Papa Francisko:kukutana sio kutoa sadaka ni kuthubutu kwa ajili ya wazo&kutembea pamoja
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 11 Februari ambapo Mama Kanisa anafanya Siku kuu ya Wagonjwa Duniani sambamba na Siku kuu ya Mama Maria wa Lourdes, ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa waamini ambao wameungana pamoja kuadhimisha katika Madhabahu huko Buenos Aires. Katika ujumbe huo Papa anabainisha wao kuungana kwa ajili ya kuadhimisha siku kuu ya Mama wa Lourdes na wanafanya hija kwa maana hiyo kwa moyo na wakiomba Bikira neema kubwa sana hasa kwamba Mama uwasaidie kuwa jumuiya moja ambayo inakwenda kukutana na wote. Kuwa Jumuiya ambayo inakwenda na kila mmoja kutoka nje ili kukutana na wengine, lakini pia wajiruhusu wao wenyewe waweze kukutatana pamoja. Papa amesema hilo si suala kama kutoa sadaka bali ni kuthubutu kwa ajili ya wazo. Ni kutembea pamoja, kuondokana na kukaa na upweke na kujitenga ili kuweza kukutana na kukaa na wengine, marafiki, familia, watu wa Mungu, wote kwa pamoja katika sala mbele ya Bikira! na ili kwenda kukuta na kama jumuiya.
Ubinafsi ni mnyoo ambao unakula moyo kutoka ndani
Mkutano daima ni kujifungulia wengine, kinyume na mkutano ni kujifungia roho binafsi. Papa Francisko anaomba Mama awafaanye mioyo yao isijifungie binafsi kwa sababu ubinafsi ni mnyoo ambao unakula moyo kutoka ndani. Baba Mtakatifu Francisko anaonesha kuuungana nao katika maadhimisho hayo katika madhabahu na kusali kwa ajili yao wakati huo huo akiwaomba wasali kwa ajili yake. Ametumia Baraka zake na Yesu awabariki sana na Bikira Maria awasindikize akiwa amewashika mikono yao.
Asili ya Siku kuu ya Bikira Maria wa Lourdes
Kila mwaka huko Lourdes Ufaransa ni mahali pa kudumu kwa ajili ya hija ya wagonjwa wapatao milioni 5 ambao huomba ulinzi na faraja. Pango lililo katikati ya Milima ya Pyrenees ya Ufaransa linaibua maonesho maarufu ya Maria katika historia, yanayotambuliwa rasmina Kanisa. Tukio hilolilitokea mnamo 1858 na mhusika mkuu ni msichana wa miaka kumi na nne, Bernadette Soubirous, ambaye BikiraMaria alimtokea mara kumi na nane kwenye pango kando ya mto wa Gave. Alizungumza naye kwa lugha ya kienyeji, akamuelekeza sehemu ya kuchimba kwa mikono ili apate kitakachothibitika kuwa chanzo cha maji, kwa kugusana na miujiza mingi ingeweza kutokea. Yote yalianza Alhamisi mnamo tarehe 11 Februari 1858, wakati Bernadette alipokwenda kuchanja kuni kavu kwenye mto wa Gave, pamoja na dada na rafiki yao. Kelele kutoka msituni pangoni ilimvutia msichana ambaye Bikira alimtokea akijionesha kuwa ni Mkingiwa dhambi ya Asili na hivyo kuthibitisha kile kilichkuwa kimetamkwa na Dogma ya Mama Maria iliyotangazwa na Papa Pius IX mnamo tarehe 8 Desemba 1854, yaani miaka minne baadaye.
Mtakatifu Yohane Paulo II alianzisha Siku ya Wagonjwa duniani
Kwa sababu hiyo, tarehe 11 Februari, Kanisa linaadhimisha kumbukumbu ya Mama Yetu wa Lourdes ambaye Mtakatifu Yohane Paulo II alitaka kuihusisha Siku ya Wagonjwa Duniani. Tokeo la Lourdes lilitambuliwa rasmi na askofu wa Tarbes mnamo Februari 1862. Upesi Kanisa kubwa lilijengwa kama vile Bikira alivyoomba. Lourdes mara moja ikawa maarufu zaidi wa maeneo ya Maria. Ofisi maalum (le Bureau medical) iliwekwakuchunguza kisayansi uponyaji ambao ulianza kutokea mara moja wa kimiujiza. Karibu miujiza sabini imetambuliwa hadi sasa, lakini kiukweli ni mingi zaidi ya iliyotambuliwa na zaidi kuna uongofu wa wengi zaidi.