Moja ya ziara za kitume za Papa. Moja ya ziara za kitume za Papa.  

Papa Francisko anatarajia kufanya ziara ya kitume huko Malta,2-3Aprili

Leo Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imetoa tangazo juu ya safari ,ambayo tayari ilikuwa imepangwa kufanyika mnamo tarehe 31 Mei 2020,na kuahirishwa kwa sababu ya janga la UVIKO. Papa atatembelea miji ya Valletta,Rabat,Floriana na kisiwa cha Gozo huko Malta.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe iliyokuwa imepangwa 31 Mei 2020, na baadaye  ikaahirishwa kwa sababu ya kuzuka kwa janga la UVIKO -19, Papa Francisko hakati tamaa ya kutembelea kisiwa cha Malta. Na kwa maana hiyo tarehe 10 Februari 2021 limetolewa tangazo rasmi kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican kwamba:  Papa atasafiri hadi kisiwa cha Mediterania kwa siku mbili, kuanzia tarehe 2 na 3 Aprili ijayo. Katika maelezo ya Msemaji Mkuu wa Vyombo vya Habari Vatican Dk. Matteo Bruni, amesema  kwamba Papa: “alikubali mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Malta, mamlaka na Kanisa Katoliki ya nchi. Maelezo zaidi  yatatangazwa hivi karibuni, lakini wakati huo huo imeelezwa kuwa Papa Francisko atatemebelea hata katika mji mkuu wa Valletta, pia atakuwa huko Rabat, Floriana na katika kisiwa cha Gozo, ambacho ni cha pili kwa ukubwa kati ya Visiwa vya Malta ambacho kimetangwa na mkono wa bahari ya kilomita 5 tu.

Kisiwa kile cha Malta, ni kiti cha kale cha Agizo la Chivalric leo hii kina wakaazi chini ya elfu 500, zaidi ya asilimia 90% yao wakiwa Wakatoliki, na kwa maana hiyo itakuwa ziara yake ya 36 ya kitume ya Jorge Mario Bergoglio, yaani Papa Francisko baada ya ile ya mwisho, mwezi Desemba alipotembelea Cyprus na Ugiriki. Atakuwa Papa wa tatu katika kipindi cha miaka thelathini kutembelea kisiwa cha Mediterania: kabla yake Papa Yohane Paulo II alikwenda huko mnamo 1990 na 2001, mara hii ya mwisho akatangzwa mwenyeheri Dun Ġorġ Preca, mtakatifu wa kwanza wa Malta katika historia ya Ukatoliki, Mtawa Adeodata Pisani, aliyekuwa mwanzilishi wa nyumba ya watawa wa Mtakatifu Pietro katika mji wa Madina, na Nazju Falzon, Ndugu mdogo ambaye aliyewasaidia askari wa Malta wakati wa Vita vya Crimea. Papa Benedikto XVI, yeye alikwenda Malta mnamo tarehe 17 - 18 Aprili 2010, kusherehekea kumbukumbu ya miaka 1950 ya ajali ya meli ya Mtakatifu Paulo katika kisiwani humo mwaka 60 BK.

Papa Francis alikuwa tayari amesisitiza nia yake ya kutembelea kisiwa hicho katika mahojiano na redio ya Uhispania ya Cope (intervista alla radio spagnola Cope.)  Mwaliko rasmi wa kwenda nchini humo ulikuja miaka mitatu iliyopita kutoka kwa Rais George Vella, wakati wa ziara yake mjini Vatican mnamo tarehe 16 Septemba 2019. Katika tukio hilo, kiongozi huyo wa Malta alikumbuka uhusiano wa kale kati ya Papa na visiwa vya Mediterania, akimaanisha Papa kwamba mamlaka ya kiraia na kidini ya Malta yalikuwa yakingoja kuwasili kwake kwa muda na kukumbuka ziara ya mara mbili ya Karol Wojtyla. Miezi miwili baadaye, mnamo Desemba 2019, mkutano wa faragha uliopangwa kwa muda na Waziri Mkuu ambaye tayari alikuwa amejiuzulu Joseph Muscat ulifuata usikilizaji huo.

10 February 2022, 16:07