Mpakani mwa Moldavia Juu ya daraja la wokovu confine moldavo file sul ponte della salvezza Mpakani mwa Moldavia Juu ya daraja la wokovu confine moldavo file sul ponte della salvezza 

Papa Francisko kwa vijana:vita ni jaribu,tuondokane navyo kwa pamoja

Katika ujumbe kwa njia ya video,Papa anawashauri vijana wa kike na kiume wanaojiandaa kwa Siku ya Vijana (WYD )2023 huko Lisbon,Ureno,kuwa na ujasiri wa kuondokana na mgogoro kwa kutumia ubunifu na mashairi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ametazama wakati mgumu wa kihistoria tunaoupitia, katika ujumbe kwa njia ya video kwa lugha ya Kihispania kwa vijana wanaohusika katika maandalizi ya Siku ya Vijana Ulimenguni(WYD) 2023, ambayo itafanyika huko Lisbon kuanzia tarehe 1 hadi 6 Agosti. Ni katika ujumbe uliorekodiwa na Askofu Américo Manuel Aguiar, Askofu msaidizi wa Lisbon, na rais wa Mfuko wa Siku ya Vijana Ulimwenguni ( WYD) Lisbon 2023, aliyekutana na Papa tarehe 3 Machi 2022, akibainisha juu ya mgogoro uliopo wa kuweza kuondoka ndani yake.

Vita ni moja ya maovu mabaya sana 

“Tumetoka kwenye mzozo wa janga la uviko, tumeingia kwenye mzozo wa kiuchumi na sasa, tuko kwenye mgogoro wa vita, ambao ni moja ya maovu mabaya zaidi ambayo yanaweza kutokea! Kwa maana hiyo mwaliko wa Papa Francisko ni kuufanya mkutano wa vijana uwe  hai, kuufanya kuwa safi na ubunifu na sio katika kivuli cha matukio mengine ya Siku ya Vijana Ulimwenguni(WYD). Papa Francisko amemnukuu Mwenyeheri Carlo Acutis kutukumbusha kwamba tumeitwa kuwa asili na sio nakala.

Migogoro inatujaribu ili tweze kuwa bora

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba katika “Migogoro unashindwa kwa kuwa pamoja na sio kujitenga. Na migogoro inatujaribu ili tuweze kutoka walio bora zaidi. Katika mgogoro hatuwezi kutoka sawa ama tunatoka tukiwa bora au vibaya zaidi. Na changamoto tunayokabiliana nayo ni kuweza kutoka humo tukiwa vizuri zaidi”, Papa Francisko amesisitiza katika ujumbe wake kwa njia ya video.

Tengeneza shairi la ubunifu kuelekea Agosti 2023

Papa Francisko ameomba vijana ikiwa wanataka kuwa bora amesema kwamba "ninyi ni wabunifu, washairi!” kwa maana hiyo mwaliko wake ni kutengeneza shairi la ubunifu linalotazama mwezi Agosti 2023”. Hatimaye, Papa anaomba sala, akiwahakikishia sala yake mwenyewe kwa ajili ya vijana watakaoshiriki na ili iwe ni mkutano wenye matunda ambao wanaweza kutokea vizuri zaidi kuliko jinsi watakavyo kuwa wamefika.

07 March 2022, 17:32