasio wanajeshi katika mchakato wa historia. Tunahitaji unabii wa kutokutumia vurugu, kwani ni rahisi sana kupiga kofi mara tu unapopigwa kofi, kinyume ni kugeuza shavu jingine”, amesisitiza Papa na kukumbuka mfano wa Gandhi. “Ukarimu ni moja ya mambo mazuri zaidi, ambayo unazaliwa na huruma.

Unafiki unaweka sumu maisha binafsi na ukweli inagharimu

Papa akiendelea aliongeza wakati huo huo kutoa hata onyo juu ya mchezo wa “unafiki” kwamba, unaweka sumu ya maisha yako". Ukweli unagharimu na unakupeleka mbele katika uongofu wa maelewano na ulimwengu”. Katika muktadha wa maelewano, Baba Mtakatifu amezungumzia hata mtazamo wa Uumbaji, masuala ambayo yamegusiwa zaidi ya mwanafunzi mmoja. Takwimu kwa sasa zinabainisha janga kwani watu milioni 20 kwa mwaka wanakimbia nchi zao kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi; matarajio ni bilioni 1,4 ya wakimbizi wa mabadiliko ya tabia nchi, kufikia mwaka 2060. Papa Francisko ametoa mwaliko wa kutunza nyumba yetu ya pamoja na kukumbusha msemo wa kisipanyola: “Bwana anasamehe daima, sisi wakati mwingine tunasamehe, lakini asili kamwe haisamehe”.

Kupokea,kusindikiza,kuhamasisha kufungamanisha

Katika mazungumzo yao nafasi kubwa ilijikita katika mada ya uhamiaji. Ilikuwa ni hotuba ya kugusa ya mwanafunzi msichana wa Amerika Kusini aliyehama na familia yake na ambaye ameshutumu jinsi alivyotendewa. “sisi sio wabakaji, wauaji, wala dawa za kulevya… Sisi ni waota ndoto za kazi hai ambao tunatoa ubora wetu wenyewe katika Nchi hii”. Papa amejibu kwa kutumia mifano ya maneno manne, ambayo ni msingi wa kukabiliana na ambayo yanafafanua moja ya majanga makubwa zaidi katika karne yetu. “Tupo tunatazama watu ambao wanaacha ardhi zao kwa sababu ya matatizo ya kisiasa, vita, matatizo ya kiuchumi na kiutamaduni. Msingi huo ni wazi: mhamiaji lazima apokelewe, lazima kumsindikiza, kumwamasisha na kumfungamanisha”. Kama katika fursa nyingine Baba Mtakatifu amerudia tena kusema kuwa Nchi lazima wasema bila kuficha ni watu wangapi wanaweza kuwapokea na kwa kufanya hivyo nchi nyingine zinaweza kuingilia kati. Kwa njia hiyo inawezekana kuunganisha udugu wa lazima kwa ajili ya ulimwengu shirikishi.

Mada ya wahamiaji inawagusa wote

Papa Francisko amesema ni vema kusisitiza juu ya mada ya uhamiaji kwa sababu inawatazama watu wote kwa sababu wengi ni watoto wa wahamiaji. Amekumbusha juu ya maisha yake kwamba: “Mimi mwenyewe ni mtoto wa wahamiaji”, mjumbe wa familia moja ya Piemonte ambayo Baba yangu alikuwa kijana wa miaka 22 hivi”. Marekani yenyewe ni Nchi ya uhamiaji wa watu kutoka Ireland, waitaliani na hata nchi yangu Argentina ni mchanganyiko wa wahamiaji”. Suala hili kwa maana hiyo linawaalika kila mmoja kwa namna ya pekee wanavyuo vikuu ambapo Papa amesisitiza wanapaswa kukabiliana, kujifunza na kubeba matatizo kwa njia ya lugha tatu: “Kuanzia na kichwa, moyo na roho" lakini  bila kuangukia katika hatari za kugeuka baridi bila moyo”.

Mazungumzo kati ya kizazi

Baba Mtakatifu Francisko hakukosa kusisitiza juu ya mazungumzo kati ya kizazi. Neno mzizi lilikuwa ni neno lililotamkwa na kijana mmoja ambalo limemsaidia Papa kusema kuwa “moja ya mambo ya uuaji wa jamii ni pale inapo kanusha mizizi yake. Kila mmoja lazima atunze mizizi yake binafsi, kwa maana hiyo ninasisitiza juu ya mazungumzo kati ya wazee na vijana. Wazee ni mizizi,matunda yote yanatokana na mizizi. Hata wahamiaja lazima wafungamanishwe katika Nchi zinazowakaribisha, lakini wasisahau mizizi yao, la sivyo wataishi kwa kosa hilo.

Kanisa litoke nje

Kwa kuhitimisha, juu ya mada ya Sinodi, Papa Francisko hakukosa kutoa wito kwa Kanisa zima ili liwe Kanisa linalotoka nje , lisiwe Kanisa kama nyumba ya makumbusho ambayohayahamishiki, mahali ambao kila kitu ni safi na kipepangwa vizuri, wakati hakifanyi kazi. Kanisa kwa maana hiyo liwe hivyo ambalo linatambua kujiweka kwenye mjadala. Katika muktadha huo, Papa Francisko amesimulia historia binafsi, kwa miaka kadhaa alipokuwa huko barrio ya Buenos Aires  Aregentina kwamba aliona padre mmoja aliyebadili Noeli na Pasaka kwenye Parokia yake kwa kutumia  ukumbi wa chakula uliofunguliwa kwa ajili ya wahamiaji na wale ambao hawakuwa na mtu yeyote wa kufanya sherehe. Papa amesema: “Ilinishtua. Lakini hilo lilikuwa kofi usoni kwangu ambalo lilibadilisha moyo wangu.”

25 February 2022, 09:32