Papa:Kwa Mungu hakutoki maovu,ni huruma,ukaribu na upole!

Ni lazima kuwa makini,hasa maovu yanapotukandamiza kwani kuna hatari ya kupoteza mwanga na kujikuta unapata jibu rahisi,ambalo ningumu kujieleza,tunaishia kumpa makosa Mungu.Na mara nyingi tuna tabia mbaya ya kukufuru.Kwa Mungu hakutoki ubaya kwa sababu hakututenda sawa sawa na hatia zetu,Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu bali kwa kadiri ya rehema zake.Mtindo wa Mungu ni huruma,ukaribu na upole.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake Dominika ya Tatu ya Kwaresima kwa kuongoza na Injili ya Luka sura ya 13, 1-9, ameanza kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 20 Machi 2022 kwamba " Tupo katikati ya safari ya Kwaresima na leo Injili inamwakilisha Yesu ambaye anatoa  habari za wakati ule. Wakati kumbu kumbu ilikuwa bado ni hai ya wale watu 18 waliokuwa wamekufa kutokana na kuangukiwa mnara: "Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha Yesu habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichangaya damu yao na dhabihu zao".  (Lk 13,1). Kuna swali ambalo utafikiri linasindikiza janga la habari hizi: Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Na Mungu aliwapa adhabu? Ni maswali ambayo yanarudi daima na sasa; tunapoona habari nyeusi zinazotukandamiza na kutufanya tuhisi tusio na nguvu mbele ya maovu, mara nyingi tunaijiwa na swali la kujiuliza; je hii inawezekana ikawa adhabu ya Mungu? Ni Yeye anayetuma vita au Uviko ili kutuadhibu na dhambi zetu? Na kwa nini Bwana haingilii kati?

Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Baba Mtakatifu Francisko hata hivyo amebainisha kwamba lazima kuwa makini, hasa maovu yanapotukandamiza kwani kuna hatari ya kupoteza mwanga na kujikuta unapata jibu rahisi, ambalo ni ngumu kujieleza, tunaishia kumpa Mungu makos. Papa ameongeza “mara nyingi hutokea na kwa matani tuna tabia mbaya ya kukufuru”. Ni mara ngapi tunaweka makosa juu yake hata makosa yetu na tunayaweka  matendo ya ulimwengu kwake na  ambaye kinyume chake anatuacha daima huru na ndiyo maana  haingilii kati kamwe badala yake Yeye hupendekeza tu: Kwake yeye ambaye hatumii vurugu badala yake anateseka kwa ajili yetu na anateseka na sisi!  Yesu kwa hakika anakataa na anapinga kwa nguvu mawazo ya kuhukumu Mungu kwa sababu ya mabaya yetu: Watu wale  ambao waliuawa na Pilato na kifo chini ya mnara hawakuwa na dhambi kubwa zaidi ya wengine na wala la siyo waathirika kwa Mungu asiye na huruma na mlipiza kisasi ambacho hakipo! Kwa Mungu haiwezekani kutoka ubaya kwa sababu hakututenda sawa sawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. (Zaburi 103,10) bali kwa kadiri ya rehema zake. Ni mtindo wa Mungu. Hawezi kamwe kufanya hivyo, bali daima anatujali kwa huruma.

Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Lakini badala ya kumpa Mungu makosa,  Yesu anasema lazima kutazama nyuma: dhambi ambayo inazalisha kifo, ni ubinafsi wetu ambao unachanachana mahusiano; ni chaguzi zetu mbaya na nguvu zinazosababisha uovu. Kwa maana hiyo Bwana anatoa fursa ya kweli ya kupata  suluhisho, la uongofu na kusema: “lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo(Lk 13,5). Ni mwaliko msingi hasa katika kipindi hiki cha Kwaresima, amesisitiza Papa. Tuupokee kwa moyo uliowazi. Tuongoke dhidi ya maovu na kukataa dhambi ambayo inatudanganya, tujifungulie mantiki ya Injili, kwa sababu mahali panapo tawala upendo na udugu, ubaya hauna nguvu tena!  Lakini Yesu anajua kuwa kuongoka sio rahisi, na hivyo anataka kutusaidia kwa hili ambako mara nyingi tunaangukia katika makosa yale yale na dhambi zile zile: tunatia bidii lakini utafikiri juhudi zetu za wema zinakuwa bure katika ulimwengu ambao unatafikiri umetawala ubaya. Na kwa maana hiyo basi baada ya wito wake, tutiwe moyo kwa neno ambalo anasimulia kwa uvumilivu wa Mungu kwetu sisi. na lazima kufikiria uvumilivu wa Mungu alio nao kwetu sisi”, Papa amesisitiza.

Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Bwana anatupatia sura ya kufariki kwa kutumia mti wa mtini ambao hautoi matunda kwa wakati uliopangwa, lakini haukatwi; kwani anatoa muda mwingine yaani fursa nyingine.  Papaameongeza kusema anavyopenda kufikiri jina zuri ambalo angeweza kumwita Mungu: ''Mungu wa uwezekano mwingine”. "Yeye anatupatia fursa nyingine daima na ndiyo huruma yake. Ndivyo anafanya Bwana kwetu. Yeye hakatishi upendo wake, wala hakati tamaa, hachoki kutupatia imani kwa huruma". Baba Mtakatifu Francisko amesema "Mungu anatuamini, Mungu anaimani na sisi na kutusindikiza kwa uvumilivu. Uvumilivu wa Mungu upo pamoja nasi".

Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Bwana hakati tamaa, bali anatoa daima matumaini ndani mwetu. Mungu ni Baba na anatutazama kama baba, kama alivyo baba bora, ambaye hatazami matokeo ambayo bado hajatimizwa, lakini matunda ambayo yanaweza bado kuonekana; yeye ahesabu makosa yetu, lakini anatutia nguvu na uwezekano; hatazami wakati wetu uliopita, lakini anathubutu kuwa na imani ya wakati ujao. Kwa sababu Mungu yuko karibu nasi.  Mtindo wa Mungu ni ukaribu, Mungu ni karibu na huruma na upole. Kwa njia hiyo anatusindikiza na tusisahau hilo kuwa Ukaribu, huruma na upole ndiyo mrindo wa Mungu”. Tuombe kwa maana hiyo Bikira Maria ili atupatike matumaini na ujasiri na kuwasha ndani mwetu shauku ya uongofu.

TAFAKARI YA PAPA KABLA YA SALA YA MALAIKA WA BWANA 20 MACHI 2022
20 March 2022, 13:53