Papa Francisko:Ulimwengu uwe wa kikristo lakini zaidi wa kibinadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video katika fursa ya miaka 70 ya tangu kuanzishwa kwa Harakati kwa ajili ya Ulimwengu Bora, Alhamisi tarehe 10 Februari 2022 kwa kuwaelezea ukaribu wake katika kuadhimisha siku hiyo tangu kuundwa kwa Harakati hiyo (Movimento per un Mondo Migliore). Papa Francisko anawaeleza jinsi ambavyo wamefanya kazi sana kwa miaka 70. Yalikuwa ni maono ya maisha, maono ya uumbaji. Kwa kufafanua amesema Papa Pio XII alikuwa anazungumzia juu ya mabadiliko. Aliweze kusema kwa kutumia hata neno kama “poli”, yaani ulimwengu wa kipoli, ambao unapaswa kuwa wa kibinadamu zaidi, kikristo zaidi lakini zaidi kibinadamu, kwa sababu Bwana daima yuko karibu na mwanadamu.
Kufanya kazi kwa wajili ya watoto, wazazi na amani
Papa Francisko amewatia moyo waendelee mbele bila kukata tamaa, waendelee kufanya kazi kwa ajili ya mabadiliko hayo ulimwenguni. Papa amesisitiza kwamba wafanye kazi kwa ajili ya haki, ya watoto, kwa wazee na kwa ajili ya amani. Papa Francisko amesema “Ni ulimwengu ulio bora ambao tunauhitaji, uwe ulimwengu wa amani.” Amewashukuru na kuwatakia matashi mema huku akiwapongeza kwa siku hiyo ya kuzaliwa kwa Harakati yao. Amewaomba kusali kwa ajili yake na kama afanyavyo yeye. Bwana awabariki na Mama awalinde.