Hija ya Kitume ya Papa Francisko Malta:Amefika Malta katika ziara ya 36 ya kitume!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Upepo mkali wa Bahari ya Mediterania ulikaribisha kuwasili kwa 'Papa Frangisku' hili ndilo jina lake katika lugha ya ndani ya kisiwa cha Malta, katika visiwa vilivyochaguliwa na Baba Mtakatifu kama marudio ya safari ya 36 ya kitume ya Papa. Hija hii ni fupi lakini nzuri ya chini ya masaa arobaini na nane hivi, kama Papa mwenyewe alivyothibitisha katika ndege, ambapo, akiwasalimu waandishi wa habari walioandamana naye,alisema kwamba wazo la safari ya kwenda Kiev ni pendekezo kwenye meza yake.
Akiwa Vella, Papa Francisko ametembea katika zulia jekundu hadi Sebule ya Rais na wenyeji wake na Sebule ya Waziri Mkuu wa Mchi. Muda mfupi baadaye alipelekwa na gari hadi Ikulu huko Valletta.
Umati mkubwa waliimba, huku wakipiga kelele na vigelegele: “Papa Francis, Papa Francis!” Ziara ya heshima imefanyika kwa rais, ambaye, pamoja na mke wake, waliongozana na Papa kwenye Chumba cha mapokezi ambapo wabadilishana zawadi. Pia hapa kumefanyika mkutano mfupi wa faragha na Waziri Mkuu Robert Abela na familia yake, ambapo mwisho wake mkutano umepangwa, katika Chumba cha Baraza Kuu, na mamlaka na wanadiplomasia. Hapo itakuwa ni hotuba ya kwanza.