Papa Francisko:Ikiwa hutazami makosa yako unapanua ya wengine

Kwa bahati mbaya,kwa kutumia lugha yetu tunaweza pia kukuza hukumu,kuinua vikwazo,kushambulia hata kuharibu;kwa ulimi tunaweza kuwaangamiza ndugu.Ni katika tafakari ya Papa Francisko akiongozwa na injili ya siku ambapo Yesu anatualika kuacha unafiki na tutoe kwanza ile boriti katika jicho letu wenyewe ndipo tutakapoona vema kutoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yetu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 22 Februari 2022 akitoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican, amesema katika Injili ya siku Yesu anatualika kutafakari juu ya mtazamo na namna yetu ya kuzungumza. Kwa maana hiyo amejikita kuzungumzia juu ya “Mtazamo na kuzungumza”. Awali ya yote akiazana na juu ya  mtazamo wetu, Papa amesema hatari tuliyo nayo Bwana anasema ni ile ya kudhibiti mtazamo wetu wa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu, na kusahau boriti iliyo ndani ya jicho letu (Lk 6,41). Kwa maneno mengine, ni kuwa makini juu kasoro za wengine hata zile zilizo ndogo kama kibanzi kwa kuacha umetulia na za zako, bila kutoa uzito wowote. Ni kweli anachosema Yesu, papa amesisitiza. Saina tunapata sababu za madhaifu na makosa ya wengine na kujisawazisha sisi wenyewe. Na mara nyingi tunalalamika kwa mambo ambayo hayaendi katika jamii, katika Kanisa na katika ulimwengu bila kujikita kwanza sisi binafsi kujiwekwa kwenye mjadala na bila juhudi ya kutaka kubadilika binafsi.

Waamini na mahujaji wakisikiliza tafakari ya Papa wakati wa malaika wa Bwana
Waamini na mahujaji wakisikiliza tafakari ya Papa wakati wa malaika wa Bwana

Kila mabadiliko yenye mafaniko, chanya Papa Francisko amebainisha kuwa ni lazima yaanzie na sisi mwenyewe. Kinyume nayo,  hakutakuwa na mabadiliko. Lakini Yesu anaeleza kwa kutumia macho yetu  kuwa ni kipofu. Na ikiwa sisi ni vipofi hatuwezi kujidai kuongoza na  kuwa walimu wa wengine “kwa kuwa kipofu hawezi kuongoza kipofu mwingine”, anasema Bwana. (Lk 6, 39). Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa Bwana anatualika kusafisha mtazamo wetu. Kitu cha kwanza anatuomba tutazame ndani mwetu ili kujua madhaifu yetu. Kwa sababu ikiwa sisi hatuna uwezo wa kutazama makosa yetu, daima tutakuwa na tabia ya kupanua zaidi ya wengine. Lakini ikiwa sisi tunatambua makosa yetu na shida zetu, unafunguliwa kwetu sisi mlango wa huruma.

Na baada ya kutazama ndani mwetu, Papa ameongeza  Yesu anatualika kutazama wengine kama yeye afanyavyo, na hiyo ndiyo siri ya kutazama wengine kama Yeye afanyavyo, na kutualika kutofafuta ubaya kwa  wengine, bali wema tu. Mungu anatutazama namna hii: haoni makosa yasiyorekebika ndani mwetu, lakini anaona watoto wanaokosea. Mtazamo unabadilishwa: hauzingatii makosa, lakini kwa watoto wanaofanya makosa. Mungu daima anatofautisha makosa yake mtu. Na anamwokoa mtu daima. Mungu anamwamini mtu daima na yuko tayari daima kumsamehe na makosa yake. Tunajua kuwa Mungu anasamehe daima.  Baada ya mtazamo,  Yesu leo hii anatualika kutafakari juu ya kuzungumza kwetu. Bwana anaeleza kuwa: “kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake” Lk 6,45).

Waamini na mahujaji wakisikiliza tafakari ya Papa wakati wa malaika wa Bwana
Waamini na mahujaji wakisikiliza tafakari ya Papa wakati wa malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema, hii ni kweli kwa jinsi mtu anavyozungumza, kwa haraka unaelewa kile kilichomo moyoni mwake. Maneno ambayo tunatumia yanamfafanua mtu alivyo. Mara nyingi lakini, hatutilii umakini maneno yetu na tunayatumia kwa namna ya kijujuu tu. Lakini maneno yana uzito mkubwa: yanaturuhusu kufafanua mawazo na hisia, ya kutoa sauti za hofu tulizo nazo na mipango ambayo tunasubiri kuitimiza, ya kubariki Mungu na  wengine. Kwa bahati mbaya, hata hivyo, kwa lugha tunaweza pia kukuza hukumu, kuinua vikwazo, kushambulia na hata kuharibu; na kwa ulimi tunaweza kuwaangamiza ndugu. Haya ni masengenyo yanaumiza na kashfa inaweza kuwa kali kuliko kisu!

Sala kwa ajili ya Ukraine
Sala kwa ajili ya Ukraine

Katika siku za leo hii, hasa baada ya ulimwengu wa kidigitali, maneno yanakimbia kwa haraka, lakini yanaonesha mzunguko wa hasira, na uchokozi, huchochea habari za uongo na kuchukua fursa ya hofu ya pamoja ili kueneza mawazo potofu. Mwanadiplomasia ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mshindi wa Nobel ya Amani, alisema: “kutumia neno vibaya ni sawa na kumdharau mwanadamu” (D. HAMMARSKJÖLD, Alama za safari, Magnano BI 1992, 131). Kwa kuhitimisha tafakari yake, Baba Mtakatifu Francisko ameomba kujiuliza maswali kwa ujumla ya maneno ambayo tunatumia: maneno yanayoelezea umakini, heshima, uelewa, ukarimu, huruma, au maneno ambayo yana lengo msingi wa kujifanya wazuri mbele ya wengine? Na baadaye je tunazungumza kwa upole au tunachafua ulimwengu kwa kusambaza sumu, hasa kwa kukosoa, kulalamika, kuchochea uchokozi ulioenea? Mama Maria ambaye Mungu alimtazama kwa unyenyekevu, Bikira wa ukimya ambaye tunamwomba atusaidie kutakasa mtazamo wetu na namna ya kuzungumza.

PAPA KATIKA SALA YA MALAIKA WA BWANA

 

27 February 2022, 15:16