Papa Francisko:Tuepushe na vita hivi vya kikatili

Papa Francisko ameongoza ibada ya toba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,ambapo mara baada ya maadhimisho hayo,amesali sala ya kuiweka wakfu nchi ya Urussi na Ukraine kwa maombezi ya Moyo Safi wa Bikira Maria.Katika tukio hili alisindikizwa na ulimwengu wote,kwenye madhabahu ya kimataifa,makanisa makuu na watu wote wenye mapenzi mema.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Kupashwa Habari Mama Bikira Maria, tarehe 25 Machi na katika siku maalum ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Ibada ya Toba imefuata tendo la  kuiweka wakfu nchi ya Urussi na Ukraine kwa maombezi ya Moyo Safi wa Bikira Maria. Tendo hilo lilifuatiliwa na Madhabahu mbali mbali kuanzia Fatima huko Ureno, hadi Kibeho, Rwanda,Ivory Coast, Tanzania, Mexico, Brazil na nchi nyingine nyingi. 

PAPA AKIUNGAMA
PAPA AKIUNGAMA
PAPA AKIUNGAMA
PAPA AKIUNGAMA

Madhabahu ya Mama Yetu wa Fatima huko Ureno alikuwapo mwakilishi wa Baba Mtakatifu Kardiali Konrad Krajewski, msimamizi wa Sadaka ya Kitume ya Papa. “Mama wa Mungu, tunakukabidhi na kujiweka sisi wenyewe wakfu kwa Moyo wake safi, Kanisa na ubinadamu wote, kwa namna ya pekee Urussi na Ukraine, chambua chuki, ondoa visasi na kutufundisha msamaha”, ni maneno yaliyosika wakati Baba Mtakatifu anaweka wakfu, sala ambayo imetumwa ulimwenguni kote kwa tafsiri za lugha mahalia.

KUWEKA WAKFU KWA MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA
KUWEKA WAKFU KWA MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA

Baba Mtakatifu alikuwa peke yake, amekaa kwenye kiti mbele ya picha ya Bikira Maria wakati akisihi  mama kuhusu hali ya wakati huu ambayo inayumbisha dunia. Hakika ilikuwa ni hali ya aina yake ambayo utafikiri Baba Mtakatifu amerudi kubisha hodi kwenye milango ya nyumba ya mama Maria. Na  Nyuma yake, katika hali hiyo hakua peke yake kulikuwa na ulimwengu wote ambao umeandika ukurasa mwingine wa Historia ya Kanisa la sasa ambalo ni uliwengu wote.

IBADA YA TOBA
IBADA YA TOBA
WAAMINI KATIKA KATIKA KANISA KUU LA MTAKATIFU PETRO
WAAMINI KATIKA KATIKA KANISA KUU LA MTAKATIFU PETRO

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, lilikuwa linajumuisha mabara yote matano na kupitia vyombo vya habari, katika viwanja mbali mbali, hata huko Ukraine ambayo imeharibiwa na vita, kama Kiev hadi Odessa, au Uwanja wa Mtakatifu Petro ambao ambao umewaona melfu ya watu wakiomba na Baba Mtakatifu.

PAPA AKIWA ANASALI MBELE YA PICHA YA MAMA MARIA
PAPA AKIWA ANASALI MBELE YA PICHA YA MAMA MARIA
IBADA YA TOBA NA KUWEKA WAKFU KWA MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA
IBADA YA TOBA NA KUWEKA WAKFU KWA MOYO SAFI WA BIKIRA MARIA

 

25 March 2022, 19:07