Tafuta

03-04-2022 Ziara ya Kitume ya Papa Francisko, Malta - Misa Takatifu katika Uwanja wa Granai, huko Floriana. 03-04-2022 Ziara ya Kitume ya Papa Francisko, Malta - Misa Takatifu katika Uwanja wa Granai, huko Floriana.  Tahariri

Evangelii gaudium na umuhimu wa imani

Maneno ya Papa Francisko katika Kanisa la Malta na sentensi iliyorudiwa mara saba.

ANDREA TORNIELLI

Mbele ya watu elfu tatu waliokusanyika mahali patakatifu kwenye madhabahu ya Ta 'Pinu katika kisiwa cha Malta na Gozo, siku ya Jumamosi jioni Papa Francisko alizungumza kuhusu mambo muhimu ya imani. Na chaguo lake la kuongeza katika maandishi yaliyo tayarishwa maneno  ya “Furaha ya Kanisa ni kuinjilisha” yalikuwa ya kushangaza. Papa Francisko hakurudia mara moja tu, lakini mara saba. Mwishoni mwa kila aya alirudia kwamba hiyo ndiyo furaha ya Kanisa, kuinjilisha. Ni Evangelii gaudium, Wosia wake wa mwezi Novemba 2013, ambao unawakilisha ramani ya mchakato wa njia ya upapa wake. Kurudi kwenye asili, alielezea Papa Francisko, sio shauku ya kupiga mbizi isiyowezekana katika siku za nyuma zilizo mbali sana, wala ukamilifu wa enzi ambazo hazitarudi kamwe. Kurudi kwenye asili kunamaanisha kurudi katika umuhimu, yaani, kurejesha roho ya jumuiya ya kwanza ya Kikristo, kurudi kwenye moyo wa imani. Na moyo wa imani ni uhusiano na Yesu na utangazaji wa Injili yake kwa ulimwengu wote. Hiyo tu ndiyo muhimu.

Kwa hiyo, wasiwasi wa Kanisa hauwezi na haupaswi kuwa utukufu wa jumuiya na wahudumu wake, hauwezi na haupaswi kuwa ushawishi wake wa kijamii, yaani “kuhesabu”, “kuinuliwa  juu ya dunia, katika jamii na katika maeneo ya madaraka. Utafutaji wa nafasi na tahadhari hauwezi na haipaswi. Wala haiwezekani kuwa na uboreshaji wa ibada, sherehe kamilifu zinazohatarisha kugeuka kwa kile ambacho Joseph Ratzinger alikifafanua kama: “ukumbi mtupu”. Kutotulia kwa tangazo na ushuhuda, kujaribu kila njia iwezekanayo ili kuhakikisha kwamba wanaume na wanawake wa wakati wetu wanakutana na Yesu aliye hai, hilo ndilo lililowachochea wafuais wa Mnazareti na kuwatia moyo wale wanao ishuhudia Injili leo hii. Kwa sababu furaha ya Kanisa ni kuinjilisha, yaani kueneza furaha ya ujumbe wa Kikristo.

Ni muhimu kwamba miaka tisa baada ya kuchaguliwa kwake kama Askofu wa Roma, Papa Fransisko bado anarudi katika Wosia wake wa Evangelii gaudium, ujumbe wake muhimu lakini usioeleweka sana. Ujumbe ambao umepata upinzani, lakini ambao pia umehatarisha na kuhatarisha kubadilishwa kuwa kauli mbiu na wale wanaorudia kuukaribisha. Kwa hiyo pia utangazaji wa Injili unaishia kunaswa katika vyombo vya habari, na kunaswa ndani ya miundo na mikakati ya masoko ya kidini. Hata katika mchakato wa njia ya sinodi ambayo Papa alitamani sana kwa ajili ya Kanisa zima haujaachwa katika hatari hiyo, ile ya “kusawazishwa kwenye ukawaida” katika urasimu wa kikanisa badala ya kuwa hatari, uwazi, kusikiliza kila mtu huku ikitoa msukumo wa upyaisho wa kimisionari.

Kuna ramani inayorudisha katika  mwanga alieleza Papa Francisko ili kuthibitisha jinsi Kanisa linavyoingiliwa na roho ya Injili. Na ni kukaribishwa, kujitwika mzigo wa mateso bila malipo. Kwa waamini wa Malta, kisiwa cha “bandari salama” kwa karne nyingi, na mahali pa kutua ambapo Mtakatifu  Paulo alifika na ambapo Wakristo wa kwanza walitendewa“kwa ubinadamu adimu”, Papa alikumbusha: “Hatuwezi kukaribisha kila mmoja peke yake; katika kivuli cha Makanisa yetu mazuri, huku nje kaka na dada wengi wakiteseka na kusulubiwa kwa maumivu, taabu, umaskini na vurugu”.

Maneno ambayo yanalingana na yale ya Baba wa Kanisa Mtakatifu Yohana Chrysostom, ambaye katika moja ya mahubiri yake maarufu alisema: “Je, unataka kuuheshimu mwili wa Kristo? Usimruhusu kuwa kitu cha kudharauliwa katika viungo vyake, yaani, katika maskini, bila nguo za kujifunika. Usimheshimu hapa kanisani na vitambaa vya hariri, wakati nje unampuuza wakati anateseka kwa baridi na uchi”. Leo, kama miaka elfu mbili iliyopita, ni ramani hiyo ya kurudisha katika mwanga na kujiuliza.  

03 April 2022, 17:49